Njia
panda kuelekea Kalambo Falls. Maporomoko hayo yanayopatikana Mkoani
Rukwa katika Wilaya ya Kalambo ni pili kwa ukubwa barani afrika yakiwa
na urefu wa mita 235. Maporomoko hayo yapo mpakani na nchi jirani ya
Zambia.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akitoa baadhi ya maelekezo
kwa wataalam hao wa majenzi kutoka MUST na wale wa ardhi kutoka
Halamashauri ya Wilaya ya Kalambo juu ya mpango wa majenzi wa eneo hilo
la kitalii hivi karibuni. Mpango huo ni pamoja na kujenga geti la
kukusanyia ushuru, eneo la mahoteli, na huduma nyingine muhimu.
Wataalamu
wa majenzi kutoka chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST),
Kutoka kushoto Omary Mwenunge na Mark Nassary wakiwa kazini kupata
taswiraya maeneo hayo na kuyafanyia kazi ikiwa ni kuweka michoro ya
huduma mbalimbali zitakazokuwa zinapatikana katika eneo hilo la kitalii
Mkoani Rukwa.
Wataalam
hao wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi
Stella Manyanya hivi karibuni walipotembelea eneo hilo. Nyuma yao ni
Maporomoko ya Mto Kalambo yenye urefu wa mita 235.
Wataalam hao kutoka MUST wakistaajabu maporomoko ya mto Kalambo.
Sehemu ya maangukio ya mto kalambo
Sehemu ya mapitio ya mto kalambo baada ya kupita kwenye maporomoko.
Picha
ya maporomoko hayo ikionekana kwa urefu yakiwa na mita 235 (kutoka juu
hadi chini).(Picha na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa
"rukwareview.blogspot.com")
No comments:
Post a Comment