Thursday, May 31, 2012

DIAMOND ASEMA ALICHOKIPATA BAADA YA KUPERFORM BIG BROTHER AFRICA!

.
Siku nne baada ya kuperform kwenye shindano la Big Brother Afrika, staa wa muziki Tanzania ambae ndio anaongoza kwa kupiga showz nyingi na zenye hela ndefu, Diamond Platnums amesema baada ya performance yake kuonekana tayari tayari milango mingine ya mafanikio imefunguka.
Amesema “nimepata vitu vingi, imenitengenezea mwanya wa kukubalika sana na karibu media zote za kule nimepata nafasi ya kusain karatasi kwenye baraza la sanaa Afrika kusini ambapo sasa radio zitaanza kucheza nyimbo zangu na nitakua nalipwa wakizipiga, nimepata connection ya kufahamiana na wasanii wakubwa wakubwa wa Afrika ambapo mda sio mrefu nitafanya nao kazi”
Kwenye sentensi nyingine Diamond amesema “Nimewapa album yangu ya kwanza na nyimbo zangu nyingine ambazo nimeshaziachia, nimetafutwa na watu wa media za Nigeria, Namibia na kwingine ambao walitaka niwape kazi zangu, hiyo ni baada ya kuperform kwenye show ya Big Brother japo kabla hawakudhani kama ningeweza kufanya hivyo… na kuna vitu vingine ambavyo nimevipata na sijaruhusiwa bado kuvizungumza ila nitavizungumza na watu wanaweza wasiamini kwamba vimetokana na show yangu BBA”
Bab Tale ambae ni Meneja wa kundi la Tip Top Connection alieongozana na Diamond kwenda Afrika Kusini amesema kwa mara ya kwanza kwenye historia ya shindano la Big Bro, kwenye show ya Diamond mmoja wa mashabiki waliopagawa ndio alipanda kwenye stage na kwenda kucheza kitu ambacho huwa hakiruhusiwi, ni masharti ambayo huwa wanapewamashabiki wote wanaokwenda kutazama show, hivyo baada ya huyo mmoja kuvunja sheria, alitolewa nje.
Tale amesema toka walipotoka bongo walipitia Nairobi na hakuna mtu aliewashangaa, yani mpaka Tale akawa anajiuliza moyoni mbona watu hata hawashtuki, walipofika pia South Afrika hakuna aliewashangaa hata walipokua wanaanza mazoezi watu waliowapokea walikua wanamchukulia poa Diamond lakini alipoanza mazoezi wakajua jamaa mkali, kwa maelezo mengine zaidi msikilize Bab Tale hapo chini…………

No comments: