Showing posts with label UMOJA. Show all posts
Showing posts with label UMOJA. Show all posts

Thursday, June 21, 2012

MPANGO WA NMB FINANCIAL FITNESS WAENDELEA KATIKA SHULE MBALIMBALI

 Dotto Mbwana, mfanyakazi wa NMB Muhimbili akigawa vijarida vya NMB Financial Fitness kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Muhimbili mpango huo ni kwa ajili ya kuwaandaa wanafuzi kupata uelewa wa masuala ya kibenki mashuleni
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mtibwa wakijisomea kijarida cha NMB Financial Fitness wakati wafanyakazi wa NMB Turiani walipotembelea shule yao
 Wanafunzi wa Shule ya Msingi Muhimbili wakisoma kijarida cha NMB Financial Fitness
 Wanafunzi wa Shule ya Msingi Muhimbili wakisoma kijarida cha NMB Financial Fitness
Meneja wa NMB Muhimbili Janeth Shango akiwasisitizia wanafunzi juu wa kuweka fedha wakiwa na umri mdogo

Thursday, May 3, 2012

WAKUU WA TAASISI ZA UMOJA WA MATAIFA (UN) WAKUTANA NA JUKWAA LA WAHARIRI

Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania, Dk Alberic Kacou (kushoto), leo akihutubia Jukwaa la Wahariri aliwashakuru wahariri nchini kwa kazi kubwa wanayofanya katika utoaji wa taarifa za umoja huo. Amesema kwamba kumekuwa na ongezeko kubwa la taarifa zinazotolewa na vyombo vya habari kuhusiana na shughuli za Umoja wa Mataifa ambalo pia limeenda sambamba maoni na taarifa zinazotolewa kuwa sahihi.
 
Dk. Kacou pia amesema kwa upande wa Umoja wa Mataifa, jitihada zimefanyika kuhakikisha kuwa masuala kutoka kwa waandishi yanapatiwa majibu kwa uharaka na urahisi. Moja ya jitihada hizo ni pamoja na uboreshwaji wa tovuti ya Umoja wa Mataifa Tanzania ambayo kwa sasa ina sehemu ya vyombo vya habari ambayo ni maalumu kwa kuhudumia mahitaji ya waandishi hapa nchini.
Mratibu huyo pia alilishukuru jukwaa la wahariri kwa kuonyesha nia ya kutaka kufahamu zaidi na kushirikiana na ofisi ya Umoja wa Mataifa katika mipango yao ya ushirikiano na serikali ya Tanzania, bara na visiwani. Katikati ni Mwakalishi wa UNESCO Tanzania Bi. Vibeke Jensen na Kulia ni Mkurugenzi wa UNDP Tanzania Bw. Phillipe Poimsot.
Mwakalishi wa UNESCO Tanzania Bi. Vibeke Jensen (wa pili kulia) amepongeza mafanikio katika kupanua elimu ya sekondari nchini na kusema kwamba mpango wa kuwa na angalau shule moja ya sekondari katika kila kata umefanikiwa kwa kiasi kikubwa. Pia amepongeza mafanikio katika kuhakikisha kwamba wanafunzi wengi zaidi wanajiunga na masomo ya sekondari na kwamba kumekuwa na usawa wa kijinsia katika uandishikaji wanafunzi shule za msingi.
Hata hivyo, Jensen, ameelezea masikitiko yake kwamba kadri wanafunzi wanavyoendelea na masomo ya juu sekondari usawa wa kijinsia umekuwa ukipungua. Amesema pia tatizo kubwa sio uandikishwaji wa wanafunzi mashuleni lakini ni kitu gani wanachojifunza.
Ameelezea kusikitishwa na kiwango cha elimu kinachotolewa nchini na kusema kwamba sio tu hakitoi uwezo wa kujiajiri kwa wanaomaliza sekondari, bali pia kinatoa fursa chache kwa wanafunzi kuendelea na masomo ya juu.
 Mkurugenzi wa UNAIDS Tanzania Dr. Luc Barrier (kushoto) amefafanua kwamba mapambano yatayoweza kuzaa matunda dhidi ya UKIMWI katika nchi ni yale ambayo yatahusisha sekta zote za jamii. Alisistiza kwamba kaasisi taasis iliyopo chini ya Umoja wa Mataifa, shughuli zao zinaendeshwa sambamba na sera za nchi husika katika masuala ya kupambana na UKIMWI.
Dr Barrier amesema kwamba jamboa la kwanza ambalo hulifanya kama taasisi ni kuangalia hali halisi ya nchi, vipaumbele vya serikali husika na ndipo hufikia maamuzi ya kukutana na wahusika kutoka upande wa serikali ili kuweza kufahamu Umoja wa Mataifa wanaweza kuchangia na kusaidia vipi katika mipango na sera ya nchi.
Ameongeza kwamba ushirikiano baina ya Umoja wa Mataifa na serikali ya nchi husika umekuwa na mafanikio kwa sababu hausishi sekta ya umma pekee bali na sekta binfansi katika kutasfiri mikakati na mipango ya kupambana na UKIMWI.Katikati ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania, Dk. Alberic Kacou, Mwakalishi wa UNESCO Tanzania Bi. Vibeke Jensen na Kulia ni Mkurugenzi wa UNDP Tanzania Bw. Phillipe Poimsot.
 Msaidizi Mshauri wa Umoja wa Mataifa Bw. Tobias Rahm akijumuisha katika mkutano wa taasisi za Umoja wa Mataifa na Jukwaa la Wahariri, Rahm alisema kwamba ni matumaini yake kuwa vyombo vya habari vitaendelea kufanya kazi kwa karibu na taasisi katika kuongea ufanisi na uelewa wa shughuli zao. 
Mkurugenzi wa UNDP Tanzania Bw. Phillipe Poimsot alisema Pamoja na utajiri mkubwa wa maliasili, Poimsot amesema kwamba Tanzania bado ina wananchi wengi sana ambao ni maskini. Amefafanua kwamba pamoja na pato la taifa limekuwa likiongeza kuanzia mwaka 2000, hali hiyo imekuwa ikitokea katika sekta ambazo haziongezi ajira kwa wananchi wa kawaida.
Pia ameelezia kwamba wananch wengi ambao wanapata fursa ya kuingia kwenye soko la ajira, mara nyingi inakuwa kwenye kilimo na sekta isiyokuwa rasmi ambapo uzalishaji pamoja na ujira unakuwa ni mdogo sana.
Baadhi ya Wahariri wa Vyombo mbalimbali vya habari waliohudhuria mkutano huo uliofanyika katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam jana.
Baadhi ya Wahariri wa Vyombo mbalimbali vya habari waliohudhuria mkutano huo uliofanyika katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam jana.

Wednesday, April 18, 2012

USHIRIKIANO WA WAISILAMU NA WAKRISTU

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA KONGAMANO LA DINI LA WAISLAMU NA WAKRISTO JIJINI DAR LEO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya viongozi wa dini alipowasili kwenye Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam,kwa ajili ya kufungua Kongamano la Dini la Waislam na Wakristo, lililoanza leo Aprili 18, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Baadhi ya Viongozi wa Dini wakifuatilia kwa makini Hotuba ya Mgeni Rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, alipofika kufungua rasmi Kongamano la Dini la Waislam na Wakristo, lililoanza leo Aprili 18, 2012 kwenye Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Baadhi ya Viongozi wa Dini wakifuatilia kwa makini Hotuba ya Mgeni Rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, alipofika kufungua rasmi Kongamano la Dini la Waislam na Wakristo, lililoanza leo Aprili 18, 2012 kwenye Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati akifungua rasmi Kongamano la Dini la Waislam na Wakristo lililoanza leo Aprili 18, kwenye Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya Viongozi wa dini baada ya kuzindua rasmi Kongamano la Dini la Waislam na Wakristo katika Hoteli ya White Sands, jijini Dar es Salaam, leo Aprili 18, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja ya kumbukumbu na baadhi ya Viongozi wa Dini, baada ya kuzindua rasmi Kongamano la Dini la waislam na Wakristo, katika Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam, leo Aprili 18, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR