“Ni jambo ambalo ameomba mwenyewe kuhamia huko na ameruhusiwa maana hilo ni jambo la kawaida kama ambavyo wajumbe wengine kama kina Freeman Mbowe waliwahi kuomba, siyo jambo geni.” Hamad Rashid Mohamed Na James Magai na Neville Meena, MwananchiKesi hiyo ilifunguliwa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam jana na Mwandishi wa Habari Saidi Kubenea, kupitia kwa wakili wake Peter Kibatala, dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).Dar es Salaam/Dodoma. Bunge la Katiba linaloendelea mjini Dodoma kwa sasa liko katika hatihati ya kuendelea baada ya kufunguliwa kesi ya kuhoji madaraka yake.Kesi hiyo ilifunguliwa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam jana na Mwandishi wa Habari Saidi Kubenea, kupitia kwa wakili wake Peter Kibatala, dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).Katika kesi hiyo iliyopewa usajili wa namba 28 ya mwaka 2014, Kubenea anaiomba mahakama hiyo itoe tafsiri sahihi ya Mamlaka ya Bunge la Katiba. Kubenea amefungua kesi hiyo akiomba mahakama itoe tafsiri hiyo, chini ya vifungu vya 25 (1) na 25 (2) vya Sheria ya Marekebisho ya Katiba namba Namba 83 ya mwaka 2011.Sambamba na kesi hiyo ya kuomba tafsiri ya mamlaka ya Bunge hilo, pia Kubenea amewasilisha maombi mahakamani hapo akiiomba mahakama itoe zuio la muda la kusimamisha Bunge hilo ili kusubiri uamuzi wa maombi ya tafsiri hiyo.Maombi hayo ya kusimamisha Bunge hilo kwa muda yaliyopewa usajili wa namba 29 ya mwaka 2014, pamoja na maombi ya msingi ya tafsiri ya mamlaka ya Bunge yote yalifunguliwa mahakamani hapo jana chini ya Hati ya Dharura.Katika kesi hiyo ya msingi anaiomba Mahakama hiyo itoe tafsiri sahihi ya masharti ya vifungu hivyo vya sheria hiyo na pia itamke kama Bunge hilo lina mamlaka ya kubadilisha maudhui ya Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kwa kiwango gani.Kwa mujibu wa hati ya madai, Kubenea anadai kuwa msingi wa kesi hiyo unatokana na uamuzi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Desemba Mosi, 2011, lililopitisha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba. Anasema sheria hiyo ilikuwa na lengo la kuratibu mchakato wa kutungwa kwa Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Anaendelea kusema kuwa kutokana na sheria hiyo, Rais aliunda Tume ya Mabadiliko ya Katiba pamoja na mambo mengine vilevile kukusanya maoni ya wananchi kuhusu mapendekezo ya Katiba Mpya na kwamba kwa msingi huo Tume hiyo iliandaa Rasimu ya Katiba.Anadai kuwa baada ya Tume hiyo kuundwa iliendelea kukusanya maoni ya wananchi yaliyotolewa katika mikutano ya hadhara na katika miundo tofauti ikiwamo mabaraza ya Katiba yaliyoanzishwa kila wilaya kwa lengo hilo.Hati hiyo inaendelea kueleza kuwa kwa mujibu wa takwimu halisi za tume hiyo, jumla ya watu 333,537 walitoa maoni yao katika nyanja tofauti, tofauti za mapendekezo ya Katiba, ambayo ndiyo Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyatumia kuandaa Rasimu ya Katiba Mpya.Inaendelea kueleza hati hiyo kuwa baada ya Rais kukabidhiwa rasimu ya mwisho Desemba 8, 2013, kwa mujibu wa vifungu vingine vya sheria hiyo, aliunda Bunge la Katiba kwa lengo la kujadili Rasimu ya Katiba na hatimaye kupata Katiba Mpya.
FOUR WAYS INTERNET & STATIONERY WANASHUGHULIKA NA USAMBAZAJI WA VIFAA VYA SHULE NA MAHITAJI MENGINE YA MAOFISINI IKIWA NI PAMOJA NA HUDUMA YA INTERNET MASAA 17 KWA SIKU INAFUNGULIWA SAA 7:00 HADI SAA 10:00 USIKU K A R I B U S A N A
Showing posts with label siasa. Show all posts
Showing posts with label siasa. Show all posts
Saturday, August 23, 2014
Kesi yafunguliwa Bunge la Katiba, Kesi ya kuhoji uhalali wake yafunguliwa
“Ni jambo ambalo ameomba mwenyewe kuhamia huko na ameruhusiwa maana hilo ni jambo la kawaida kama ambavyo wajumbe wengine kama kina Freeman Mbowe waliwahi kuomba, siyo jambo geni.” Hamad Rashid Mohamed Na James Magai na Neville Meena, MwananchiKesi hiyo ilifunguliwa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam jana na Mwandishi wa Habari Saidi Kubenea, kupitia kwa wakili wake Peter Kibatala, dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).Dar es Salaam/Dodoma. Bunge la Katiba linaloendelea mjini Dodoma kwa sasa liko katika hatihati ya kuendelea baada ya kufunguliwa kesi ya kuhoji madaraka yake.Kesi hiyo ilifunguliwa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam jana na Mwandishi wa Habari Saidi Kubenea, kupitia kwa wakili wake Peter Kibatala, dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).Katika kesi hiyo iliyopewa usajili wa namba 28 ya mwaka 2014, Kubenea anaiomba mahakama hiyo itoe tafsiri sahihi ya Mamlaka ya Bunge la Katiba. Kubenea amefungua kesi hiyo akiomba mahakama itoe tafsiri hiyo, chini ya vifungu vya 25 (1) na 25 (2) vya Sheria ya Marekebisho ya Katiba namba Namba 83 ya mwaka 2011.Sambamba na kesi hiyo ya kuomba tafsiri ya mamlaka ya Bunge hilo, pia Kubenea amewasilisha maombi mahakamani hapo akiiomba mahakama itoe zuio la muda la kusimamisha Bunge hilo ili kusubiri uamuzi wa maombi ya tafsiri hiyo.Maombi hayo ya kusimamisha Bunge hilo kwa muda yaliyopewa usajili wa namba 29 ya mwaka 2014, pamoja na maombi ya msingi ya tafsiri ya mamlaka ya Bunge yote yalifunguliwa mahakamani hapo jana chini ya Hati ya Dharura.Katika kesi hiyo ya msingi anaiomba Mahakama hiyo itoe tafsiri sahihi ya masharti ya vifungu hivyo vya sheria hiyo na pia itamke kama Bunge hilo lina mamlaka ya kubadilisha maudhui ya Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kwa kiwango gani.Kwa mujibu wa hati ya madai, Kubenea anadai kuwa msingi wa kesi hiyo unatokana na uamuzi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Desemba Mosi, 2011, lililopitisha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba. Anasema sheria hiyo ilikuwa na lengo la kuratibu mchakato wa kutungwa kwa Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Anaendelea kusema kuwa kutokana na sheria hiyo, Rais aliunda Tume ya Mabadiliko ya Katiba pamoja na mambo mengine vilevile kukusanya maoni ya wananchi kuhusu mapendekezo ya Katiba Mpya na kwamba kwa msingi huo Tume hiyo iliandaa Rasimu ya Katiba.Anadai kuwa baada ya Tume hiyo kuundwa iliendelea kukusanya maoni ya wananchi yaliyotolewa katika mikutano ya hadhara na katika miundo tofauti ikiwamo mabaraza ya Katiba yaliyoanzishwa kila wilaya kwa lengo hilo.Hati hiyo inaendelea kueleza kuwa kwa mujibu wa takwimu halisi za tume hiyo, jumla ya watu 333,537 walitoa maoni yao katika nyanja tofauti, tofauti za mapendekezo ya Katiba, ambayo ndiyo Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyatumia kuandaa Rasimu ya Katiba Mpya.Inaendelea kueleza hati hiyo kuwa baada ya Rais kukabidhiwa rasimu ya mwisho Desemba 8, 2013, kwa mujibu wa vifungu vingine vya sheria hiyo, aliunda Bunge la Katiba kwa lengo la kujadili Rasimu ya Katiba na hatimaye kupata Katiba Mpya.
Thursday, August 21, 2014
Monday, September 17, 2012
ZANZIBAR NAKO PAZUKA VURUGU ZA UCHAGUZI MDOGO BUBUBU
Vurugu hizo ambazo kwa kasi zilifanyika katika kitucha shule ya Bububu iliyoko Zanzibar
Kiongozi wa chana cha siasa akiongea na waandishi wahabari nje ya kituo cha kupihia kura
Thursday, September 6, 2012
Tendwa Atamani Kuifuta CHADEMA
Msajili wa vyama vya siasa nchini John Tendwa amesema sasa amechoka kusikia mauaji kwenye mikutano ya kisiasa ya CDM na atatumia rungu lake kufutia usajili chama chochote kitakachoshindwa kutunza amani ya nchi.Tendwa amewaambia waandishi wa habari hatishiki na chama chochote kuwa na wabunge kwani sheria inamruhusu kufuta chama hata kama kina wabunge 100.
Katika hali ya kushangaza Tendwa ameshauri vyama visubiri nyakati za uchaguzi ndipo vifanye mikutano ya kisiasa.Hata hivyo amekiri sheria inaruhusu vyama kufanya mikutano na maandamano wakati wowote.
Source:Habari Radio Tumaini.
Monday, September 3, 2012
Sitta ageukwa CCM, Aibuka kumjibu Dk. Slaa,

SIKU moja baada ya Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa kumrushia kombora zito Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Hamis Mgeja amemtaka waziri huyo na wabunge wengine 55 wapime, watafakari na hatimaye wachukue hatua kwa kuondoka ndani ya CCM.
Mgeja ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, amesema tuhuma zilizotolewa na Dk. Slaa dhidi ya Sitta na wabunge hao, zinathibitisha jinsi kiongozi huyo na wenzake walivyo wasaliti ndani ya chama chao na serikali, na kwamba kitendo cha kuigeuza ofisi ya spika kuwa kijiwe cha kupanga uhaini na usaliti ndani ya CCM hakivumiliki hata kidogo.
Mgeja alitoa kauli hiyo jana jijini Mwanza, alipozungumza na waandishi wa habari kwa lengo la kumpongeza Dk. Slaa kwa kufichua uozo wa Waziri Sitta na wenzake hao. Alisema Dk. Slaa ameisaidia CCM kutambua viongozi wake wanaokisaliti.
"Nianze kwa kumpongeza Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Slaa kwa kufichua madhambi ya Samuel Sitta. Huyu mtu (Sitta), ni hatari sana katika maendeleo ya chama chetu.
"Dk. Slaa ametueleza jinsi Sitta alivyotumia ofisi ya spika kama kijiwe cha kutaka kukisaliti chama chetu na kuanzisha CCJ. Huyu mtu ni hatari sana... tunaomba CCM imtose yeye na wabunge hao 55 maana uroho wao wa madaraka unaweza kuigharimu CCM.
"Kwa kashfa hii nzito dhidi yao, namshauri wapime, watafakari na hatimaye wachukuwe hatua. Pia nawashauri kwanza watubu na kuomba radhi chama na wana CCM wote, au wajiengue kwa hiari yao bila shuruti, ili walinde heshima yao. Wasingoje kuhukumiwa na wanachama," alisema.
Mjumbe huyo wa NEC na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga aliyejipambanua kupiga vita ufisadi na vitendo viovu ndani na nje ya CCM, alisema historia ya Waziri Sitta inajionesha wazi kwamba ni 'mkorofi na msaliti mkubwa', kwani mwaka 1966 akiwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alishiriki maandamano hadi Ikulu kupinga sheria ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Alisema katika harakati zao hizo za kupinga sheria hiyo iliyotaka kila mwanafunzi wa Chuo Kikuu lazima ajiunge na Jeshi la Kujenga Taifa, Baba wa Taifa wakati huo akiwa Rais wa nchi na mkuu wa chuo hicho, alilazimika kumchapa viboko Sitta kutokana na usaliti wake huo kwa serikali.
Mgeja alisema mbali na kufanya maandamano hayo, Sitta na wenzake ambao wengine ni marehemu kwa sasa walikuwa na mabango yenye ujumbe mkali kwa serikali, ukiwemo uliosema 'Onyo kali na la mwisho kwa serikali', na kwamba alikuwa akiipinga pia Serikali ya Baba wa Taifa huku akiusifu uongozi wa kikoloni.
"Huyu Sitta ambaye leo hii anawadanganya watu, kipindi hicho akisoma Chuo Kikuu alikuwa akiipinga serikali na kudai afadhali serikali ya kikoloni. Tusipoamini leo usaliti wake huu tunasubiri hadi aje shetani atuambie usaliti wa Sitta ndipo tuamini?
"Za mwizi ni 40, ndiyo maana tumeambiwa toka mwaka 2005 hadi 2010 huyu Sitta amekuwa akikisaliti chama chetu kupitia Bunge alilokuwa akiliongoza. Tunataka chama kimtose na kisiwaonee haya wasaliti hawa wakubwa. Wasipoondoka kwa hiari yao wataondolewa kwa nguvu ya wanachama wa CCM,” alisema.
Alimtuhumu pia Waziri Sitta kwa kauli zake za kulalamikia serikali bila kutafuta ufumbuzi wa matatizo yanayolikumba taifa, na alimtaka ataje jinsi alivyoisaidia serikali kupunguza tatizo la ajira kwa vijana, mfumuko wa bei, ufisadi na mambo mengine ndani ya chama na serikali.
Kwa mujibu wa Mgeja anayedaiwa kuanza kuundiwa mbinu chafu za kutaka kuangushwa katika kinyang'anyiro cha uenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga na kundi la kigogo mmoja anayetajwa kutaka kugombea urais mwaka 2010, tuhuma hizo dhidi ya Waziri Sitta zimekisaidia maradufu chama, kwani siyo Dk. Slaa pekee aliyewahi kumshutumu kiongozi huyo kwa usaliti ndani ya chama.
Alisema yupo tayari kusulubiwa, kutolewa kafara au kufukuzwa na chama kwa kusema ukweli daima, kwani anayasema hayo kwa kufuata kiapo cha katiba ya CCM.
Sitta amjibu Dk. Slaa
Waziri Sitta amemjibu Dk. Slaa akimwita dikteta na asiye na uvumilivu na kwamba ana hulka ya kujisikia kuwa mawazo yake hayapingwi.
Waziri Sitta amemwita Dk. Slaa kuwa ni mzushi, asiyeogopa kusema na kupindisha mantiki ya jambo ili tu kushinda hoja.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari aliyoitoa jana, Sitta alisema amesikitishwa na kauli hizo za Dk. Slaa alizoziita za jazba na mwangwi wa kiwewe alipokuwa Iringa juzi hadi akafikia hatua ya kumwita mnafiki, mwongo, mtu wa hatari n.k
“Hali hii inatia shaka juu ya uwezo wa kiongozi huyo wa kisiasa kuhimili kukosolewa ambayo ni sifa muhimu ya maisha ya mwanasiasa yeyote hususani anapojinadi kuwa anaweza kuchukua madaraka ya kuiongoza nchi.
“Iweje mtu aliyenibembeleza nigombee urais kupitia chama chake mwaka juzi leo aseme sifai kuongoza hata kata kwa sababu tu nimetamka ukweli juu ya udhaifu wa chama chake cha siasa?” alihoji Sitta.
Alieleza kuwa aliyoyasema Karagwe majuzi katika uchambuzi wake wa vyama vya siasa nchini ni kwamba CHADEMA wamekuwa hodari wa kukosoa na kuishambulia CCM na serikali zake lakini wanasahau kuwa ili wawe mbadala kwa kuiongoza nchi hawana budi kurutubisha safu yao ya uongozi na uwe na watu wa kutosha kuweza kushika madaraka ya ngazi mbalimbali.
“Kuukataa ukweli kwamba safu ya uongozi wa CHADEMA ni nyembamba ni kujidanganya tu. Kupita mikoani kutangaza kwamba matatizo yote ya wananchi yanatokana na CCM ni kazi rahisi na ina mvuto wake kisiasa, lakini mwanasiasa makini hana budi kwenda mbele zaidi ya hapo,” alisema Sitta katika taarifa yake.
Alimtaka Dk. Slaa kueleza wapiga kura mipango ya chama chake inayoeleweka na inayotekelezeka na iliyo makini kukabiliana na changamoto mbalimbali za maendeleo ya nchi.
Amgwaya Mbowe
Kuhusu Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, Sitta alionyesha kumgwaya akieleza kuwa katika hotuba yake hakukejeli uzoefu wa kiongozi huyo wala hakusema ni mcheza disko.
“Niliuchambua wasifu wa viongozi wa CHADEMA na kutamka uzoefu wa Mhe Mbowe katika vitega uchumi vya burudani, hii siyo kudharau bali ni kutamka ukweli tu.
“Huwezi kuuelezea wasifu wa Mhe Mbowe bila kuelezea mchango wake mkubwa katika tasnia ya burudani,” alisema.
Alieleza kuwa mmoja wa marais maarufu wa Marekani, Ronald Reagan, alikuwa ni mcheza sinema. Na hapa Tanzania kulikuwa na Rashidi Kawawa (sasa marehemu) ambaye alianzia katika tasnia ya uigizaji hivyo Mbowe au Dk. Slaa wanaweza wakawa marais wa nchi kwa maana ya kupigiwa kura za uchaguzi wa demokrasia.
“Kumudu au kutoyamudu madaraka hayo ni suala tofauti. Tathmini yangu ilihusu safu nzima ya uongozi wa CHADEMA kwa ujumla wao. Ni safu nyembamba mno,” alisema Sitta.
Kujiunga na CHADEMA
Kuhusu suala hilo, alisema CHADEMA walifanya jitihada ya kumshawishi aingie kwenye chama hicho kwenye uchaguzi wa mwaka 2010 na ili awe mgombea wao wa urais.
“Jambo hili nililitafakari na kutafuta ushauri kwa watu wangu wa karibu na nikabaini kwamba; CHADEMA wana migawanyiko yao ya uongozi tena ni ya hatari kwa sababu ni ya kikanda za nchi – yaani nani anatoka wapi.
“Kutokana na yaliyomo katika ilani yao ya uchaguzi 2010 – 2015 nilibaini mambo ya kiitikadi ambayo siyakubali kama vile sera ya majimbo,” alisema Waziri Sitta.
Alisema sera ya majimbo inawezekana katika nchi ambazo ni tajiri na pia isiyo na tofauti kubwa ya hali ya maisha baina ya kanda mbalimbali za nchi kama vile Marekani.
Sitta alisema kuleta majimbo Tanzania ambako kuna tofauti kubwa za kimaendeleo baina ya Kaskazini, Mashariki, Kati, Kusini na Magharibi ni kusababisha nchi ichanike vipande vipande.
Kuhusu CCJ
Alisema kama ilivyo kawaida kwa vyama vya siasa kutafuta wagombea bora, CCJ ni miongoni mwa vyama vilivyomtafuta na baadhi ya wanasiasa wengine wakati wa maandilizi ya uchaguzi mkuu.
“Jambo hili si la siri wala la ajabu na nimelizungumza hili mara nyingi. Isitokee katika mfumo wa vyama vingi vya siasa mtu kutoka chama kumoja cha siasa na kujiunga na chama kingine haiwezi kusemwa kuwa ni uhaini,” alisema Sitta.
Alisema kama angeridhika na mambo yao angejiunga na CCJ mwaka 2010 lakini hakufanya hivyo.
Alieleza kuwa ni uzushi usio na msingi kumuhusisha na uanzishaji wa chama hicho kwani waanzilishi wa chama hicho cha siasa wanajulikana na wapo hai lakini alieleza kuwa ni haki ya kikatiba ya kila Mtanzania kuanzisha au kujiunga Binafsi na chama chochote cha siasa. Hata hivyo mmoja wa waanzilishi wa CCJ, Fred Mpendazoe, alimtaja Sitta kama mwasisi mwenzake ambaye hakutaka kujitokeza hadharani kabla chama hakijapewa usajili wa kudumu.
Kuhusu madai yake ya kutamka kwamba angehamia CHADEMA na wabunge wa CCM 55 alisema hizo ni porojo za Dk. Slaa kama ulivyo usemi ‘ningeihama CCM siku chache kabla ya kuvunjwa Bunge la 9’.
“Inashangaza kwa Dk. Slaa kukejeli uendeshaji wa Bunge la 9 ambalo ndilo lililowapa fursa watu kama yeye kujulikana na kujipatia umaarufu,” alisema Sitta.

Wednesday, August 29, 2012
ASEMAVYO MWANACHADEMA KUHUSU MAUAJI YA RAIA MOROGORO
Mbunge wa jimbo la Ubungo Jijini Dar es Salaam John Mnyika akipanda jukwaani
Tunalaani vikali mauaji yaliyofanywa leo na Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro katika harakati za kuzuia Maandamano ya amani ya CHADEMA. Ikumbukwe kuwa tulitaka kuzindua Operesheni Sangara tarehe 08/08/2012 Morogoro Mjini, RPC akakataa kwa sababu ya sherehe za nane. Baada ya majidiliano ya viungozi wetu Wakuu na IGP tulikubaliana kwenda kuzindua Operesheni yetu Jimbo la Kilombero-Ifakara kwa makubali
ano kuwa tutafungia Operesheni yetu Morogoro Mjini kwa maandamano.
Tulipotaka kufunga jana tarehe 26/08/2012 busara ikatushauri tupishe zoezi la sensa na tufunge tarehe 27/08/2012 na tukakubaliana na RPC hivyo tarehe 25/08/2012. Jana jioni ndio RPC anakataa kusiwe na maandamano na badala yake viongozi ndio wawe kwenye msafara wa magari kwani eti shughuli za Morogoro zitasimama. Alipokumbushwa makubaliano akawa na kiburi cha Madaraka.
Leo asubuhi wakati watu wanakusanyika ili wajue namna ya kufanya ndipo Polisi wakaanza kuwatawanya kwa mabomu ya machozi na Risasi za Moto hadi kuuwa raia. MUNGU AILAZE PEMA ROHO YA MAREHEMU ALLY ZONA PEPONI. DAMU YAKO HAIJAMWAGIKA BURE KAMANDA ITAKUWA SABABU YA UKOMBOZI WA TAIFA HILI
PANTALEO ANSELEM

Vuta Nikuvute Baina Ya Polisi Na Chadema Imehamia Iringa
VUTA nikuvute baina ya Polisi na Chadema imehamia Iringa, ambako jeshihilo limezuia maandamano na mikutano yote ya chama hicho iliyokuwa imepangwa kufanyika kwa siku nane kuanzia jana.
Amri hiyo ya polisi imekuja siku moja baada ya kutokea vurugu kubwa mjini Morogoro, baina ya wafuasi wa chama hicho na polisi na kusababisha kifo cha mtu mmoja na wawili kujeruhiwa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Michael Kamhanda alisema jana kuwa wameamua kuzuia maandamano na mikutano ya Chadema iliyopangwa kuanza jana kutokana na Sensa ya Watu na Makazi.
“Kutokana na hali halisi ya Sensa, tumeamua kuzuia maandamano na mikutano yote ya vyama vya kisiasa mkoani Iringa wakiwamo hawa watu wa Chadema,” alisema.
Alisema kabla ya kuwazuia, walikutana na viongozi wa chama hicho Wilaya ya Iringa na kuwataka wazuie mikutano yao, jambo ambalo alisema walilikubali kwa ‘mbinde’.
Dk Slaa: Wametuomba
Awali, akiwa Mjini Morogoro, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema polisi wamekiomba chama hicho kusitisha maandamano na mikutano yake iliyopangwa kufanyika mkoani Iringa kupisha Sensa ya Watu na Makazi.
Alisema Chadema imekubali ombi hilo lililotolewa na Mkuu wa Polisi, IGP Said Mwema hivyo kuamua kusitisha mkutano wake uliopangwa kufanyika katika Viwanja vya Mwembetogwa, Iringa jana.
“Juzi Agosti 27, 1:00 usiku tulipata barua kutoka Jeshi la Polisi Iringa iliyokubali Chadema kufanya maandamano wakiwa ndani ya magari na si matembezi ya miguu, lakini baadaye saa 3:00 usiku, tulipigiwa simu na OCD wa Iringa akitujulisha kuwa maandamano yao yamebatilishwa na kutengua mambo yote tuliyoafikiana mwanzo,” alisema Dk Slaa na kuongeza:
“Asubuhi ya leo (jana) tulipigiwa simu na RPC (wa Iringa) na kudai kuwa wanataka kuonana na viongozi wa Chadema, huku wakiwa na hoja kuwa tuahirishe kufanya mkutano kutokana na Sensa.
Hoja nyingine ambayo mimi naona ni ya upuuzi ni ile ya kusema kwamba wananchi wa Iringa watakuwa wameathirika na kifo cha kijana aliyekufa Morogoro,” alisema Dk Slaa.
Alisema baada ya kutokubaliana na hoja hizo, alipigiwa simu na IGP Mwema akimwomba asitishe mkutano na maandamano ya mkoani Iringa kwa kuwa hiyo ni amri kwa vyama vyote vya siasa na si Chadema pekee.
“Nimeongea na IGP leo kwa dakika zaidi ya 40 akisema Dk Slaa sijawahi kukuomba hata siku moja, naomba nikuombe na usinikatalie kati ya siku nne hadi tano kuanzia sasa tumezuia vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara kutokana na kuwapo kwa Sensa naomba tuelewane,” alisema Dk Slaa akimnukuu IGP Mwema.
Vurugu za Morogoro
Juzi, chama hicho kikuu cha upinzani kilifanya maandamano mjini Morogoro na kuzua taharuki, baada ya kutokea vurugu wakati polisi walipoamua kuyasambaratisha na kusababisha mauaji ya mtu mmoja, Ally Zona (38) mkazi wa Kihonda
Akizungumzia kifo hicho, Dk Slaa alisema chama chake kitashiriki kikamilifu katika mazishi ya kijana huyo kulingana na ratiba ya ndugu wa marehemu.
“Endapo familia itaamua kusoma dua hapa Morogoro na kuzika hapa, tutashiriki kikamilifu. Tumejadiliana na wanafamilia kuna mambo ya msingi tumekubaliana na walichoomba ni kusaidia kusafirisha mwili. Hatutajali itikadi aliyokuwa nayo marehemu,” alisema.
Chanzo: http://www.mwananchi.co.tz/habari
Monday, August 27, 2012
Wanasheria CHADEMA wampa Nape Nnauye siku 7 aombe radhi la sivyo atafikishwa Mahakama Kuu
Izingatiwe kuwa matamshi yake yalitangazwa na vyombo vya habari vya kielekroniki ikiwemo vituo vya televisheni, radio na kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii tarehe 12 Agosti 2012 na katika kurasa za mbele za magazeti mbalimbali tarehe 13 Agosti 2012.
Bodi ya Wadhamini wa CHADEMA iliagiza wanasheria wamwandikie barua ya kumtaka kukiomba radhi Chama Cha Demokrasia na Maendeleo kwa kutumia njia ile ile aliyotumia kufanya propaganda chafu za kuikashifu na kuifitisha CHADEMA kwa umma wa watanzania ikiwemo kuzusha kuwa upo uwezekano wa CHADEMA kupewa fedha hizo kwa mikataba yenye masharti ya kuiweka nchi rehani.
Tayari ameshaandikiwa barua ya kisheria tarehe 24 Agosti 2012 ya kumtaka aombe radhi na kulipa fidia ya bilioni tatu kwa matamshi hayo ya uzushi na uongo yenye maana ya kuwapotosha waliyoyasikia na kuyasoma kuwa CHADEMA kinawalaghai wananchi, kina viongozi wasio waaminifu na kwamba kiko tayari kuuza nchi wa uroho wa madaraka.
Kipaumbele cha CHADEMA katika suala hili ni kuombwa radhi hata hivyo kiwango cha fidia ya fedha kwa fedheha kilichotakiwa ni fundisho kuwa uzushi na uongo unagharimu.
Ikumbukwe kwamba tarehe 12 Agosti 2012 nilitoa kauli ya awali baada ya mkutano Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM na waandishi wa habari ambapo pamoja na mambo mengine nilieleza kwamba tutatoa tamko la kueleza hatua za ziada baada ya kupata taarifa kamili aliyoitoa.
Katika kauli hiyo nilitoa mwito kwa Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete kueleza watanzania iwapo propaganda hizo chafu zina baraka zake; hivyo ukimya wake mpaka sasa kuhusu matamshi hayo inakifanya CHADEMA kuwa na imani yenye shaka (benefit of doubt) kwamba Nape hakutumwa na chama chake kutoa matamshi aliyoyatoa.
CHADEMA inachukua fursa hii kuutaarifu umma kwamba asipotekeleza matakwa hayo ndani ya siku saba kuanzia tarehe hiyo aliyopokea barua hatua nyingine ya kumfikisha Mahakama Kuu zitaanzishwa ili aweze kuchukuliwa hatua zaidi.
Pamoja na kuchukua hatua za kisheria, CHADEMA kinaendelea kutimiza dhima yake ya kuleta uongozi bora, sera sahihi, mikakati makini na oganizesheni thabiti kwa maendeleo endelevu ya Tanzania kwa pamoja na mikakati mingine kutekeleza operesheni ya vuguvugu la mabadiliko nchini (M4C) na tunawashukuru wananchi kwa kuendelea kuunganisha nguvu ya umma kwa hali na mali katika maeneo mbalimbali nchini.
Taarifa hii imetolewa tarehe 26 Agosti 2012 na:
John Mnyika (Mb)
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi
Sunday, August 26, 2012
Makada CCM Wamnyooshea Kidole Mkapa.
KITENDO cha Mahakama Kuu Kanda ya Tabora kutengua matokeo ya ubunge Jimbo la Igunga yaliyompa ushindi Dk Dalaly Peter Kafumu (CCM), kimeibua mvutano mwingine ndani ya CCM, ambapo sasa baadhi ya makada wake wameanza kumnyooshea kidole Rais Mstaafu Benjamin Mkapa na baadhi ya mawaziri kuwa ndiyo chanzo cha kushindwa huko.
Baadhi ya makada maarufu na wenye uzoefu wa muda mrefu ndani ya chama hicho tawala, kwa nyakati tofauti kwenye mahojiano na Mwananchi Jumapili wamekiri kwamba, imefika mahali ambapo CCM inapaswa ijitazame na kuwa makini juu ya watu inaopaswa kuwatumia katika kampeni zake.
Katika tathmini yao, makada hao wamemtaja Rais Mstaafu Mkapa na mawaziri kadhaa, wakisema kuwa CCM haikuwa makini katika kuwateua wasimame kwenye majukwaa kupiga kampeni za kisiasa. Walitaja moja ya sababu kuwa ni Mkapa na baadhi ya mawaziri hao mashuhuri kuwa siyo wanasiasa wa jukwaani bali ni watendaji.
Licha ya CCM kujaribu kumtumia rais huyo mstaafu na mawaziri hao kutokana na heshima iliyojengeka kwao mbele ya Watanzania walio wengi, tathmini ya makada hao inaeleza kuwa hoja zao katika kampeni ama ziliwapa mwanya wapinzani, hasa Chadema kuiumbua CCM kwenye propaganda za majukwaani, hata kisheria.
Walikuwa wakizungumzia chaguzi ndogo zilizofanyika hivi karibuni katika Jimbo la Arumeru na ule wa Igunga Oktoba mwaka jana, ambao licha ya CCM kushinda, wiki hii mahakama kuu ilitengua ushindi huo. Kuanguka Igunga Dk Kafumu aliibuka mshindi kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika Oktoba 2, mwaka jana kuziba nafasi ya Rostam Aziz aliyejiuzulu kwa madai ya kuchoshwa na kile alichoita siasa za majitaka ndani ya CCM, lakini mahakama imetengua ushindi wake.
Uchaguzi huo ulikuwa wa ushindani mkubwa kati ya Dk Kafumu na aliyekuwa mgombea wa Chadema, Joseph Kashindye ambaye aliamua kupinga ushindi wa Dk Kafumu mahakamani akidai hakuridhishwa na mwenendo wa uchaguzi huo. Kashindye alifungua kesi hiyo Machi 26, mwaka huu. Wakati wa kampeni za uchaguzi huo vigogo mbalimbali wa CCM akiwamo Mkapa walipiga kambi Igunga na kushiriki mikutano mbalimbali ya kampeni, ambapo pamoja na mambo mengine walitoa kauli tata zilizosababisha CCM kushindwa katika kesi hiyo.
Mbali na Mkapa viongozi wengine waliotoa kauli hizo na sasa wananyooshewa vidole ni Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli, Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama na Mbunge wa Tabora, Ismail Aden Rage. Kauli tata ya Mkapa Wakili wa mlalamikaji, Profesa Abdallah Safari, Agosti 20 mwaka huu aliwasilisha mahakamani hapo zaidi ya malalamiko 13 dhidi ya Dk Kafumu na wenzake.
Mbali na kueleza yaliyozungumzwa na Dk Magufuli, Profesa Safari alidai hoja nyingine ni Baraza la Waislamu (Bakwata) Wilaya ya Igunga kuwakataza waumini wasiipigie kura Chadema na kwamba naye Rais Mstaafu Benjamin Mkapa alitoa ahadi ya kugawa mahindi kwa wananchi wa Igunga siku moja kabla ya uchaguzi ili waichague CCM. Makada waonya
Mbunge wa Kahama, James Lembeli alisema kuwa utaratibu wa sasa wa chama hicho kuwatumia viongozi wastaafu umepitwa na wakati kwa sababu Watanzania wa sasa hawahitaji kusikia maneno mengi, bali sera. Alisema kuwa CCM inatakiwa itazame ilipojikwaa na kuacha kutafuta mchawi kwa kuwa matatizo yaliyokifikisha chama hicho kilipo sasa yanajulikana.
“Kampeni za CCM hivi sasa hazina maandalizi, kila anayeweza kuzungumza anachukuliwa na kujumuishwa kwenye kampeni, jambo ambalo siyo sahihi,” alisema Lembeli na kuongeza: “Inatumia watu bila kuangalia kama wanakubalika, katika chaguzi zinazokuja, chama kiwatumie makada wanaopendwa na wananchi na wenye uwezo wa kuuza sera za chama.”
Alitaja sababu nyingine ya CCM kuanguka hasa Igunga kuwa ni pamoja na mgawanyiko uliokuwapo ndani ya chama hicho baada ya baadhi ya makada kuzuiwa kushiriki katika kampeni hizo wakati wana mvuto kwa wapiga kura. Akitolea mfano watu hao alisema kuwa ni pamoja na Mbunge wa Urambo Mashariki, Samuel Sitta, ambapo alibainisha kuwa waliotoswa katika kampeni hizo wasingeweza kuishiwa maneno ya kuzungumza na kuanza kutoa ahadi zinazovunja sheria ya uchaguzi.
Dk Kigwangallah Akizungumzia suala hilo, Mbunge wa Jimbo la Nzega, Dk Hamisi Kigwangallah alisema kitendo cha CCM kutumia vigogo akiwamo Rais mstaafu Mkapa katika uchaguzi wa Igunga, ndiyo chanzo cha kushindwa kwa kesi hiyo kwa kuwa walizungumza mambo yasiyo na msingi wowote.
Dk Kigwangallah ambaye Agosti 22 alichukua fomu za kuwania kiti cha Uenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa alisema kuwa uchaguzi mwingine ukifanyika katika jimbo hilo, viongozi na wabunge kutoka mikoa ya Tabora, Mwanza na Shinyanga ndiyo waachwe kufanya kampeni.
Chanzo http://www.mwananchi.co.tz/habari
Saturday, August 25, 2012
Mkutano Wa CUF Jangwani Jumapili Septemba 9, 2012.
CUF – Chama Cha Wananchi, kitafanya Mkutano mkubwa wa hadhara katika Viwanja vya Jangwani siku ya Jumapili tarehe 09/09/2012 kuanzia saa 6 mchana hadi 12 jioni.
Viongozi wote wa kitaifa watahudhuria.Nyote mnakaribishwa!
ASIBAKI MTU NYUMBANI
Ni “Mchakamchaka mpaka 2015”Hakiiiiii....!Sawa Kwa Wote!!!!
Friday, August 24, 2012
Oparesheni Sangara Kijijini Kododo Mvomero.
Katibu Mkuu wa BAVICHA Deogratias Munishi akimkabidhi kadi ya CHADEMA aliyekuwa mwenyekiti wa serikali ya kitongoji cha Kododo jimbo la Mvomero, bwana Charles Kiwaga. Wengine ni wanachama wapya wa CHADEMA tawi la Kododo Mvomero.
Operesheni Sangara inayoendelea kwa upande wa Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana la CHADEMA (BAVICHA), Bwana Deogratias Munishi amezidi naye kupasua vijiji ndani ya Mvomero, Morogoro. Pia wanavijiji walimuonyesha hali halisi ya maendeleo katika kata yao ya Luale kwa kipindi kirefu walichokuwa chini ya CCM tangu miaka 50 iliyopita mpaka sasa na wakiwa wamekata shauri kujiunga na CHADEMA kama chachu ya mabadiliko.
Tuesday, August 21, 2012
Mahakama Yatengua Ubunge Jimbo La Igunga
Mahakama Kuu Kanda ya Tabora imetoa hukumu ya kesi ya ubunge iliyokuwa ikimkabili mshindi wa ubunge jimbo la Igunga Dk Peter Kafumu (CCM).Hukumu hiyo ya kupinga matokeo yaliyompatia ushindi Dk Kafumu imetolewa leo ambapo imemuengua mbunge huyo katika nafasi yake ya ubunge
Shauri hilo lilifunguliwa na mlalamikaji Joseph Kashindye dhidi ya Dk Kafumu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na msimamizi wa uchaguzi.
Wednesday, August 15, 2012
Operesheni Sangara Ya CHADEMA Yavuna Wanachama Wapya Ulanga Mashariki,Kijiji Cha Nkonongo
Wapenzi na Washabiki wa Chadema wakijiandikisha na Kuchukua kadi mpya za uanachama Ulanga Mashariki, Kijiji cha NkonongoPicha Zote na CHADEMA
Katibu Mkuu wa BAVICHA taifa Bw Deo Munisi akiwa na Mkuu wa shule kijijini Nkonongo wakiangalia hali halisi ya ubora wa shule ilivyo.
Picha Zote na CHADEMA
Friday, August 3, 2012
Dk Mwakyembe Agoma Kujiuzulu...!
WAZIRI wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe amesema hawezi kujiuzulu kutokana na ajali ya Mv Skagit kwa sababu hahusiki na suala hilo.
Pia, amesema kitendo cha kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri wa Mawasiliano Zanzibar, Hamad Masoud kwasababu ya ajali hiyo kimechelewa kwa kuwa alitakiwa afanye hivyo tangu wakati wa ajali ya Mv Spice Islanders.
Wednesday, August 1, 2012
CHADEMA WATETEA KITI CHA NAIBU MEYA MUSOMA MJINI
Baadhi ya madiwani waliohudhuria
Uchaguzi wa Naibu Meya wafanyika na naibu Meya Bwire Nyamwero amepajipatia kura zipatazo 13 ambapo Diwani wa Chama cha Upinzani CCM, Ally Helce Jama akapata kura 4.
Akitangaza matokeo ya Uchaguzi Kaimu Mkurugenzi John Maselo alimtangaza Nyamwero kuwa Naibu Meya.
Awali Naibu Meya alikuwa, Mama Angela Gerick Lima ambaye kwa taratibu za CHADEMA aliteuliwa na kupata kura punguza katika Uchaguzi uliofanyika Wiki iliyopita Julai 28 katika kikao cha kamati Tendaji cha CHADEMA alipata kura 3 na Diwani mwingine pia kupata kura pungufu 9, ambapo Nyamwero alipita kwa kura 13.
Tamko La Chadema Kuhusu Kufungiwa Kwa Gazeti La Mwanahalisi.
TAMKO LA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)
KUHUSU KUFUNGIWA KWA MWANAHALISI
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinalaani uamuzi wa Serikali inayoongozwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kulifungia kwa muda usiojulikana gazeti la MwanaHalisi kwa kutumia mwanya wa sheria mbovu ya magazeti inayokwenda kinyume na haki za binadamu na utawala bora.
CHADEMA kinaitaka Serikali kulifungulia gazeti hilo haraka iwekanavyo na kimewasiliana na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na CHADEMA kuchukua hatua za kibunge kuisimamia Serikali kurekebisha udhaifu huo ikiwa inaheshimu uhuru wa habari na inazingatia maslahi ya taifa.
CHADEMA kinatafsiri hatua hiyo ya Serikali ya kufungia gazeti la MwanaHalisi kuwa ni sawa na kufungia uhuru wa kusambaza habari, uhuru wa kupokea habari na uhuru wa kutoa maoni, hivyo tunatoa mwito kwa wananchi na wadau wote wa habari kuungana pamoja kupinga hatua hiyo, na CHADEMA kitaeleza hatua za ziada za kuchukuliwa iwapo Serikali haitasikiliza kauli za wadau wa habari juu ya suala hili.
CHADEMA kinatambua kuwa uamuzi wa Serikali kufungia gazeti hilo kwa mara nyingine tena ni kwenda kinyume na haki za binadamu, kinyume na utawala bora na ni kikwazo kwa demokrasia na maendeleo nchini.
CHADEMA kinapinga hatua ya Serikali ambayo viongozi na watendaji wake wakiwa wametajwa kama watuhumiwa katika habari zilizoandikwa na gazeti hilo imetumia mamlaka haramu ya Waziri mwenye dhamana ya sekta ya habari kugeuka mlalamikaji, mwendesha mashtaka na mfungaji huku ikipuuza taasisi za kusimamia uwajibikaji na haki.
CHADEMA ilitarajia badala ya kulifungia gazeti la MwanaHalisi ingewezesha kufanyika kwa uchunguzi huru kufuatia habari za kiuchunguzi zilizoandikwa na gazeti hilo juu ya watendaji na watumishi wa Serikali kuhusishwa na jaribio la mauji ya Dr Ulimboka Steven, kupanga njama za mauji ya viongozi wa CHADEMA na matukio mengine ambayo yenyewe ndiyo yenye mwelekeo wa kufanya wananchi wapoteze imani na vyombo vya dola hali ambayo inaweza kuhatarisha amani na mshikamano uliopo nchini.
CHADEMA kinalinganisha uamuzi huo wa Serikali uliotangazwa tarehe 30 Julai 2012 na Msajili wa Magazeti chini ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuwa ni sawa kujichukulia sheria mikononi kwa kuwa Serikali yenye kuheshimu misingi ya asili ya haki ingezingatia kwamba ikiwa chombo chochote cha habari kimedaiwa kuvunja sheria ama kukiuka maadili dhidi ya Serikali, viongozi wake ama watu binafsi mashtaka au malalamiko yangepelekwa kwa taasisi zinazohusika mathalani Baraza la Habari (MCT) au mahakama.
CHADEMA kinafahamu kuwa Serikali imeamua kulifungia kutochapishwa kwa muda usiojulikana gazeti la MwanaHalisi, kwa mujibu wa Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976, kifungu Na. (25) (i); hata hivyo uamuzi huo ni kinyume cha misingi ya asili ya utawala wa sheria.
CHADEMA kinaelewa kwamba zipo sheria nyingine katika nchi yetu ambazo Serikali ingeweza kuzitumia kushughulikia madai iliyoyatoa kuwa Gazeti la Mwanahalisi limeandika habari na makala za uchochezi, uhasama na uzushi kupitia mahakama lakini imeamua kwa makusudi kuendelea kutumia sheria mbaya isiyokuwa na uhalali wa kihaki (illegitimate).
CHADEMA kinakumbusha kuwa kwamba Sheria hiyo ni kati ya Sheria zilizotajwa na Tume ya kukusanya maoni juu ya mfumo wa vyama vingi (Tume ya Nyalali) kuwa ni sheria mbaya miaka 20 iliyopita kuwa na Sheria mbaya na Serikali imekuwa ikikwepa kutunga sheria mpya pamoja na wadau wa habari kuandaa miswada ya sheria ya huduma za vyombo vya habari na uhuru wa taarifa kwa nyakati mbalimbali.
CHADEMA kinatoa mwito kwa wananchi na taasisi zote za kitaifa na kimataifa kufuatilia kwa karibu tukio hili la kufungiwa kwa gazeti la MwanaHalisi na matukio mengine ya hivi karibuni kuhusu asasi za kiraia, makundi mbalimbali katika jamii ikiwemo madaktari na vyama vya siasa hususan CHADEMA yenye kuashiria kwamba Serikali inayoongozwa na CCM imeanza mkakati wa kuficha ukweli na kudhibiti mabadiliko kwa kutumia sheria kandamizi, vyombo vya dola na njia nyingine haramu.
Hivyo, ieleweke kwamba hatua hii dhidi ya Gazeti la MwanaHalisi ni mwanzo tu wa hatua zingine zaidi dhidi ya magazeti mengine na taasisi nyingine hali ambayo inahitaji wananchi na wadau wote kuunganisha nguvu za pamoja katika kuchukua hatua za haraka kuinusuru nchi na mwelekeo huo.
Imetolewa tarehe 30 Julai 2012 na:
John Mnyika (Mb)
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi
Monday, July 30, 2012
CCM,Chadema Wawatangazia Kiama Wabunge Mafisadi

DK SLAA AONYA HAKUNA HURUMA, MSEKWA ASEMA RUSHWA ADUI WA HAKI, MBATIA ATOA WIKI MOJA SPIKA AWATAJE WOTE
Kizitto Noya, Dodoma na Leon Bahati, Dar
VYAMA vya CCM na Chadema vimetoa onyo kali kwa wabunge wanaotuhumiwa kwa kashfa ya kuhongwa na baadhi ya kampuni za mafuta na kulihujumu Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), vikisema havitasita kuwawajibisha pindi tuhuma hizo zitakapothibitika.
Kauli ya vyama hivyo imekuja siku moja baada ya wabunge watano, watatu wa CCM na wawili wa upinzani kudaiwa kuhusika na vitendo hivyo vya rushwa, ambavyo vimesababisha Spika wa Bunge, Anne Makinda kuivunja Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini na kuagiza uchunguzi wa kina ufanyike ili majina ya wahusika yawekwe hadharani.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, viongozi wa juu wa vyama hivyo walisema wanasubiri kwa hamu taarifa rasmi kutoka bungeni.
CCM: Rushwa adui wa haki
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Pius Msekwa alisema chama hicho kimewaapiza wanachama wake wote kutotoa wala kupokea rushwa.
Alisema rushwa ni kosa la jinai hivyo anaamini vyombo husika vya dola vitachukua hatua zinazofaa kwa mujibu wa sheria za nchi.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alikazia kauli hiyo akisema rushwa inaelezwa katika katiba ya chama hicho kwamba ni, ‘adui wa haki’ na wanachama wote waliapishwa kuwa hawatapokea wala kutoa rushwa.
Alisema yeyote anayekwenda kinyume na kanuni za CCM, anajiweka katika kundi la wasaliti wa chama.
Alisema wabunge ni kundi maalumu nchini ambalo linalipwa vizuri ili lisimamie vyema misingi ya maendeleo ya nchi pasipo tamaa wala vishawishi hivyo wanapotajwa miongoni mwa kundi la wala rushwa, CCM kinalaani vikali tukio hilo.
Kuhusu tuhuma hizo kutajwa kuwahusisha wabunge watatu wa chama hicho, Nape aligoma akisema habari hizo siyo rasmi, hivyo hawezi kuzizungumzia.
Hata hivyo, alisema CCM kinasubiri uchunguzi ufanyike ambao ndiyo utakaoweka bayana wahusika wa tuhuma... “Tusubiri uchunguzi ukamilike. Idadi inawezekana ikawa hiyo au ikapungua au kuongezeka.”
Dk Slaa: Hatufumbii macho ufisadi
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema: “Nalaani kitendo cha wabunge kuhusishwa na ufisadi hasa ikizingatiwa kwamba Chadema tumekuwa tukiupinga vikali. Tumekuwa tukipinga rushwa kwa sababu ndiyo inayoielekeza nchi pabaya… Chadema hatufumbii macho rushwa.”
Alisema tangu kuanza Bunge la 10, Chadema kimekuwa kikiona baadhi ya mambo yanayoendelea katika mhimili huo muhimu wa dola yamejaa walakini... “Ndiyo maana sisi Chadema tumekuwa tukisema Bunge limepoteza mwelekeo.”
Alisema akiwa mtendaji mkuu wa chama, anasubiri taarifa kamili kutoka katika kikao cha wabunge wa chama hicho ili kuweka wazi majina ya wahusika na kisha kufuatiwa na kikao cha Kamati Kuu (CC) ambacho kitakaa na kuchukua hatua kali.
“Tunahitaji tupate maelezo ya kina... chama chetu hakikurupuki… Nasubiri taarifa ya kokasi ya chama. Katiba ya Chadema inatambua uwapo wa kikao cha wabunge wetu na kwa bahati nzuri, kiongozi wake mkuu ni Mwenyekiti wa Chadema (Freeman Mbowe) na katibu (David) Silinde ni mbunge wetu. Tunasubiri taarifa yao.”
Alisema Chadema kina kanuni ya kudhibiti rushwa hivyo, mbunge wake akitajwa miongoni mwa wanaohusishwa na rushwa, atawajibishwa kupitia kikao cha CC ya chama hicho.
NCCR-Mageuzi yakoleza moto
Katika hatua nyingine, Chama cha NCCR- Mageuzi jana kilikoleza moto baada ya kumtaka Spika Anne Makinda awataje wabunge hao bungeni ili wafukuzwe na kufungwa kama Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge inavyotaka.
Chanzo: http://www.mwananchi.co.tz
Thursday, July 26, 2012
Mansour Yusuf Himidi; Hata Nikivuliwa Uwanachama Wa CCM, Sitabadili Mawazo Yangu Kuhusu Muungano
Monday, July 23, 2012
Mkutano wa CCM Kigoma
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala wa Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI,) Aggrey Mwanri akihutubia, kwenye mkutano wa CCM uliofanyika, jana , Julai 22, 2012, kwenye Uwanja wa Community Centre, Mwanga mjini Kigoma.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akihutubia, kwenye mkutano wa CCM uliofanyika, jana , Julai 22, 2012, kwenye Uwanja wa Community Centre, Mwanga mjini Kigoma. 
Waziri wa Nchi Ofsi ya Rais, Mahusiano, Steven Wasira akihutubia kwenye mkutano wa CCM uliofanyika, jana , Julai 22, 2012, kwenye Uwanja wa Community Centre, Mwanga mjini Kigoma.

Mamia ya wananchi waliofurika kwenye mkutano wa CCM katika Uwanja wa Community Centre, Mwanga mkoani Kigoma.

Wazee kwenye mkutano wa CCM, Uwanjwa wa Community Cetre Mwanga Kigoma

Viongozi mbalimbali wa CCM waliohudhuria katika mkutano huo.

Habibu Ally wa kikundi cha Ujiji cha Sebene akicharaza kinanda akiwa chali wakati wa mkutano huo

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akituzwa na Mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba alipocharaza gita, kwenye mkutano wa CCM, Uwanja wa Communiy Cetre, Mwanga Kigoma
Posted in:
Subscribe to:
Posts (Atom)