Tuesday, September 17, 2013

MDALASINI NI SABUNI YA KUSAFISHA DAMU MWILINI

MPENDWA msomaji, wiki iliyopita tulijifunza jinsi ya kutumia mti wa muarobaini kutibu maradhi mbalimbali. Makala yale yaliwavutia wasomaji wengi na wengine kutaka ufafanuzi katika maeneo ambayo nilisahau kuyaelezea vizuri kama ifuatavyo:
Mdalasini.
Namna ya kutengeneza juisi ya muarobaini. Juisi hii hutengenezwa kwa kutwanga majani yake kwa kuweka na maji safi kidogo na kuyakamua ili  upate juisi ambayo utaitumia kujipaka au kuinywa kwa vipimo tofauti kulingana na maradhi yanayokusumbua. Kwa wenye ‘Blender Machine’, wanaweza kutumia hiyo kupata juisi.
Mjadala wa pili, japo haukuwa mkubwa lakini ulisema kuwa Mzee Makamba siye aliyeuleta mti wa Muarobani nchini. Hilo ni kweli, lakini hakuna aliyeujua muarobaini kabla ya kampeni ya “panda miti” ya mzee huyo ambayo ilifanikisha kuleta utitiri wa miti ya muarobani jijini Dar es salaam. Watu wengi tukaujua mti huo kutokea hapo.

MADA YA LEO YA MDALASINI
Mpendwa msomaji, asilimia 80 ya simu nilizopokea kutoka kwa wasomaji wetu zilikuwa ni za kuelezea matatizo ya kiafya waliyonayo yanayoambatana na mfumo wa damu. Ingawa Muarobaini unatibu maradhi mengi yakiwemo ya kwenye mfumo wa damu, lakini dawa mbadala nzuri zaidi kwa kutibu matatizo yanayotokana na damu ni magome ya mdalasini.
Magome ya mdalasini huweza kutoa nafuu na kutibu magonjwa mbalimbali kama vile malaria, shinikizo la damu, kisukari, hedhi zenye maumivu na zisizokoma, mapele, ukurutu na mapunye ya mchafuko wa damu, maambukizi ya bakteria na maradhi mengine ambayo mgonjwa aendapo hospitalini hupimwa damu kabla ya tiba.

JINSI YA KUANDAA MDALASINI
Chukua gome moja la mdalasini weka kwenye sufuria kisha mimina maji kiasi cha glasi nane au lita moja na nusu hadi mbili, chemsha kwa dakika kumi hadi 15, kisha ipua na yaache yapoe (hata kwenye friji weka), halafu kunywa kila usikiapo kiu hadi utakapoyamaliza, iwe ndani ya mchana kutwa kwa muda wa siku tano hadi kumi.
Mdalasini kitaalamu huitwa “sabuni ya kusafisha damu na njia zake”, huondoa maradhi yote yaliyojificha kwenye mishipa ya damu. Tahadhari: Mdalasini ni mmea kama ilivyo mimea mingine na hutegemea sana aina ya udongo kuzalisha vitamini, madini na tindikali mbalimbali ambazo ndiyo tiba. Hivyo ni muhimu kupata mdalasini ulio bora.
Upo mdalasini kutoka Arabuni ambao umepandwa na kuvunwa kwa ajili ya tiba ambao unaweza kuutumia kwa uhakika zaidi wa kupona. Kwa watakaouhitaji, basi tuwasiliane kwa njia ya simu, nitawapa ushauri na kuwaelekeza pa kuupata pia.
Kuna kila sababu  ya Watanzania kujua umuhimu wa kutumia vyakula na mitishamba yetu ya asili katika kutibu na kutoa kinga kwenye miili yetu dhidi ya maradhi mbalimbli na kuishi maisha ya afya njema.

No comments: