Showing posts with label jami. Show all posts
Showing posts with label jami. Show all posts

Thursday, July 19, 2012

MWANAFUNZI WA CHUO CHA IFM AFARIKI KIFO CHA KUTATANISHA: AOKOTWA MAENEO YA KOKO BEACH AKIWA HAJITAMBUI.

 Marehemu Agnes B. King'unza wakati wa uhai wake.Agnes alikuwa ni mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) akiwa mwaka wa kwanza akichukua Shahada ya Kodi (Bachelor of Taxation).
 Mwili wa Marehemu Agnes ukiwa kanisani tayari kwa heshima ya mwisho katika kanisa la Romani katoliki Mbezi Temboni.
 Mwili wa marehemu Agnes ukiwa kwenye jeneza ulipokuwa ukiwasili nyumbani kwao Mbezi kwa Msuguri.
 Aliyevaa Koti jeusi ndio baba mzazi wa Agnes Bwana Bernard King'unza.
 Mama Mzazi wa Agnes akilia kwa uchungu baada ya kuona mwili wa Mwanae.
 Makamu Rais wa Serikali ya wanafunzi wa IFM akitoa salamu za rambi rambi kwa niaba ya wanafunzi wenzake.
 Baba Padre wa Parokia ya Mbezi Temboni akibariki mwili wa Agnes King'unza.
 Hawa ni baadhi ya wanafunzi wenzake aliokuwa akisoma nao katika chuo cha usimamizi wa fedha IFM na kushoto mwenye shati la mistari ni mwakilishi kutoka wafanyakazi wa IFM.
--
Agnes aliokotwa na msamaria mmoja ambaye kwa taarifa za awali zinasema alikuwa ni mlinzi wa nyumba moja maeneo ya Koko Beach ambako ndio alikutwa ametupwa na watu wasiofahamika na kupelekwa kituo cha Polisi cha Oysterbay na baadae kukimbizwa hospitali ya Agha khan.

Marehemu Agnes B. King'unza alifariki Jioni ya tarehe 16/07/2012 katika Hospitali ya Muhimbili ambako alipelekwa baada ya Madaktari wa Hospitali ya Agha khan kushindwa kumtibu na kumrufaa Muhimbili kwa matibabu zaidi.

Mwili wa Marehemu Agnes King'unza umesafirishwa jana Jioni kwenda Nyumbani kwao Kalenga - Iringa kwa mazishi ambayo yatafanyika leo tarehe 19/07/2012.

BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.

Saturday, July 14, 2012

Mwandishi Wa Blogi Atupwa Jela Miaka 18 Nchini Ethiopia

Mwanahabari maarufu ambaye pia ni mwandishi wa Blogi amefungwa jela miaka 18 nchini Ethiopia kwa madai ya kukiuka sheria ya ugaidi. Eskinder Nega na wenzake 23 walipatikana na hatia mwezi uliopita.
Walikamatwa kwa madai ya kuwa na uhusiano na kundi moja la upinzani lililo na makao yake Marekani kwa jina Ginbot Seven. Serikali ya Ethiopia inadai kuwa kundi hilo ni la kigaidi.
Mahakama hiyo ya Addis Ababa pia ilimfunga jela maisha mwanaharakati wa upinzani,Andualem Arage.
Kutokana na kazi yake ya uwana-habari na kuandika Blogi, Mwezi wa May, Eskinder alipewa tuzo maarufu la kimarekani la Pen America's Freedom to Write.
Makundi ya kutetea haki za kibinadamu zimekuwa ikiilaumu serikali kwa kubuni sheria hiyo ya kukabiliana na ugaidi yakisema sheria hiyo haifai.
Siku ya Ijumaa Mwanahabari ,Eskinder na mwanachama wa chama cha upinzani cha Unity for Democracy and Justice party walikuwa mahakamani kuhukumiwa.Washukiwa wengine 16 waliopatikana na hatia mwezi wa Juni wako ukimbizini.
Walipokuwa wakiingia mahakamani wawili hao waliwapungia mikono jamaa zao na marafiki pamoja na maafisa wa kibalozi waliokuwemo ndani.
Eskinder alikamatwa mwezi wa Septemba mwaka jana baada ya kuandika makala iliyokuwa ikiilaumu serikali ya Ethiopia kwa kukamata wapinzani wake kwa kutumia sheria ya ugaidi.
Miongoni mwa watu ambao wamekamatwa chini ya sheria hiyo ni msanii na mcheza filamu maarufu nchini Ethiopia, Debebe Eshetu ambaye ni mkosoaji mkuu wa serikali.

Friday, July 13, 2012

Madaktari Waandaa Maandamano

 Mwakilishi wa Madaktari wa Mafunzo kwa Vitendo Dk Frank Kagoro akifafanua jambo kwa waandishi   wa habari jijini Dar es Salaam jana

KITENDO cha Baraza la Madaktari Tanganyika (MCT), kusitisha usajili kwa baadhi ya madaktari waliokuwa kwenye mafunzo ya vitendo (Interns), kimekoleza moto wa mgomo wa madaktari baada ya wanataaluma hao kutangaza maandamano yatakayofanyika wakati wowote kuanzia sasa.

Kwa muda wa wiki tatu sasa, madaktari wamekuwa katika mgomo wakitaka kuboreshewa masilahi yao na huduma za afya hospitalini, lakini wanataaluma hao walionekana kuchukizwa zaidi baada ya tukio la kutekwa, kupigwa na kutelekezwa porini kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk Steven Ulimboka huku rais wa Chama cha Madaktari (MAT), Dk Namala Mkopi akifunguliwa mashtaka ya kukiuka amri ya mahakama.

Jana, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa MAT, Dk Rodrick Kabangila alitaja lengo la maandamano hayo kuwa ni kupinga dhuluma na uonevu dhidi ya taaluma ya udaktari na madaktari wenyewe.

Dk Kabangila alitaja sababu ya pili kwamba, ni kulaani kitendo alichofanyiwa Dk Ulimboka cha kutekwa, kupigwa, kuteswa na kutupwa katika msitu wa Pande nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na sababu ya tatu ni kushinikiza Serikali kuunda Tume Huru ya kuchunguza suala hilo, ili wahusika wajulikane na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Alisema pia kwamba hatua hiyo imekuja kutokana na kitendo cha Serikali kuendelea kuchukua hatua ya kuwafukuza madaktari na kusitishiwa leseni wale waliokuwa chini ya mafunzo, badala ya kusikiliza na kutatua madai yao yaliyolenga kuboresha huduma hiyo nchini.

“Kama mnavyofahamu, mpaka sasa takriban madaktari 400 walio chini ya usimamizi na wale walio kazini wamesitishiwa usajili na wengine kusimamishwa kazi, na haya yanaendelea wakati suala la msingi likiwa mahakamani na pia Tanzania ikiwa na upungufu mkubwa wa madaktari kwa daktari mmoja kuwa na uwiano wa kuhudumia wagonjwa 30,000,” alisema Dk Kabangila na kuongeza:

“MAT inasikitishwa na dhuluma hii inayoendelea dhidi ya taaluma ya udaktari na madaktari wenyewe na hivyo inapanga kuitisha mkutano mkubwa kesho (leo) na inatangaza maandamano ya amani ya madaktari na wale wote wenye mapenzi mema na taaluma hii na sekta ya afya kwa ujumla.”

Dk Kabangila aliongeza kuwa, maandamano hayo yatafuata taratibu zote za kisheria, ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa polisi saa 48 kabla ya kuandamana na madaktari wote watavaa makoti meupe na wasio madaktari watatakiwa kuwa na vitambaa vyeupe.

Alisema maandamano hayo ya amani yataanzia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) hadi Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, ambako watakabidhi madai yao serikalini.

Thursday, July 12, 2012

Kikwete Atoa Msaada Wa Baiskeli Kwa Wagani Wa Njombe Na Iringa

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Christine Ishengoma (kulia) akimkabidhi baiskeli Mgani nje ya ofisi yake



Baiskeli hizo zimekabidhwa kwa wagani hao na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Christine Ishengoma kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete. Chanzo: www.frankleonard.blogspot.com
Reactions::

Ndoa Ya Dkt Slaa Kortini