Showing posts with label kazi kweli kweli. Show all posts
Showing posts with label kazi kweli kweli. Show all posts

Thursday, June 14, 2012

TRL HAPATOSHI SASA

Dk .Mwakyembe Awasha Moto TRL



Mussa Juma, Dodoma


BAADA ya kusafiri kwa treni kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma, Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe amebaini hujuma nzito katika Shirika la Reli Tanzania (TRL) ikiwamo ofisa mmoja kuwaibia abiria kwa kughushi viwango vya nauli na ameagiza afukuzwe kazi.



Licha ya kuagiza kutimuliwa kwa ofisa huyo, pia alitangaza kuandaliwa utaratibu wa kufanya mabadiliko kadhaa katika kuboresha usafiri huo, ikiwamo kuondoa malipo ya nusu nauli kwa watoto wadogo kuanzia miaka mitatu hadi miaka 10 na pia kuondolewa kwa utaratibu wa malipo ya mizigo midogo ya abiria.



Juzi, Dk Mwakyembe ambaye tayari amewang’oa vigogo wanne wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), aliamua kusafiri kwa treni hadi Dodoma akitokea Dar es Salaam ili kujionea utendaji kazi wa shirika hilo.



Mara baada ya kuwasili katika Stesheni ya Dodoma saa 1:30 asubuhi, Waziri Mwakyembe alizungumza na waandishi wa habari na kusema akiwa katika safari hiyo, amepata fursa za kutembelea mabehewa yote na kuzungumza na abiria.



Dk Mwayembe alisema ingawa safari ilikuwa nzuri, kuna mengi ambayo ameyabaini ambayo ni pamoja na abiria kulipa nauli kubwa na kuandikiwa tiketi tofauti jambo ambalo alisema ni wizi na kamwe wizara yake haiwezi kulifumbia macho.



“Unakuta nauli halali ni Sh9,000 lakini, abiria ameandikiwa Sh29,000. Sasa nimeagiza huyu anayehusika afuatiliwe na kujulikana na nipewe taarifa ameondolewa,” aliagiza Dk Mwakyembe.

Alisema pia katika safari hiyo, alibaini uchakavu mkubwa wa mabehewa na hakuna tofauti ya daraja la tatu na la kwanza, upungufu mwingine ni katika utendaji na taratibu jambo ambalo linapaswa kuchukuliwa hatua.



Dk Mwakyembe alisema si vyema mtoto kuanzia miaka mitatu kulipishwa nusu nauli, kwani taratibu zinapaswa kufanywa ili hadi mtoto wa miaka 10 ikiwezekana asilipishwe nauli kwani treni ndiyo usafiri wa umma.



Kuhusu mizigo, alisema kwa sasa mizigo ya abiria inalipiwa kwa kilo kama ilivyo usafiri wa ndege jambo ambalo si sawa kwani mzigo wa abiria kuanzia kilo 20 unalipishwa jambo ambalo linapaswa kuangaliwa.



“Usafiri huu mimi nasema ndiyo wa umma hivyo, tusizuie watu kupeleka hata zawadi nyumbani kwao ni vyema tuwe na utaratibu walau mizigo kidogo ya abiria isilipiwe,” alisema Dk Mwakyembe.

Wednesday, June 13, 2012

MUNGU TUSAIDIE VENGU WETU APONE



Na Mwandishi Wetu
WAKATI afya ya staa wa filamu Bongo, Sadick Juma Kilowoko ‘Sajuki’ ikiendelea vizuri baada ya kupata matibabu nchini India, kuna utata juu ya maendeleo ya afya ya mchekeshaji maarufu nchini, Joseph Shamba ‘Vengu’ ambaye naye yuko nchini humo kwa matibabu, Risasi Mchanganyiko lina kitu cha kueleza.
Habari ambazo hazina ganzi hata chembe zinadai kuwa hali ya msanii huyo wa Kundi la Orijino Komedi imekuwa ya giza mbele ambapo nduguze waishio Dar hawajui nini kinaendelea.
Katikati ya mwezi Mei, ilidaiwa Vengu angerejea nchini wakati wowote baada ya afya yake kutengemaa, lakini ndugu mmoja wa karibu (jina lipo) akasema imeshindikana kuruhusiwa baada ya hali ya msanii huyo kubadilika ghafla.
“Ilikuwa arudi nyumbani kweli, maana kidogo alikuwa anaridhisha, lakini ghafla hali ikabadilika tena, kwa hiyo hatarudi kwa sasa,” alisema ndugu huyo.
Kwa mujibu wa habari za ndani, hali ya Vengu ni kama bahari kupwa na kujaa, kwani kuna wakati analeta matumaini lakini ‘vikicharuka’ anakuwa kama alivyoondoka Tanzania.
Awali Vengu alilazwa kwa muda mrefu Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) akikabiliwa na ugonjwa uitwayo Brain au Cerebral Atrophy. Ugonjwa huu husababisha seli za kichwani kukosa mawasiliano na sehemu nyingine na mgonjwa huzimia mara kwa mara.
Akiwa hospitalini hapo, hali ilizidi kuwa mbaya hivyo ‘komediani’ huyo alikimbizwa katika Hospitali ya Apolo iliyopo nchini India kwa matibabu zaidi.
Kwa upande wake, Sajuki alikwenda Mumbai, India katikati ya Mei mwaka huu kutibiwa matatizo ya uvimbe tumboni. Alirejea Bongo, Juni 6 mwaka huu akiwa anaendelea vizuri.

Saturday, April 28, 2012

TANROADS YASAINI MKATABA WA TSH BILIONI 12.34 UJENZI WA DARAJA LA MBUTU

Na Ismail Ngayonga

MAELEZO

Dar es Salaam


SERIKALI kupitia Wakala wa Barabara Nchini (Tanroads) imesaini mkataba na makampuni 13 ya wakandarasi wa ndani kwa ajili ya ujenzi wa daraja la Mbutu lililopo katika Wilaya ya Igunga mkoani Tabora.

Akizungumza kabla ya utiaji saini mkataba huo jana (juzi), Mtendaji Mkuu wa Tanroads Mhandisi Patrick Mfugale alisema ujenzi wa daraja hilo utagharimu kiasi cha Tsh. Bilioni 12.34 na unataraji kukamilika mwezi Septemba mwaka 2013.

Alitaja wakandarasi hao 13 waliounda umoja wa ujenzi wa mradi daraja hilo kuwa ni Skol Building Contractors Ltd, Del Monte (T) Ltd, Mayanga Contractors Company Ltd, Casco Construction Ltd, Electrics International Company Ltd, Kika Construction Company Ltd.

Wakandarasi wengine ni Gemen Engineering Company Ltd, Milembe Construction Company Ltd, Lukolo Company Ltd, Mac Contractors Co. Ltd, Nyakirang’anyi Construction Ltd, Nyegezi J.J Construction Ltd na Concrete Meters Company (T) Ltd.

Mhandisi Mfugale aliwataka wakandarasi kujenga daraja hilo katika ubora na viwango walivyojiwekea kwani la Serikali la kuwatumia wakandarasi ni pamoja kupunguza gharama za miradi ya ujenzi wa barabara na pia kutoa kipaumbele kwa wakandarasi wazalendo.

Akifafanua kuhusu ujenzi huo, Mhandisi Mfugale alisema daraja hilo litajengwa kwa zege la simenti na litakuwa na urefu wa mita 40 na upana wa mita 10.7. “Daraja litakuwa na uwezo wa kubeba uzito wa juu kabisa unaokubalika kisheria hapa nchini ambao ni tani 56” alisema.

Aidha alisema kuwa mradi huo pia utahusisha ujenzi wa makaravati 7 ya zege yenye upana wa mita 8 hadi 14 pamoja na ujenzi wa tuta la barabara lenye urefu wa kilomita 3 kwa kiwango cha changarawe.

Kwa mujibu wa Mhandisi mfugale alisema matarajio ya Serikali ya kutekeleza mradi huo ni kuhakikisha kuwa panakuwapo mawasiliano ya uhakika ya barabara katika vipindi vyote vya mwaka kati ya vijiji vilivyopo katika tarafa ya Igurubi yenye wakazi zaidi ya 94,449 na mji wa Igunga.

Kukamilika kwa mradi huu kutachochea ukuaji wa shughuli za kiuchumi na kijamii kwa wananchi wa Igunga ambao hujishughulisha na kilimo cha mazao ya biashara na chakula yakiwemo pamba, mahindi, mtama, viazi na dengu.

Kwa upande wake, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mhandisi Dk. John Ndunguru alisema Serikali ilianza kutenga fedha ya ujenzi wa mradi huo katika mwaka wa fedha 2011 na kuikamilisha katika mwaka wa fedha 2012.

Aidha Dk. Ndunguru aliitaka Tanroads kusimamia kwa karibu kazi ya ujenzi huo na kuhakikisha kuwa inafanywa kwa ubora na kuzingatia muda uliowekwa.

“Ni matumani yangu kuwa malengo yaliyokusudiwa ya utekelezaji wa mradi, ambayo ni kuimarisha mawasaliano ya barabara kwa vipindi vyote vya mwaka yatafikiwa’’ alisema Dk. Ndunguru.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wakandarasi Nchini CRB), Bi. Consolata Ngimbwa aliishukuru Serikali kwa kusikia kilio cha wakandarasi wazalendo na kuahidi bodi itawasimamia wakandarasi hao ili kuhakikisha kuwa kazi ya ujenzi huo itafanyika katika viwango vinavyotakiwa.

“Wakandarasi wenzangu mmepewa fursa ambayo wengine waliitaka na hamna budi kutambua kuwa wenzetu wapo nyuma yenu kutazama kile mnachokifanya” alisema.

Mwaka 2006 mvua kubwa ilinyesha Wilayani Igunga kuharibu madaraja ya Mbutu na hivyo kukatisha mawasiliano kati ya tarafa za Igurubi na makao makuu ya Wilaya ya Igunga.

Monday, April 9, 2012

ROMA HAWASHA MOTO PASAKA NDANI YA UKUMBI WA LINA'S NIGHT CLUB

 Ilikuwa ni burudani ya aina yake kutoka kwa msanii wa muziki wa Hip hop Ibrahim Mussa “Roma Mkatoliki” Usiku wa Pasaka ndani ya Club Linas mjini Bukoba, chini ya Tang Records,bukobawadau  na Linas night Club(Jimy Yeyoooo
 wadau wakichill ndani ya Linas Night Club wakati wa show
 Wadau wakiwa katika show
 Mashabiki wakimtuza Roma
 Muonekano wa Club linas wakati wa show
 Ma-Deejay kazini
 Mashabiki wakijirusha na ngoma za Roma
 Wadau wakiwa cool
Roma akiwasha moto Club Linas
 


Ni baada ya uvumilive kushindikana wadau wakaamua kuonesha walivyonavyo.


Mdada shabiki wa kwanja za Hip hop akipagawa na Tshert  aliyotupia mshkaji yenye maneno "I LOVE HIP HOP" hapa kazi hipo...