Gari ikiwa na Mwili wa marehemu Bi. Kidude ukiusafirisha kutoka katika
Kijiji cha Kihinani kuupeleka nyumbani kwake Rahaleo kwa matayarisho ya
mazishi kesho mchana na kuzikwa Kitumba. Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini
Unguja.(Picha zote kwa hisani ya Othman Maulid
wa ZanZinews)
Mwili wa marehemu ukishushwa katika gari wakat ukiwasili nyumbani kwake
Rahaleo kwa taratibu za mazishi kesho mchana na kuzikwa Kitumba.
Ndugu na Jamaa wakiubeba mwili wa marehemu Bi.Kidude wakati ulipowasili nyumbani kwake Rahaleo kwa ajili ya mazishi kesho.
Mrajisi wa Baraza la Sanaa Zanzibar Khadija Batashi akizungumza na Waandishi jinsi alivyoupokea msiba wa Bi. Kidude
Matayarishi ya mazishi ya Bi. Kidude yakitayarishwa katika Nyumba yake Rahaleo.
Mjuukuu wa Bi Kidude Omar Ameir akiwasiliana na jamaa kuwajulisha msiba
wa Marehemu Bi. Kidude, baada ya kuwasili katika nyumba yake kwa
matayarisho ya mazishi kesho mchana saa saba baada ya sala ya adhuhuri
na kuzikwa Kitumba.
Bi.Maryam Hamdani akilakiwa na Bi Sihaba baada ya kuwasili katika makazi ya bikidude rahaleo , akiwa na majonzi.
Waandishi wa habari wakizungumza na Mfadhili Mkubwa wa Bi Kidude Maryam
Hamdan,kuhusiana na marehemu ambaye yeye alikuwa ni mtayarishaji na
mratibu wa safari za Bi Kidude nje ya Nchi katika matamasha mbalimbali
aliyokuwa akihudhuria nje ya nchi katika uhai wake.
Meneja wa Sauti ya BUSARA Zanzibar Stella Steven, akizungumza na
waandishi wa habari kuhusiana na marehemu Bi Kidude ambaye alikuwa
akidhaminiwa na BUSARA katika matamasha mbalimbaliyaliokuwa yakiandaliwa
na Busara.jinsi walivyopokea kifo chake kwa masikitiko makubwa na
kuacha pengo katika tasnia ya muziki wa taarab asilia Zanzibar.
No comments:
Post a Comment