Saturday, April 7, 2012

MWONEKANA WA MPAMBANO WA SIMBA NA SETIF NCHINI ALGERIA, AMBAPO SIMBA IMESONGA MBELE KATIKA MICHUANO HIYO

 Mtandao wako wa Umma www.fourwaysbukoba.blogspot.com unakuletea Taswira za mpambano wa Simba na Setif moja kwa moja kutoka Algeria, kama anavyoonekana mchezaji wa timu ya Simba mwinyi Kazimoto wa nne kutoka kulia akinyanyua mikono yake kulalamikia jambo, katika mchezo huo Simba imfanikiwa kusonga mbele katika hatua nyingine ya michuano hiyo baada ya kufungwa magoli 3-1 huku ikifaidika na goli la ugenini baada ya kuifuna timu ya Es Setif magoli 2-0 katika mchezo wa kwanza uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Tanzania wiki mbili zilizopita, Hongereni sana wachezaji wa Simba, Viongozi, Marafiki wa Simba pamoja na mashabiki kwa ujumla.
 Wachezaji wa Simba wakipeana mawaidha kabla ya kuanza kwa mchezo huo ambao katika dakika ya 12 tu ya mchezo beki mahiri wa Simba Juma Nyoso alipewa kadi nyekundu na kutolewa nje ya uwanja.
 Mashabiki wa timu ya Es Setif wakiwa wamejaa uwanjani kabla ya kuanza kwa mpambano huo jijini Setif Algeri.
Wanafunzi wa Kitanzania walitupa sapoti kubwa. Zacharia Hans Poppe ndiye aliyegharamia kiingilio cha wanafunzi wote walioingia uwanjani!
 Mdau Nick Magarinza  katikati pamoja na wanasimba wengine wakiwa uwanjani wakishuhudia mpambano huo.
Wachezaji wa Simba wakipata chakula cha usiku mara baada ya kuwaondosha waarabu hao huko Setif na kutinga hatua ya makundi.Kwa hisani ya Blog ya four ways bukoba

No comments: