Thursday, July 5, 2012

TUME YA UTUMISHI WA UMMA YANG’ARA KATIKA UTOAJI WA HUDUMA BORA KWA UMMA WA WATANZANIA

Tume ya Utumishi wa Umma imepata tuzo ya kombe baada ya kuwa MSHINDI WA PILI kati ya Taasisi 34 zilizoshindanishwa katika eneo la utoaji wa huduma bora kwa Umma Tanzania. Tuzo hiyo ilitolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Hawa Ghasia katika kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo yalifanyika Jijini Mwanza kuanzia tarehe 16 – 23/6/2010.
Imeibuka mshindi wa pili katika utoaji wa huduma kwa Umma Tanzania kutokana na usimamizi mzuri unaofanywa na Tume ya Utumishi wa Umma.
Miongoni mwa huduma ambazo zinatolewa na Tume ya Utumishi wa Umma ni pamoja na kuwezesha Mamlaka za Ajira na Nidhamu kuzingatia Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002, Kanuni na taratibu zake kwa kuandaa na kusambaza miongozo ya Ajira, Nidhamu na Rufaa kwa Mamlaka hizo. Miongozo ambayo tayari imesambazwa na Tume ya Utumishi wa Umma ni Mwongozo wa Ajira katika Utumishi wa Umma, Toleo Na. 1, 2005 na Toleo Na.2,  2009, Mwongozo wa Mashauri ya Nidhamu na Rufaa, Toleo Na. 1, 2005 na Toleo Na. 2, 2009.
Aidha Miongozo mingine ni pamoja na Maelekezo Mahususi kwa Mamlaka ya Nidhamu na Kamati za Uchunguzi kuhusu namna ya kuendesha uchunguzi wa Mashauri ya nidhamu Na. 1 ya mwaka 2008 na Nyaraka mbalimbali za ajira zilizotolewa na Tume ya Utumishi wa Umma.
Miongozo hiyo imeongeza uelewa wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002, Kanuni na taratibu zake kwa Mamlaka za ajira na nidhamu na hivyo kuchangia kupanda kwa uzingatiaji wa sheria, kanuni na taratibu zinazohusu rasilimali watu katika Utumishi wa Umma. Maeneo ambayo uzingatiaji wa sheria, kanuni na taratibu umepanda ni pamoja na ajira, nidhamu na rufaa.
Tume ya Utumishi wa Umma imewahi kuwa mshindi wa tano wa Taasisi zinazosimamiwa vizuri kati ya Taasisi 184 zilizoshiriki maonyesho ya Kimataifa ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo yalifanyika kuanzia tarehe 15 – 23/6/2009. Aidha Tume ya Utumishi wa Umma imewahi pia kuwa mshindi wa pili kati ya Taasisi 153 zilizoshiriki katika maonyesho ya Nane Nane yaliyofanyika Mkoani Dodoma kuanzia tarehe 1 - 8/8/2009 kutokana na utoaji wa huduma bora kwa Umma Tanzania.
Taasisi 157 zimeshiriki katika maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambapo Taasisi 34 kati ya 157 zilishindania Tuzo ya Taasisi zinazosimamiwa vizuri katika utekelezaji wa majukumu ya serikali

No comments: