Sunday, July 1, 2012

UCHAFU KUFUTIKA TANZANIA NI KAMA NDOTO!!!!!!!!!!!!!!!!



Dar es Salaam inafahamika kwa kuwa mji mkubwa Tanzania kwanini usiwe mfano wa kuwa unatunza mazingira.??? MULTINET imeshindwa kwa nini tusiikubali Green Waste Pro Ltd kufanya usafi wa jiji letu na miji mingine hapa nchini.
Tuipende nchi yetu na tuwe wa kweli kwenye nafsi zetu, usafi unaanza kwa nini.? Kwa mtu mmoja nyumbani kwake tunakuanzishia ubora nyumba kwa nyumba tukaribishe. Pichani ni barabara ya Jamhuri karibu na kituo cha mafuta BP kama kamera yetu ilivyokuta lundo la uchafu usiku huu.

Green is Good.!(G G).
Huu ni Mtaa wa Libya.
Barabara ya Morogoro karibu na Makao Makuu ya Ofisi za Mohammed Enterprises Ltd pako hivi.
Barabara ya Shabaan Robert karibu na Umoja House.
Barabara ya India nyuma ya TTCL House.
Kama ilivyo ada kila kukicha viongozi wa nchi yetu wanasema na kufanya kwa mda juu ya usafi wa miji na vijiji kwa ujumla lakini inakuwaje hakuna mabadiliko juu ya kitu wanachokuwa wanakizungumzia mpaka leo.
Nini kifanyike kama Dar es salaam ndipo walipo vingozi wa ngazi za juu lakini hali ya uchafu nika mashimo ya uchafu kila sehemu kuna kila sababu ya kusema kuwa tubadilike ili kutunza mazingira yetu kwa afya za vizazi vyetu na sisi wenyewe kwa ujumla. 
Napenda niwataarifu kuwa tuache kuwaachia viongozi tu wafanye na kuimiza juu ya usafi wa nchi yetu ni jukumu la kwetu sote tushirikiane kutokomeza uchafu.
Eliud 
0768078360

No comments: