Sunday, January 24, 2016

WAZIRI NAPE AWATAKA WASANII KUFANYA KAZI ZENYE UBORA


MAMBO YA UZINDUZI WA CHANELI 294 CLOUDS PICHANI
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akipiga gitaa kwenye sherehe za uzinduzi wa Chaneli 294 itakayokuwa inapatikana kwenye king'amuzi cha DSTV.
Waziri Nape aliwataka wasanii nchini kufanya kazi zenye ubora kwani zitaangaliwa na mataifa zaidi ya 11.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza na wasanii wa tasnia ya filamu Tanzania walipokutana kwenye uzinduzi chaneli 294 ya Clouds itakayo patikana kwenye DSTV.

Friday, October 30, 2015

MKURUGENZI WA UCHAGUZI JIMBO LA ILEMELA AMTANGAZA BI.AGELINE KUWA MBUNGE MTEURE WA JIMBO LA ILEMELA

Mkurugenzi wa Uchaguzi Jimbo la Ilemela amemtangaza rasimi Bi,Angeline Mabula kuwa mbunge anayesubili kuapishwa ili kuanza kutekeleza majukum ya mbunge ndani ya jimbo la Ilemela


 Bi.Angeline akikabidhiwa cheti cha ushindi
 Bi.Angeline akupeana mkono na Mkurungenzi wa uchagauzi
 Mkurugenzi wa Uchaguzi akiwapungiz mkono wananchi mara baada ya kumaliza kumkabidhi cheti cha ushindi Bi.Angeline

Ni Mbunge mteule wa Jimbo la Ilemela akiwaonesha wananchi waliomchagua cheti cha ushindi alichokabidhiwa na mkurugenzi wa uchaguzi.

Sunday, October 11, 2015

MAMA SAMIA AMALIZA KAMPENI MKOA WA MWANZA NA KUANZA SHINYANGA KWA KISHINDO KLEO


MGOMBEA MWENZA WA URAIS KWA TIKETI YA CCM, MAMA SAMIA SULUHU HASSAN, AKIWA KATIKA KIVUKO CHA MV MISUNGWI, WAKATI AKITOKA MWANZA KWENDA SENGEREMA MKOANI HUMO, KUENDELEA NA KAMPENI LEO

 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akiwasalimia wananchi (Hawapo Pichani) aliosafiri nao katika Kivuko cha Misungwi, wakati akienda Sengerema kutoka jijini Mwanza, kwenda Sengerema kuendelea na kampeni zake leo 
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama samia Suluhu Hassan (wapili kushoto), akiwa katika Kivuko cha mv Misungwi, wakati akitoka jijini Mwanza kwenda sengerema kuendelea na kampeni zake leo. Kushoto ni Mjumbe wa Kamati ya Kampanei za CCM Kitaifa, Christopher Ole sendeka na watatu pia Mjumbe wa kamati hiyo, Angela Kizigha na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza Baraka Konisaga ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa mkoa wa Mwanza
 Wananchi wakimsubiri kwa hamu Mgomea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan wakati Kivuko ca Mv Misungwi kilipokuwa kiliwasili katika eneo la Busisi wilayani Sengerema mkoani Mwanza
 
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akijiandaa kutoka katika kivuko cha Mv Misungwi, baada ya kuwasili Busisi wilayani Sengerema mkoa wa Mwanza leo
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akilakiwa na Mkuu wa wilaya ya Sengerema, alipowasili kwenye Kivuko cha Busisi,wilanai humo leo
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akiwasalimia wananchi wakati akitoka kwenye Kivuko cha mv Misungwi baada ya kuwasili Busisi wilayani Sengerema leo
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM,Mama Samia Suluhu Hassan akizungumza na baadhi ya wananchi waliomlaki eneo la Busisi baada ya kushuka katika Kivuko cha Mv Misungwi leo
 Msafara wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan ukenda katika jimbo la sengerema mkoani Mwanza leo











Kina Mama wakimshangilia Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan wakati akipita kwenye Kijiji kimoja wakati msafara ukienda Jimbo la Sengerema mkoani Mwanza leo
Wananchi wakiwa wameusimamisha msafara wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM Mama Samia Suluhu Hassan katika eneo la Nyasenga, wakati ukienda Sengerema mkoani Mwanza leo
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM,Mama Samia Suluhu Hassan, akihutubia wananchi katika mkutano wa kampeni aliofanya katika jimbo la Sengerema mkoani Mwanza leo
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akimnadi Mgombea Ubunge jimo la Sengerema, William Ngeleja wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo hilo leo
Baadhi ya wagombea Udiwani katika jimbo la Sengerema, mkoani Mwanza wakiwasalimia wananchi waliponadiwa na Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo hilo leo
Magombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akihutubia umati wa wananchi katika mkutnao wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Buchosa mkoani Mwanza leo













Umati wa wananchi ukimshangilia Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM,Mama Samia Suluhu Hassan alipouhutubia kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Buchosa mkoani Mwanza
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akimnadi Mgombea Ubunge jimbo la Buchosa, Charles Tizeba, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo hilo mkoani Mwanza
Baadhi ya wagombea Udiwani katika jimbo la Buchosa, wakisalimia wananchi baada ya kunadiwa na mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo hilo leo
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika Uwanja wa Sabasaba, eneo la Maganzo katika jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga leo
Wananchi wakimshangilia mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga 
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akimkabidhi  kitabu cha Ilani ya CCM, Mgombea Ubunge jimbo la Kishapu Suleiman Nchambi baada ya kumnadi katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo hilo mkoani Shinyanga leo
Mgombea  Ubunge jimbo Shinyanga mjini Steven Masele akiomba kura kwa wananchi wakati wa mkutano wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM uliofanyika leo kwenye Viwanja vya Chuo Cha Biashara mkoani Shinyanga leo
Wananchi wakishangilia wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Shinyanga mjini mkoani Shinyanga
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akimnadi Mgombea bunge jimbo la Shinyanga Mjini, Steve Masele, katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo hilo. 

Saturday, August 23, 2014

TANZANIA 11 YAAMBULIA KICHAPO CHA 1-3 DHIDI YA WAGEN REAL MADRI


VS

TUNATANGAZA UTALII WA NDANI: FAHAMU HIFADHI YA TAIFA YA ZIWA MANYARA



Ndege wakiwa katika Hifadhi ya Taifa ya Manyara
 Baadhi ya Nyani  wakiwa katika Hifadhi ya Taifa ya Manyara



Tembo wakiwa katika Hifadhi ya Taifa ya Manyara

Picha zote na Francis Godwin

Hifadhi ya Ziwa Manyara ni maarufu sana nchini Tanzania kwa simba wanaopanda miti. aina hii ya simba hupatikanandani ya hifadhi hii pekee barani Afrika. Umaarufu wa hifadhi Ziwa manyara unaongezeka kila siku kutokana na kukua kwa utaliiwa ndani ambapo wananchi wengi kutoka katika mikoa ya kaskazini mwa Tanzania hupenda kutembelea hifadhi hii.
  • Hifadhi hii ipo ndani ya Bonde la Ufa ambalo kingo zake zinaongeza mandhari zaidi. Ziwa Manyara lililo ndani ya hifadhi ni kivutio kikubwa kwa watalii kutokana na wingi wa ndege aina yakorongo walio na mvuto mkubwa kwa kila mtu. Ndege hao huonekana kama pazia kubwa jeupe nyakati za mchana wanapokuwa ziwani kujipatia chakula na mapumziko.
  • Vilevile , umaarufu wa hifadhi ya Ziwa Manyara unakua kutokana na wingi wa wageni wanaotoka nje ya nchi. Idadi kubwa ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali nchini Tanzania hutembelea hifadhi hii kujionea maajabu ya dunia hasa viumbe wa porini, wanyama, mimea na ndege.
  • Wanyama wanaopatikana ndani ya hifadhi hii ni pamoja na simba, nyati, tembo, nyani, chui, pundamilia na wanyama wengine wanaokula majani. hifadhi hii pia inasifika kwa wingi wa wake wa ndege hasa heroe na mnandi ambao huonekana katika makundi makubwa na kufanya eneo hili la utalii kuwa na aina 400 za ndege wanaovutia.

  • Mji mdogo wa Mto-wa-Mbu ni kituo kikubwa cha biashara kinachotoa huduma kwa wageni wanaotembelea hifadhi ya Ziwa Manyara.Mji huu mdogo upo karibu na lango la hifadhi.Chemchem za maji moto ni maajabu mengine ndani ya hifadhi hii. Maji hayo yanayobubujika kutoka ardhini huonekana yakitoa moshi kama vile maji yanayochemka jikoni. Chemchem hizi za maji moto ya asili zimekuwa zikibubujika bila kukauka kwa kipindi cha mamilioni ya miaka.
Hifadhi hii iko umbali wa kilometa 126 kutoka Arusha mjini ina ukubwa wa kilometa za mraba 330.

Kesi yafunguliwa Bunge la Katiba, Kesi ya kuhoji uhalali wake yafunguliwa


“Ni jambo ambalo ameomba mwenyewe kuhamia huko na ameruhusiwa maana hilo ni jambo la kawaida kama ambavyo wajumbe wengine kama kina Freeman Mbowe waliwahi kuomba, siyo jambo geni.” Hamad Rashid Mohamed Na James Magai na Neville Meena, MwananchiKesi hiyo ilifunguliwa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam jana na Mwandishi wa Habari Saidi Kubenea, kupitia kwa wakili wake Peter Kibatala, dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).Dar es Salaam/Dodoma. Bunge la Katiba linaloendelea mjini Dodoma kwa sasa liko katika hatihati ya kuendelea baada ya kufunguliwa kesi ya kuhoji madaraka yake.Kesi hiyo ilifunguliwa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam jana na Mwandishi wa Habari Saidi Kubenea, kupitia kwa wakili wake Peter Kibatala, dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).Katika kesi hiyo iliyopewa usajili wa namba  28 ya mwaka 2014, Kubenea anaiomba mahakama hiyo itoe tafsiri sahihi ya Mamlaka ya Bunge la Katiba. Kubenea amefungua kesi hiyo akiomba mahakama itoe tafsiri hiyo, chini ya  vifungu vya 25 (1) na 25 (2) vya Sheria ya Marekebisho ya Katiba namba Namba 83 ya mwaka  2011.Sambamba na kesi hiyo ya kuomba tafsiri ya mamlaka ya Bunge  hilo, pia Kubenea amewasilisha maombi mahakamani hapo akiiomba mahakama itoe zuio la muda la kusimamisha Bunge hilo ili kusubiri uamuzi wa maombi ya tafsiri hiyo.Maombi hayo ya kusimamisha Bunge hilo kwa muda yaliyopewa usajili wa namba 29 ya mwaka 2014, pamoja na maombi ya msingi ya tafsiri ya mamlaka ya Bunge yote yalifunguliwa mahakamani hapo jana chini ya Hati ya Dharura.Katika kesi hiyo ya msingi anaiomba Mahakama hiyo itoe tafsiri sahihi ya masharti ya vifungu hivyo vya sheria hiyo na pia itamke kama Bunge hilo lina mamlaka ya kubadilisha maudhui ya Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kwa kiwango gani.Kwa mujibu wa hati ya madai, Kubenea anadai kuwa msingi wa kesi hiyo unatokana na uamuzi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Desemba Mosi, 2011, lililopitisha  Sheria ya Mabadiliko ya Katiba. Anasema sheria hiyo ilikuwa na lengo la kuratibu mchakato wa kutungwa kwa Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Anaendelea kusema kuwa kutokana na sheria hiyo,  Rais aliunda Tume ya Mabadiliko ya Katiba pamoja na mambo mengine vilevile kukusanya maoni ya wananchi kuhusu mapendekezo ya Katiba Mpya na kwamba kwa msingi huo Tume hiyo iliandaa Rasimu ya Katiba.Anadai kuwa baada ya Tume hiyo kuundwa iliendelea kukusanya maoni ya wananchi yaliyotolewa katika mikutano ya hadhara na katika miundo tofauti ikiwamo mabaraza ya Katiba yaliyoanzishwa kila wilaya kwa lengo hilo.Hati hiyo inaendelea kueleza kuwa kwa mujibu wa takwimu halisi za tume hiyo,  jumla ya watu 333,537 walitoa maoni yao katika nyanja tofauti, tofauti za mapendekezo ya Katiba, ambayo ndiyo Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyatumia kuandaa Rasimu ya Katiba Mpya.Inaendelea kueleza hati hiyo kuwa baada ya Rais kukabidhiwa rasimu ya mwisho Desemba 8, 2013, kwa mujibu wa vifungu vingine vya sheria hiyo, aliunda Bunge la Katiba kwa lengo la kujadili Rasimu ya Katiba na hatimaye kupata Katiba Mpya.

Hata hivyo, kwa mujibu wa hati hiyo baada ya Bunge la Katiba kuundwa, mjadala uliibuka ndani na nje  ya  misingi ya kisheria kuhusu mamlaka yake, kama Bunge linaweza kwenda kinyume na Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na tume hiyo.

TRAFFIC MPO! MNAIONA HII IMESHAFIKA SAE KUTOKA SOWETO!



Vijana wakiwa wanasukuma wakitokea Soweto
Kulia jamaa wakiwa wanashangaa tuu

Haoo.... Mwendo Mdundo

Sasa hapa wapo Sae.. Safari inaendelea 
WAP TRAFFIC

WHO:Itachukua mda kukabili Ebola


Shirika la afya duniani WHO limeonya kuwa ueneeaji wa haraka wa Ugonjwa wa Ebola Magharibi mwa Afrika si jambo la kawaida na kwamba itachukua miezi kadhaa ili kuudhibiti ugonjwa huo.

limeonya kuwa viwango vya ugonjwa huo vilipuuzwa kwa sababu nyingi ikiwemo ile ya familia kuwaficha wagonjwa katika majumba yao.
Shirika hilo pia limesema kuwa kuna maeneo ambayo maafisa wa matibabu hawawezi kufika.
Kufikia sasa zaidi ya vifo 1400 vimethibitishwa nchini Liberia,Guinea,Sierra leone na Nigeria.