Sunday, April 22, 2012

Bwanaharusi Zuma avalia kijadi

Katika habari za tarehe kumi na tano tulikujuza juu ya maandalizi ya harusi ya Zuma

Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini ameoa mke wane, kwenye sherehe ya jadi ambapo wake zake wengine watatu piya walihudhuria.

Rais Jacob Zuma
Rais Jacob Zuma katika mavazi ya Kizulu
Bwana Zuma, mwenye umri wa miaka 70, alivaa ngozi ya chui na kubeba mkuki na ngao, mavazi ya jadi ya Kizulu, kwenye harusi iliyofanywa jimbo la KwaZulu-Natal.
Wakuu wanasisitiza kuwa Bwana Zuma mwenyewe anagharimia sherehe hizo za wikiendi hii.
Bi arusi, Bongi Ngema, amefuatana na Rais Zuma kwenye ziara zake rasmi kwa miaka kadha.

No comments: