Sunday, April 22, 2012

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wafika Homs

Ujumbe mdogo wa wachunguzi wa Umoja wa Mataifa kwa mara ya kwanza umeruhusiwa kuzuru mji wa Homs, Syria - shina la upinzani - ambao umekuwa ukishambuliwa kwa mizinga na jeshi la serikali.
Picha ya YouTube ikionesha nyumba za Homs zikishambuliwa na jeshi la serikali
Maafisa hao walikutana na gavana wa Homs na waliona baadhi ya mitaa iliyoangamia.
Wanaharakati wanasema jeshi liliacha mashambulio dhidi ya Homs leo, kwa mara ya kwanza kwa muda wa majuma kadha, na mizinga ilifichwa.
Ziara hiyo ilifanywa saa chache kabla ya Baraza la Usalama kupiga kura kuzidisha idadi ya wachunguzi nchini Syria, ili wafikie 300.
Serikali ya Syria imetia saini mpango wa amani wa Umoja wa Mataifa, lakini hadi sasa imeshindwa kusitisha mapigano.

No comments: