Mark Hughes yupo njiani kupokea kiasi cha £1millioni kama bonasi ikiwa ataiwezesha QPR kubaki katika Barclays Premier league Jumapili na matokeo ambayo ambayo yanawza kutibua sharehe za Manchester City kunyakua kombe lao kwanza la ligi baada ya miaka 43.
Wasaidizi wa Hughes, Mark Bowen na Eddie Niedwiecki, pia watapata mkwanja mrefu ikiwa Rangers watabaki EPL. Timu hiyo ya London Magharibi inahitaji japo pointi moja tu pale Etihad Stadium kuepuka kushuka darJ. Ingawa Roberto Mancini na vijana wake wanahitaji ushindi ili kujihakikishia ubingwa wa ligi wa kwanza tangu 1968, huku mahasimu wao Manchester United wakiwa wanahitaji ushindi na kuiombea mabaya City ili kuweza kubeba ubingwa wa 20.
City walimtimua Hughes mwaka 2009 na kumpa ulaji Roberto Mancini - jambo ambalo mwalimu wa United Sir Alex Ferguson akikielezea kitendo hicho ni kwamba hakikuwa sahihi.
Mark Hughes akifanya vitu vyake akiwaonyesha Manchester City kuwa nahitaji pointi 3 kesho
Mark Hughes akishangilia siku chache za nyuma baada ya kushinda, kesho anataka kufunga msimu na mtu
Angalia hiki kibonzo hapa juu kikimwonesha Mark alipotimuliwa Man City mwaka 2009, mwisho kabisa kulia ni Mancini sijuhi alikuwa anasemaje kichini chini!!! yote tutayajua kesho kuanzia jioni saa 12....
No comments:
Post a Comment