Wednesday, April 18, 2012

RATIBA YA RAIS DK SHEIN KISIWANI PEMBA KESHO



Na Marzuku Khamis Maelezo Pemba
 
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein kesho anatarajiwa kuendelea na ziara yake katika Mkoa wa Kusini Pemba baada ya kumaliza ziara katika Mkoa wa Kaskazini Pemba hapo leo kwa kutoa majumuisho ya Mkoa huo.
 
 
Kwa mujibu wa taarifa iliotolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kusini Permba Imeonesha kuwa Rais asubuhi atapokea taarifa ya utekelezaji ya Mkoa huo na baadae kuelekea Chambani Wilaya ya Mkoani kwenye Bonde la Maziwa Pacha ambapo atakaguwa Bonde hilo.
 
 
Aidha Mheshimiwa Rais atafunguwa Jengo la Skuli ya Ukutini na Kuzungumza na Wananchi pamoja na kuweka jiwe la msingi kituo cha Afya cha Michenzani na pia kuzungumza na Wanananchi.
 
 
Mchana Dkt Shein  atakaguwa kilimo cha Umwagiliaji Maji Makombeni na jioni atazungumza na wana CCM na Wanananchi wa Tawi la CCM Mwambe.
 
 
Ijumaa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa BAraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein atazungumza na Kikosi Kazi cha Taifa kuhusu uvunaji wa  zao la Karafuu  huko katika Kiwanda cha Makonyo chake chake Wawi Pemba na baadae kuelekea Ziwani ambapo atafunguwa Tangi la Maji Ziwani.
 
 
Jioni Dkt Shein ambae ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM ataweka Jiwe la Msingi Tawi la Vitongoji na Matungu Changamka kuzungumza na wana CCM na kutoa kadi kwa wanachama  wapya wa CCM.
 
 
Rais wa Zanzibar anatarajiwa kumaliza ziara yake ya siku sita Kisiwani Pemba Jumaamosi baada ya kutoa majumuisho ya ziara yake ya Mkoa wa Kusini Pemba na kurejea Unguja siku hiyo hiyo.

No comments: