Tuesday, April 17, 2012

MAANDALIZI NA JINSI YA KUTENGENEZA TOGWA MPAKA INAKUJA KUWA LUBISI THEN NK`ONYAGI (GONGO YA KIENYEJI)

Kitendo cha kwanza ni kutengeneza togwa maarufu kama okujunga omuramba

Ni kinywaji kama vinywaji vingine katika Dunia hii na kama haitoshi kwa asilimia kubwa watu waliongazi za juu wamesomeshwa na wazazi wake kupitia bihashara ya kuuza Mlamba +Lubisi+Gongo ambayo ndiyo mwisho.
Nchi kama  China wanahita Kalinya na wanatumia hasa wakati wakiwa wanafanya kazi ngumu ,uwasaidia kuongeza nguvu pamoja na msisimuko wa kuweza kufanya kazi zaidi.
Kwa Nchi kama Tanzania Gongo ni alamu kisheri  ingawaje wapo watu na wahasisi wa nchi hii wamepata elimu kupitia bihashara hii na kama haitoshi pia inaweza tumika kama dawa hasa kama tumbo limevuligika.
VIFAA VINAVYOITAJIKA
  1.   Ndizi kali (embile)
  2. Nyasi (ebinyasi)
  3. Mtumbwi (obwato)
  4. Maji
  5. Makuti ya migomba (ebishansha)
  6. Mtama (omugusha)
Kwa pamoja vinasaidia kutengeneza Obulamba

HATUA ZINAZOFANYIKA
  1. Kutindika ndizi kali (okualika) .hapa inasemekana baada ya siku kumi na nne ndizi kali zinakuwa tayari kwa ajiri ya kutumiwa  
  2. Kuandaa Mtumbwi (obwato) ni kwa ajiri ya kuweza kupata sehemu ya kuweka ndizi kali hapa kifaa hiki kinaweza kuchuka ha lita 300 hadi mia tano kwa mjibu wa maelezo ya wazee wa zamani na wazoefu katika hili
  3. Kusaga mtama.
  4. Kuandaa maji haya ni kwa ajiri ya kuweza kupunguza ukali wa ndizi kali ambazo tayari zinakuwa zimezalisha omulamba (togwa)
  5. Mtu atakayekanyagia ndizi hizo hadi zinatoa togwa.Ni kitendo kinachohitaji nguvu kwani bila nguvu mambo yanaweza kualibika (OKUKOKA) ni jina la kiruga kihaya  kwa  maana (kuharibika).
  6. Mwisho ni kuweka ndizi kali kwenye mtumbwi baada ya hapo wanaweka majani ili yasaidi katika kulainisha ndizi kali  na hatimaye kutoa mlamba ambao huitwa omunene.Mara baada ya muda uchanganywa na maji na kuhitwa Kaizi.Sasa tayari kwa kuchanganya na Mtama ili kutengeneza Olubisi.Hapa huachwa kwenye mtumbi kwa kipindi kisichopungua masaa 24 hadi 30 baada ya hapo tayari lubisi (OMUTAGATA)inakuwa iko tayari.Kitendo cha okutaa(kutoa Lubisi) ndicho kinafuataia.
  7. Baada ya lubisi kuwa imetengenezeka huachwa kwa mta husiopungua siku tatu hadi nne ambapo huitwa OMULALA.
hatua ya mwisho ni kutengeneza gongo wanasayansi wanajua hili 
Unaweza kutuongeza ujuzi kwa kupitia njia ya maoni ili kuwaelimisha wengine na kusaidia watu kukumbuka wapi walitoka.

No comments: