Monday, December 2, 2013

KOCHA MPYA WA SIMBA AWASILI..!

a_6a71e.jpg

Mashabiki wa Timu ya Simba, wakimpokea kwa shangwe na nderemo, kocha wao mpya aliyetua nchini leo machana.
b_36c4e.jpg
Kocha huyo akikabidhiwa taji la maua na mashabiki baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere Dar leo.
Na http://www.sufianimafoto.com (P.T)
Mara kadhaa kumekuwa kukitokea furaha kwa mashabiki, viongozi na hata wachezaji wa Klabu zetu kubwa hapa nchini, wakati wanapokuwa wanamkaribisha Kocha mpya ama kumtambulisha kwa mbwembwe nyingi, lakini anapotokea kukosea kidogo haijalishi ni muda gani amekwisha kaa na Klabu husika, anaweza kutimulia ama kuanzishiwa mizengwe hadi akakata tamaa ya kuonyesha yale yote aliyojiandaa nayo kuifanyia Klabu husika.
Wakati umefika sasa kwa Klabu zetu kufunguka kifikra na kuwa na upeo wa kufikiri ili kuziendeleza klabu zetu, kwa kuwaachia makocha waweze kufanya yale yanayostahili bila kuingiliwa na viongozi ama watu flani kwa pesa zao ama umaarufu wao katika klabu. Huko nyuma walikwishapokelewa makocha kadhaa kama alivyofanyiwa kocha huyu leo na waliondoka kimya kimya huku wengine wakiondoka klabuni kwa mafalakano na viongozi wa klabu.
c_5dc27.jpg
Akipata menu.....
d_8d6e9.jpg
Kocha huyo akiongozana na baadhi ya viongozi wa Simba wakati alipotembelea na kukagua uwanja wa mazoezi wa Klabu hiyo wa Kinesi.Picha kwa Hisani ya Lenzi ya Michezo

No comments: