Sunday, June 17, 2012

MATILDA MARTIN ATWAA TAJI LA MISS DAR CITY CENTRE 2012

Miss Dar City Centre 2012, Matilda Martin, akiwa katika pozi muda mfupi baada ya kuibuka kidedea.
Miss Dar City Centre aliyepita Alexa William (kushoto), akimkabidhi taji hilo Matilda muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi.
Matilda (katikati), akiwa katika pozi na mshindi wa pili na tatu mara baada ya kutangazwa.
Warembo waliobahatika kuingia tano bora wakiwa katika pozi.
Mmoja wa majaji,Wema Sepetu akiwasomea maswali washindi waliofauru kuingia tano bora.
Majaji wa shindano hilo wakiwa katika meza yao.
Mkurugenzi wa Miss Tanzania Hasheem Ludenga, akiwakaribisha wageni kabla ya mchakato huo kuanza.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sophia Mjema, akifungua mashindano hayo kwa niaba ya mgeni rasmi.
Mshereheshaji wa shindano hilo Hamisi Mandi ‘B12’, akiwajibika jukwaani hapo.
Miss Tanzania 2011, Salha Israel akifuatilia mshindano hayo.
Rapa wa Bendi Twanga Pepeta, Msafiri Diouf akipiga misumali kwa mashabiki wake.
Luiza Mbutu na Dogo Rama wakiwajibika kwenye shindano hilo.
Msanii kutoka THT, Rachel akitumbuiza na msanii mwenzake Sharomilionea jukwaani hapo.
Diamond akipagawisha jukwaani hapo.
Diamond akiwa amezungukwa na mashabiki zake.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Estelina Sanga ‘Linah’, akishuhudia mashindano hayo.
Washiriki wa shindano hilo wakiwa katika pozi la pamoja.
Beny Kinyaiya akiagana na marafiki zake muda wa kuondoka ukumbini hapo.
Baadhi ya mashabiki wakifurahia burudani zilizokuwa zikitolewa ukumbini hapo.
Mashabiki wakifutilia burudani.
USIKU wa kuamkia leo kulifanyika mchuano wa kumsaka Miss Dar City Centre 2012, ndani ya Ukumbi wa Golden Tulip Masaka jijini Dar es Salaam, ambapo Matilda Martin aliibuka kidendea, akifuatiwa na Magdalena Ryamond ambaye alitwaa nafasi ya pili huku nafasi ya tatu ikienda kwa Witness Michael, Viola Mwamba, akisimamia namba nne na pazia likafungwa na aliyeshika namba tano ambaye ni Leila Heri.
Shindano hilo lilipambwa na burudani kutoka kwa Naseeb Abdul ‘Diamond’, Rachel na Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta International,’
Huku Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sophia Mjema akimwakilisha mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, ambaye ilikuwa awe mgeni rasmi wa shindano hilo.
Habari/Picha: Musa Mateja/GPL

No comments: