Saturday, December 7, 2013

R I P MANDERA

WA UZANI WA JUU



Hata wakati yupo kifungoni katika chumba chake kidogo cha gereza katika kisiwa cha Robben, Nelson Mandela alifanya mazoezi kujiweka fiti kiafya na mwili na akili.

Enzi za ujana wake alipata kuwa bondia wa uzani wa juu (Heavyweight), kama ambavyo anaonekana katika picha kadhaa akijifua.

Mandela pia alikuwa akijifua na swahiba wake na bondia wa uzito wa kati Jerry Moloi ambaye yeye ngumi kwake ilikuwa ni kazi na sehemu ya maisha yake kwani rekodi yake inaonyesha kushinda mabambano 13, kupoteza 15 na kutoka sare 30.
Picha hii wakiwa juu ya jengo mjini Johannesburg.
Sanamu hii ya Nelson Mandela iliyotokana na picha hiyo hapo juu ikiwa imewekwa mtaani kumuenzi Bondia huyo mpigania uhuru wa Afrika Kusiani.

Katika kitabu chake mzee Nelson Mandela alicho anza kukiandika akiwa gerezani cha, Safari ndefu ya Uhuru (Long Walk to Freedom), Mandela anaelezea upendo wake katika mchezo wa ngumi wa ndondi (na kwa nini alifanya hivyo):
“Mimi sikuwa na furahia mapambano uliongoni katika ngumi sana kama sayansi ya yake inavyosema. Mimi nilikuwa navutiwa na jinsi mtu anavyouongoza mwili kujikinga, na vile mwingine akitumia mkakati wa kushambulia na kurui nyuma ili kupata ushindi katika mchezo”, aliandika Mandela.
Ngumi ni usawa katika ulingo, lakini cheo, umri, rangi, na mali ni vitu visivyo na maana. . . Mimi kamwe sijafanya mapigano yoyote halisi baada ya mimi kuingia katika siasa. 

Madhumini yangu makubwa yalikuwa katika mafunzo; mazoezi ya ngumi yalinifanya kupiteza msongo wa mawazo. Baada ya ya mazoezi ya jioni nilijihisi kiakili na kimwili ni mwepesi.
 
Nelson Mandela akirusha ngumi kwa Bigwa wa Masubwi wa zamani Duniani Mohamed Ally.
Nelson Mandela akiweka paling na Mkali wa ngumi duniani Lennox Lewis.
Nelson Mandela akiwa na Mkali wa ngumi duniani Mike Tyson.

No comments: