Showing posts with label BURUDANI. Show all posts
Showing posts with label BURUDANI. Show all posts

Thursday, August 21, 2014

AIBU: MSANII WA BONGO FLEVA ANASWA LAIVU AKINUNUA NGONO KWA MAKAHABA USIKU WA MANANE

WAKATI wasanii wakitakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuenzi maadili mema kwa jamii ya Kitanzania, mambo yamekuwa kinyume, baada ya nyota wa muziki wa kizazi kipya, Ramadhan Shaban 'Wabibi' kukutwa live, akipatana bei na wanawake wanaojiuza katika eneo maarufu kwa machangudoa la Sinza Africasana jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.

Nyota wa muziki wa kizazi kipya, Ramadhan Shaban 'Wabibi' akitega 'mingo' kujiopolea machangu maeneo ya Sinza Africasana jijini Dar.

Wabibi anayetamba na kibao chake cha Kitenge kwenye vituo mbalimbali vya redio na runinga nchini, usiku wa saa saba alikuwa akivinjari katika viwanja hivyo, akichagua kama wafanyavyo wateja wa nguo dukani.

Mara baada ya kuonekana kwa msanii huyo katika viwanja hivyo, chanzo chetu ambacho ni kikereketwa cha maadili, kilipiga simu katika ofisi za Oparesheni Fichua Maovu (OFM) kitengo kilicho chini ya Global Publishers saa saba usiku kikiripoti skendo hiyo ya aibu.

Msanii Ramadhan Shaban 'Wabibi' akipatana bei na mmoja wa machangudoa.

Bila kuchelewa paparazi wetu alifika eneo la tukio kwa pikipiki na kumkuta staa huyo akiendelea na chaguachagua yake kwa akinadada waliovalia kihasara ili kuwavutia wanaume wakware.

Mwanga wa kamera zetu hata hivyo haukuonekana kumshtusha sana msanii huyo ambaye alijichekesha na kujifanya kuendelea na shughuli nyingine, kama walivyokuwa wakifanya watu wengine katika eneo hilo linalosifika kwa biashara ya ukahaba jijini Dar.


Ramadhan Shaban 'Wabibi' akiwa na changudoa mwingine.

Baada ya kujipatia picha za kutosha za tukio hilo na kuondoka eneo hilo, makamanda wa OFM hawakwenda kulala, bali waliendelea na uchunguzi wao katika mitaa mbalimbali.Katika hali isiyotarajiwa, saa mbili baadaye, msanii huyo kwa mara nyingine alikutwa na OFM akiwa anaendelea na biashara yake ya sagulasagula ya machangudoa, lakini hivi sasa akiwa amehamishia kambi katika eneo la Sinza ya Mapambano.

Akiwa amevutiwa na mwanadada mmoja na kuanza kufanya naye mapatano ya bei, paparazi wetu alimuwahi kwa kumpiga picha, ambapo safari hii alishtuka zaidi na chapchap, akachukua Bajaj na kutokomea.
'
Wabibi' akikurupushwa na kamera zetu za Global katika eneo la tukio.

Wabibi aliwahi kuwa memba wa kundi la muziki la Suba Mkole, akijulikana kama Wambua Classic ambao walitoa albamu iliyotamba kwa jina la Sonde.

Wednesday, August 20, 2014

EXTRA BONGO KUSINDIKIZA MASAI SAFARI BANDI KATIKA UZINDUZI WA ALBAM YAO


Wapiga magitaa wa bendi ya masai safari band wakichalaza magitaa wakati wa mazoezio yao ya kujiandaa na uzinduzi wa albam yao ya kwanza kushoto Josephe Bivence na Juma Ali
Wapiga magitaa wa bendi ya masai safari band wakichalaza magitaa wakati wa mazoezio yao ya kujiandaa na uzinduzi wa albam yao ya kwanza kushoto Josephe Bivence na Juma Ali
Na Mwandishi Wetu
 BENDI ya masai safari ya jijini Dar es salaam inatarajia kuzindua albam yake ya kwanza kabisa

watakayozindua siku ya augost 30 katika ukumbi wa raunch time ya jijini akizungumzia uzinduzi wa albam hiyo rais wa bendi hiyo Fransic Mwaisela amesema kwamba siku hiyo watasindikizwa na bendi mbalimbali wakiongozwa na bendi ya Extra bongo inayo ongozwa na Ali Choki

alizitaja nyimbo zilizomo katika albam hiyo ni sita itakayozinduliwa siku hiyo ikiwa nyimbo ambayo iliyobeba albam ni akuna kama baba ya pili ni njia panda,mikono ni kazi,ndoa ni mpango wa mungu,usiwasikilize wambeya,kilio changu nyimbo hizo ndio zitakazokuwa katika albam hiyo itakayo zinduliwa mwishoni mwa mwezi huu


aliongeza kwa kutaja wasanii wengine watakaokuwepo siku hiyo ni Omari Tego,Maua Tego pamoja na wasanii mbalimbali wa bondo flefa watakaosindikiza uzinduzi uho

bendi hiyo kwa sasa ipo kwenye mazoezi ya nguvu kwa ajili ya kutoa burudani kabambe siku ya uzinduzi wa albam ya bendi hiyo

Saturday, September 8, 2012

MREMBO WA REDDS MISS ILALA APATIKANA



Miss Ilala 2012, Noela Michael (katikati), akiwa kwenye pozi na mshindi namba mbili Magdalena Roy Munisi (kulia), na mshindi namba tatu Mary Chizi muda mfupi baada ya kutangazwa washindi.
Miss Ilala aliyeachia taji hilo Salha Israel, akikatiza kuaga jukwaani hapo kabla ya kukabidhi rasmi taji hilo.
Mary Chizi akionyesha kipaji chake cha ziada wakati wa kugombea miss Talent ambapo aliibuka kidedea.
Magdalena Roy Munisi akicheza kama msanii wa Marekani … kwenye mchakato wa kugombea taji la kipaji.
Warembo walioingia kwenye tano bora ya shindano hilo.
Baadhi ya majaji waliyokuwa wakiratibu shindano hilo.
Msanii wa kundi la Wanaume Family Chege, akitumbuiza jukwaani hapo.
Wasanii wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper (kulia), na Jennifer Kyaka ‘Odama’, wakifuatilia mpambano huo.
Vicent Kigosi ‘Ray’ (kulia), na Single Mtambalike ‘Richie’, wakifuatilia burudani hiyo.
Mtangazaji wa Times FM, Gardina G Habash (katikati), akiwa kwenye pozi na wasanii wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Chege na Chid Benzi.
Mratibu wa mashindano hayo Gardina G, akiongea jambo mahari hapo.
Moja ya kikundi cha sanaa kikitumbuiza.
Baadhi ya Mashabiki waliyohudhuria mahari hapo wakifuatilia kwa makini burudani za mashindano hayo.
Usiku wa kuamkia leo kulifanyika mashindano ya kumsaka mrimbwende wa kuwakilisha Wilaya ya Ilala Ndani ya Ukumbi wa Nyumbani Lounge jijini Dar es Salaam, ambapo shindano hilo lilikuwa likishirikisha warembo 12.
Shindano hilo lililo anza majira ya saa nne na nusu usiku, lilipambwa na burudani kutoka katika bendi ya B Band, msanii wa TMK Family Chege na wasanii wa kusheki.
Hadi mwisho wa shindano hilo Noel Michael aliibuka kidedea, huku nafasi ya pili ikitua kwa Magdalena Roy Munisi na nafasi ya tatu ikitwaliwa na Mary Chizi ambaye pia amechukua taji la Miss mwenye kipaji akiwabwaga wenzake watano.
Habari/Picha: Musa Mateja/GP

Wednesday, September 5, 2012

FULL BURUDANI


JAYDEE, DIMPOZ, BANANA, CHEGGE KUIPAMBA REDDS MISS ILALA


Warembo wanaoshiriki kwenye shindano la Redd's Miss Ilala 2012 wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa utambulisho huo.
WASANII nguli wa miondoko ya bongofleva sanjari na Machozi Band, kesho watalipamba shindano la kumsaka mrithi wa Salha Israel katika shindano la Miss Ilala litakalofanyika kwenye ukumbi wa nje wa Nyumbani Lounge uliopo maeneo ya Namanga, Dar es Salaam.
Wasanii hao ambao watatumia bendi katika kuonesha umahiri wao, wamejumuika kwenye shindano hilo ili kukidhi kile mashabiki wa Miss Ilala wanachotarajia. Mbali ya wasanii hao, msanii wa luninga, Steve Nyerere ndiye atakayeliongoza kama MC ambapo Alhamis (kesho) watakuwa na mkutano na waandishi wa habari kwenye club ya City Sports Lounge kwa ajili ya kutangaza zawadi.
Vimwana 14 wanaotarajiwa kupanda jukwaani kuwania umalkia wa Kanda ya Manispaa ya Ilala, Redds Miss Ilala 2012, kati yao 12 wiki iliyopita walishindana kwenye kategoria ya kipaji ambapo watano kati yao walitinga hatua ya fainali, ambayo itamaliziwa siku ya shindano lenyewe Ijumaa.
Katika kinyanganyiro hicho mrembo Mary Chizi alikuwa kivutio zaidi kwa jinsi alivyoonesha umahiri wake wa wepesi wa kujvingirisha mwili huku Mectilda Martin akizoa ukumbi mzima kwa kurap na huku akiwa ameandana kwa kucheza hata mavazi yanayotumiwa na wasanii wa miondoko hiyo.
Magdalena Munisi hakuwa nyuma kabisa katika kumwigiza mwanamuziki nguli wa marekani, Ciara kwa umahiri wake wa kulitumia jukwaa, lakini kubwa kuliko pia kwa mrembo Amina Sangawe alibuni nguo kwa kutumia vipande viwili vya khanga ambapo aliliunganisha jukwaani kupitia pini nakumvika mmrembo mwenzie. Stella Moris kwa upande wake alionesha ukali kwa kuimba.
Warembo hao, wamekuwa wakijifua kwa takriban wiki nne sasa chini ya wakufunzi, Slyvia Mashuda ambaye ni Miss Tanzania namba mbili mwaka 2008 na Miss Ilala wa mwaka huo, na Neema Mbuya na Dickson Daudi wa THT katika shoo.
Miss Ilala, yenye rekodi ya kutoa warembo wanne waliotwaa taji la Miss Tanzania kuanzia mwaka 1999, (Hoyce Temu), 2000 (Jacquline Ntuyabaliwe aka K-Lyne), 2002 (Angela Damas Mutalimwa) na Salha Israel anayeshikilia taji hilo kwa sasa, imepania kuendeleza rekodi yake nzuri mwaka huu.
Miss Ilala inahusisha warembo kutoka vitongoji vya Dar City Center, Tabata na Ukonga na inadhaminiwa na City Sports Lounge, Redd's Premmium Cold, Uhuru One, Dodoma Wine, Nyumbani Lounge, gazeti la Jambo Leo,  100.5 Times FM, Redio ya watu 88.4 Cloud's FM.
Mbali ya walioingia tano bora katika vipaji, warembo wengine wanaoshiriki shindano hilo ni pamoja na Mary Chizi, Matilda Martin, Magdalena Munisi, Suzan Deodatus, Whitness Michael, Stella Moris na Elizaberth Pertty. Wengine ni Wilmina  Mvungi, Zawadi Mwambe, Rehema Said, Diana Simon, Amina Sangwe, Noela Michael na Phillios Lemi.
Mbali ya Redd's Premmiun Cold, wadhamini wengine katika mashindano hayo ni pamoja na  Uhuru One, Dodoma Wine, City Sports Lounge, gazeti la Jambo Leo, Nyumbani Lounge, 100.5 Times FM, Redio ya watu 88.4 Cloud's FM na Amaya Salon.
Natanguliza shukrani, wanahabari wenzangu
Gadna G. Habash
Mkurugenzi Machozi Entertainment

Sunday, July 29, 2012

Vijana zaidi ya 300 wajitokeza EBSS jijini Tanga leo


Mshiriki wa Shindano la Epiq Bongo Star Search Digna Mbetela kutoka Dodoma akiwa mbele ya majaji wa shindano hilo (hawapo pichani) walipokuwa wakifanya mchujo mkoani Tanga katika Ukumbu wa Club La Casa Chika Julai 28,2012 na mwana dada huyo kujitosa tena kujaribu bahati yake ya kwenda jijini Dar es Salaam.

 Mwamko wa washiriki katika shindano la Zantel Epiq Bong Star Search umekuwa kama ulivyotegemewa ambapo zaidi ya washiriki 300 walikuwa wameisha jisajiri kwanza kwa ajiri ya kufanya usaili siku ya leo.

Washiriki wengi walioshindwa kupata nafasi katika mikoa usaili uliopitiawamejitokeza katika mkoa wa Tanga kitu ambacho kimeongeza ushindani kwawashiriki kutokea eneo hili la Tanga.
 Washiriki wa EBSS wakiwa nje ya ukumbi wa Club la Casa Chika jijini Tanga tayari kwa kufanya usaili na kupatiwa namba zao kusubiri kuingia kwa majaji.
 Mshewa Mussa akiwakilisha tena baada ya kete yake ya awali mkoani Arusha kugonga mwamba na kuamua kutia maguu jijini Tanga kujaribu bahati yake.
 Washiriki wa EBSS wakiwa nje ya ukumbi wa Club la Casa Chika jijini Tanga kusubiri kuingia kwa majaji.
 Faisal Jafari wa kutoka Tanga nae akisubiri kurusha kete yake kwa majaji.
Mshiriki Hidaya Hanein akiwa katika foleni ya kuingia kwa majaji

Saturday, July 28, 2012

YANGA FC WALAMBA BINGO DHIDI YA AZAM FC

Yanga leo ameweza kulaza chari mtanzania mwenzake katika fainali ya Kagame Cup ilisakatiwa katika Uwanja wa taifa  leo.
Azam Fc amelamba kichambo hicho cha 2-0 mara baada ya kuonesha uzembe wa kiufundi ulioweza kutumiwa vizuri na wapinzani wao kitu kilichopelekea kukubaliana  na hali iliyojili uwanjani hapo
Tutaendelea kukujuza zaidi......................

WACHEZAJI WA YANGA NA RAHA YA UBINGWA WA KAGAME CUP LEO

 Wachezaji wa timu ya Yanga wakishangilia na kombe lao walilokabidhiwa leo mara baada ya kuifunga timu ya Azam FC katika mchezo uliokuwa ni wa kuvutia kwa timu zote baada ya kuitandika timu ya Azam magoli 2-0 kwenye mchezo wa fainali katika michuano ya kombe la Kagame iliyomalizika leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Fullshangweblog na kikosi chake cha kazi inawapa hongera Wachezaji wa timu ya Yanga Uongozi na mashabiki wote wa Yanga pamoja na wanachama kwa kuutwaa ubingwa huo kwa mara ya pili mfurulizo hongereni sana.
 Wachezaji wa timu ya Azam ambayo imechukua nafasi ya pili wakipita jukwaani na kupewa medali zao baada ya mchezo huo kumalizika jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa.
Wachezaji wa timu ya Vita kutoka DRC Congo wakipta jukwaani na kupokea medali zao Vita wamechukua nafasi ya tau baada ya kuifunga timu ya APR ya Rwanda katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu uliofanyika kalba ya mchezo wa fainali.

Thursday, July 26, 2012

Shirikisho la Filamu Tanzania TAFF landaa semina ya mpango mkakati wa miaka mitano



Shirikisho la Filamu TanzaniaTAFF limeandaa Semina ya siku mbili kwa ajili ya kutayarisha mpango Mkakati wa miaka mitano ijayo. Semina hiyo itafanyika katika ukumbi wa Ofisi za  TCRA  Jengo la Mawasiliano Towers ubungo  kuanzia saa 3 asubuhi tarehe  30 – 31, Julai  2012.
Semina hiyo inafuatia baada ya kufanyika ya awamu ya kwanza ambayo ilifanyika 28 – 20 Mei 2012 katika Ukumbi wa Hotel ya White Mark iliyopo eneo la Ubungo Plazza Mjini Dar  es  Salaam.
Aidha Wajumbe wataohudhuria semina hiyo wanatoka taasisi za Benki za N.M.B, CRDB , Backelys Bank, Bank of India, TRA , TCRA, TBS, NSSF , Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Bodi ya Filamu Tanzania, BASATA, COSOTA, ITV Equity Bank, European Union, Foundation for Civil Society, Ubalozi wa Sweden, Uholanzi, US – AID, Global Publishers,               UNESCO, UNICEF, TGNP, T.I.B Mpigile Company , Wizara ya Viwanda Biashara, Tigo, Vodacom, TBL, ADB, TWAWEZA, Ubalozi wa Canada, Ubalozi wa Ufaransa , Ubalozi wa Denmark ,Wasanii kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Morogoro, Mwanza,Pwani na Dodoma..
Malengo ya Semina hiyo ni kujadili na kuweka utekelezaji wa vipaumbele muhimu vya utekelezaji wa majukumu ya Shirikisho la Filamu.

Sunday, July 22, 2012

Shindano la Miss Utalii Kanda ya Ziwa lafutwa


BODI ya Taifa ya Miss Tourism Tanzania Organization (MTTO), imelifuta shindano la Miss Utalii Kanda ya Ziwa 2012, lililo fanyika New Mwanza Hotel, juzi, huku taifa likiwa kwenye maombolezo ya siku tatu kutokana na msiba mkubwa wa ajali ya meli ya Mv Skagit, mjini Zanzibar na kupoteza uhai wa watu wengi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa katika vyombo vya habari jana jijini Dar es Salaam na kutiwa sahihi na Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa Miss Utalii Tanzania, Abubakari Omary Bakari, ilisema shindano hilo limefanyika kimakosa na matokeo yake hayawezi kutambuliwa kwa namna moja ama nyingine.
Alisema uamuzi wa serikali ni wa mwisho, hivyo hawajaunga mkono kufanyika kwa shindano hilo wakati nchi ina majonzi ya kupoteza ndugu na jamaa waliokufa kwenye ajali hiyo.
“Shindano limefanyika bila kuzingatia misingi ya kiubinadamu na uzalendo kwa taifa, hivyo bodi imeamua kulifuta na waandaaji watafuata tena utaratibu mwingine,” ilieleza taarifa hiyo na kuongeza:
“Miss Utalii ni shindano lenye uzalendo, hivyo inapotokea matatizo kama haya na agizo la maombolezo kutoka kwenye serikali nadhani kuna kila sababu ya kuliafiki.”
Shindano hilo limeandaliwa na Fania Beauty Salon, chini ya Mkurugenzi wake Fania Hassan, ambaye sasa ana changamoto nyingine ya kujiweka sawa katika jamii, ukizingatia kwamba taifa lilikuwa kwenye maombolezo ya siku tatu.

Friday, July 13, 2012

REDDS MISS PWANI 2012 KUPATIKANA LEO


 Warembo wanaowania taji la Redd's Miss Pwani wakiwa katika pozi la picha katika kambi yao iliyopo kwenye hoteli ya Apaikunda,iliyopo Kibaha maili moja.Warembo hawa usiku wa leo wanaingia katika kinyang'anyiro hicho kitakachofanyika kwenye ukumbi wa hoteli hiyo.

Thursday, July 12, 2012

Nani zaidi kati ya Msondo na Sikinde kesho dodoma mbele ya wabunge


Bendi kongwe nchini Msondo Ngoma Music na Mlimani Park Orchestra “Sikinde Ngoma ya Ukae”
zinatapambana kesho Ijumaa kuanzia saa moja usiku  kwenye ukumbi wa Klab Lazizi Dodoma.
Pambano hilo ambalo tayari limevuta hisia za mashabiki wa muziki wa dansi nchini ikiwemo wabunge   imeandaliwa kwa ajili ya kujua nani zaidi baada ya mwaka jana kuwa na utata wa nani zaidi ambapo kila mmoja alikua anadai yeye ni zaidi.
Akizungumza na waandishi wa Habari Msemaji wa Bendi Ya Msondo ngoma Rajabu Mhamila Super D' alisema
Onyesho hilo pia ni maalum kwa ajili ya kuwaaga mashabiki wao kwa kuwa tunaelekea mwezi mtukufu wa Ramadhani ambapo wapenzi wa muziki watajumuika kwa pamoja kwenye Ukumbi huo  hivyo kufurahia
Bendi hizo ambazo zina mashabiki wengi nchini kuliko bendi nyingine zozote, zimeahidi kutowaangusha mashabiki wao kwa kila moja ikijinasimu kuwa itaibuka na ushindi.
Mara nyingi bendi hizo zikipambana huwa ni patashika nguo kuchanika, kwani mbali na mashabiki kushangilia bendi wanazozipenda vibweka na vituko kemkem vimekuwa vikitawala.
Sikinde ambayo iliweka kambi jijini Dar es Salaam imejinasibu kuibwaga Msondo na kudai kuwa hivi sasa haitishi kama ile ya miaka kadhaa iliyopita.
Itakuwa ni mara nyingine tena  kupambana 
 katika pambano hilo mbali na kuwakumbuka wanamuziki wao waliofariki, lakini pia itakuwa ni kusherehekea miaka 50 ya Uhuru huku zikiwa bado zinadumu kwani bendi nyingi za rika lao zimeshafutika kwenye ramani ya muziki nchini.

 
Sikinde  inayongozwa na Habibu Jeff  huku Msondo ikiongozwa na Mkongwe wa  muziki nchini Muhidini Gulumo.
Tunataka mashabiki wa bendi zote wajitokeze kwa wingi bila ya kuwa na wasiwasi kwani watapata burudani ya kutosha , kwani watapiga zile nyimbo za zamani wakati bendi hiyo inaanzishwa mwaka 1978 kama vile 'Selina', Wiki endi', 'Penzi la Fukara', 'Hiba', 'MV Mapenzi namba 1 na 2 hadi za kisasa kama vile 'Supu Umelitia Nazi' na 'Jinamizi la Talaka'.
Naye kiongozi wa Msondo Said Mabera maarufu kama Doctor amesema kuwa kama kawaida yao Msondo ni bendi isiyoshindwa daima.
Mabera amesema kuwa siri ya bendi hiyo kupata ushindi miaka yote ni ushirikiano wanaoupata wanamuziki na wapenzi wao.
Wamewataka wapenzi wao kama kawaida yao kujitokeza kwa wingi na kuishangilia kwa nguvu Msondo Ngoma kwani itaporomosha vibao vya enzi za Nuta, Juwata, Ottu hadi Msondo Ngoma.
Baadhi ya nyimbo zao ni 'Nimuokoe nani', 'Zarina', 'Mwanaidi', 'Kanjelenjele', 'Bahati', 'Sesilia', 'Usiue Usiibe', 'Asha Mwana Seif', 'Kauka Nikuvae', Chuma Chikoli Moto', 'Kilio cha Mzima', 'Ajali', 'Suluhu' na nyingine nyingi.
Kikosi cha Sikinde kitakuwa na Hassan Rehani Bitchuka, Hassan Kunyata, Kaingilila Maufi, Tonny Karama, Shaaban Mabuyu, Habib Abassi, Juma Choka, Ally Jamwaka, Athumani Kambi, Mbaraka Othman, Milambo, Shaaban Lendi, Joseph Benard na Ramadhani Mapesa.
Msondo itawategemea akina Shaaban Dede alijiunga hivi karibuni kutoka Sikinde, Mabera, Abdul Ridhiwani Pangamawe, Saad Ally 'Mashine', Eddo Sanga, Huruka Uvuruge, Zahor Bangwe, Ibrahim Kandaya, Ismail Mapanga, James Mawilla, Muhidini Gurumo, Eddo Sanga, Juma Katundu, Hamisi Mnyupe, Roma Mng’ande `Romario’ na Hassan Moshi.


Aidha Super 'D' alimariza kwa kutaja  ratiba yao ya wiki hii kuwa jumamosi watakuwa Kibaha Kontena kwa ajili ya kuwapa burudani mashabiki wake na watamaliza wikiendi katika ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala Dar es salaam siku ya jumapili hivyo wapenzi wajitokeze kwa wingi ili wapate burudani

Sunday, July 8, 2012

CHAMELEONE AONESHA MAKEKE YAKE

CHAMELEONE AFUNIKA TAMASHA LA USIKU WA MATUMAINI NDANI YA UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR

 

Jose Chameleone.
 
 Diamond Platinumz.
Wakali wa Stage Naseeb Abdul 'Diamond Platinumz' na Jose Chameleone 'Dk' wakiwa 'Back Stage' kabla ya kupanda jukwaani kukata kiu ya mashabiki waliofurika Uwanja wa…
Chameleone akiingia uwanjani kuwarusha mashabiki waliofurika Uwanja wa Taifa usiku huu.…
Chameleone akiingia uwanjani kuwarusha mashabiki waliofurika Uwanja wa Taifa usiku huu.
Jose akiimba na maelfu ya wapenzi wa burudani waliofurika ndani ya Uwanja wa Taifa usiku huu.
Sehemu ya maelfu ya wakazi wa jiji la Dar waliokuwa wanafuatilia shoo hiyo.
Mwanamuziki mahiri kutoka nchini Uganda, Joseph Mayanja 'Jose Chameleone' usiku wa leo amefunika vilivyo katika Tamasha la Usiku wa Matumaini lililofanyika ndani ya Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Chameleone aliwarusha mashabiki kwa baadhi ya nyimbo zake za zamani kama Mambo bado, Kipepeo na ile mpya iitwayo Valu Valu inayopendwa na watu wengi hapa Bongo.
(PICHA ZOTE NA WAPIGA PICHA WETU WALIOKUWA UWANJA WA TAIFA/GPL)