Monday, April 30, 2012

Msikiti wa Sunni Muslim Jamatin wadai kutaka kumfikisha waziri wa mambo ya ndani mahakamani

NA MWANDISHI WETU
UONGOZI wa Msikiti wa Sunni Muslim Jamatin umesema unatarajia kumfikisha Mahakamani wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha baada ya kuuengua uongozi wa Kamati ya muda iliochaguliwa kihalali na waumini wa Msikiti huo kwa madai kuwa hautambuliki.
Hali hiyo imekuja baada ya mgogoro wa kugombea madaraka katika msikiti huo kudumu kwa muda mrefu sasa kitendo kilichosababishwa kuundwa kamati ya Muda kuelekea mchakato wa Katiba mpya ambayo ingefanya uandaliwe uchaguzi wa kuwapata viongozi wapya.
Akizungumza na wandishi wa habari, kiongozi wa kundi la viongozi walionguliwa madarakani Sheikh Majid Saleh Mohammed alisema wanatarajia kwenda Mahakamani siku ya Jumatano kupinga kitndo cha waziri huyo kwani kimekiuka sheria na kuingilia imani ya dini hiyo.
Alitanabaisha kuwa lengo lao ni kuitaka mahakama kuusimamisha uongozi huo mpya ulioingizwa kimahaba na waziri huyo hadi hapo pande hizo mbili zitakapofikia muafaka na kuandaliwa uchaguzi mpya kama ilivyo agizwa na mahaka hapo awali.
“Waziri kitendo alichofanya waziri hakikubaliki kwani ni cha ubaguzi kutokana na viongozi alioweka madarakani waote ni wazanzibari wenzake hivyo amekiuka madaraka yake kwa kuonyesha upendeleo wa wazi kwa kuwabagua watu wa Tanzania Bara kitendo ambacho hakikubaliki hivyo tunaenda kusimamisha uongozi huo mahakamani”alisema Sheikh Maohammed.
Mohammed alisema Waziri alionyesha udhaifu katika maamuzi yake kwani katika muda wa siku mbili aliweza kuwapa haki Kamati ya muda kisha kubadilika na kuwapa Wazanzibari wenzake uongozi.
Aidha, alimtaka waziri kuhakikisha kuwa anatii sheria za nchi ambapo mahakama iliagiza kusifanyike mabadiliko ya uongozi hadi pande hizo zitakapokaa kwa pamoja kisha kupanga jinsi zitakavyoendesha uchaguzi.
Alisema haipendezi kweli migogoro yao kutatuliwa mahakamani lakini hali hiyo imesababishwa na chombo ambacho kingesimamia migogoro hiyo Baraza la Kuu la Waislam Nchini (Bakwata kushindwa kabisa kutekeleza majukumu yake kutokana  viongozi wake wengi kujiingiza zaidi katika maswala ya kidunia.

No comments: