Friday, July 6, 2012

ZIJUE ATHARI ZA BANGI NA ASILI YAKE

Picture
Vituko vya kweli vya wavuta bangi
Katika maisha yangu nimekwisha sikia vituko vingi kuhusu bangi. Nikikumbuka siku ya kwanza nimemuona rafiki yangu akivuta bangi(1968), jina lake ni Iddi sitataja majina mengine ameshakuwa mtu mzima sasa ninauhakika anawajukuu wengi tu. Alikuja mahala ambapo tulikuwa tunafanya mazoezi ya muziki maana naye alikuwa mpiga gitaa mzuri, akatoa bangi kwenye kibox cha njiti za kibiriti akasokota akavuta, wote tukimkodolea macho na kusubiri apagawe, hakuna cha ajabu alichofanya ila tu nakumbuka alikuwa anarudia rudia na kudai sisi sote ni samaki. Mpaka leo nikikutana nae huwa namtania, 'samaki'.  Rafiki yangu mwingine ambaye ana wadhifa mkubwa serikalini aliwahi kunambia kuwa kuna siku alivuta bangi akahisi shati lake lina siafu, ilibidi alitoe na kulitupa pembeni huku akipiga kelele 'siafu siafu'. Kuna Mzee mwingine Richard, ambaye kwa sasa mawasiliano yetu yamekuwa ni kupitia FB maana miaka mingi hatujaonana, aliwahi kuwa kituko shuleni baada ya kuvuta bangi wakati wa mapumziko ya saa 4, enzi hizo akiwa form 2, yeye alihisi mbingu zinateremka na kuja kumbana, kwa hiyo nae akazidi kutembea huku akiwa ameinama macho yake juu, akiangalia mbingu ambazo kwake zilikuwa zinateremka na kukaribia kumbana, watu wote tukimuangalia na kumshangaa. Sitasahau nilivyocheka kituko cha rafiki yangu marehemu aliyekuwa mwanamuziki muimbaji, ambaye alinambia yeye na rafiki zake mara nyingi walikuwa wanazungumza kuwa kuna wauza bangi huchanganya bangi na kinyesi cha binadamu ili iwe kali zaidi. Sasa siku moja wenzie walipompa kipisi cha bangi, kilianza kumletea hisa za kufa kufa hivyo akahisi 'wamemchanganyia'. Kadri muda ukivyozidi ndivyo alivyozidi kujisikia vibaya, ikalazimu akimbilie kwa baba yake huku akilia,'Baba baba wamenichanganyia'

Mmea wa bangi (cannabis sativa) hukua mwituni na hustawi katika maeneo mengi tofauti ulimwenguni. Unajulikana kwa majina menegi, bangi, mbanje, marijuana, nyasi, gugu, mtungi, kivuto, ganja, rifa, jive, katani, ikisokotwa kwa karatasi ya sigara yaitwa kiungo, kipeo au kijiti. kemikali tandaji (yenye mguvu) katika bangi yaitwa 'delta-9-tetra-hydrocannabinol (THC), ambayo imekusanyika katika utomvu wa jani lake. Hicho kileo kinachotumiwa vibaya mara kwa mara hutolewa katika sehemu ya juu inayochanua maua na majani ya mmea uliokaushwa na mara nyingi huwa na mbegu na mashina. katika hali hi ina rangi ya kijivu-kijani hadi kijani-hudhurungi. Yaweza kutayarishwa iwe vumbi nyororo au mithili ya majani chai. Hashishi ikiwa hali mojawapo ya bangi iliyo na nguvu zaidi amabayo ni utomvu uliokaushwa ambao hutolewa kutoka kwenye maua na matawi ya mimea ya kike.
bangi huvutwa pekee au huchnganywa na tumbaku. bangi mara nyingine hutumiwa pamoja na nyingine hutumiwa pamoja na vinywaji au kuokwa kuwa halua. Matumizi ya bangi yanahusishwa na madhara mbalimbali kutegemea na kiasi cha bangi kilichotumiwa na matarajio ya mtumiaji mwenyewe. Wakati bangi inatumiwa kidogo hadi kipimokiasi cha kadiri inaleta kikwakwa na wingi na furaha, ikijumuisha hisia-mwili za raha. Utafiti uliofanyika hivi majuzi katika mabara ya Ulaya na Marekani unaonyesha kuwa huweza kufaa kama dawa ya kuondoa maumivu, kuzuia kutapika, na kuboresha hamu ya kula kwa wagonjwa wa saratani na UKIMWI. Utafiti zaidi unapendekezwa.
Bangi husababisha mabdaliko katika uwezo wa mtu wa kutmabua wakati na nafasi. Taarifa za matokeo yake zimechnganyika. Watumiaji wanadai wao hupata utambuzi zaidi, hupoteza vizuizi, ukuzaji wa muda wa hisia-bunifu, na uwezo wa kucheza muziki, kusimulia hadithi, kuimba, au kucheza dansi. Hii ndiyo sababu kileo hiki kinapendwa zaidi miongoni hiki kinapendwa zaidi miongoni mwa wasanii. bangi inaaminiwa sana na wengi kuwa na matokeo ya kuamsha ashiki ya kujamiiana katika hatua za mwanzo za 'kuikoka', huku ikiongezwa nyege na raha ya kujamiaana lakini siyo lazima kwamba inaongeza uwezo wa kitendo chenyewe, kabla ya mtumiaji hajapatwa na madhara ya kulevya yasababishayo usingizi.
Bangi huzidisha hisia za mtumiaji. Hivyo, humfanya mtu mwenye furaha ajihisi mwenye furaha zaidi,lakini yaweza pia kumfanya mtu mnyonge awe mnyonge zaidi, mwenye kufadhaika, mwoga na mwenye wazimu wa kufikiria anaonewa kila wakati.
Kama ilivyo pombe, bangi ni kitoa vizuizi - 'hulegeza' au hupunguza vizuizi vya mtumiaji binafsi. Hii ndiyo sababu labda yaweza kupendelewa zaidi na wasanii kama kichocheo cha bunifu. Hata hivyo, pia hudhoofisha ulinganishi, hisiaghafla, maamuzi na kumbukumbu, hususani ikitumiwa kwa mazoea. Hasa husababisha mwasho na wekundu wa macho, na kupnua mboni ya jicho. Wakati mtumiaji anapokokwa uchovu na usingizi humwingia.
Madhara hasi kiafya yatokanayo na utumiaji endelevu kwa kiasi kikubwa cha kama uvutaji mzito wa hashishi kali ni pamoja na kope za macho kuwa na vimbe kwa ndani na ugonjwa wa mapafu, ilihali athari mbaya zaidi huonekana katika utambuzi na usumbufu. Kuchngayikiwa na tabia za kurukwa na akili zinaweza kujitokeza na wakati mwingine huenda ikaelekeza kuwa na wazimu sugu wa bangi. Matumizi ya bangi kwa muda mrefu yanasabaisha kupoteza nguvu za uume au uke, upungufu wa kujihami dhidi ya magonjwa na maambakizo. Mara nyingine inapoteza nguvu na msukumo, fikira za polepole na zilizochanganyikwa, na kuathiri kumbukumbu.
Katika sehemu ya kusini mwa Afrika bangi mara nyingine huvutwa ikichanganywa na mandrax katika mchanganyiko wenye nguvu sana uitwao 'poda nyeupe.' Watumiaji wa heroini wanaweza kuchanganya heroini na bangi marijuana ili wavute. Ikitumiwa katika hali hii, heroini ina ulevi wa njozi sawa na uvutaji wa afyuni.
 

No comments: