Katibu Mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue (Kulia) akimsikiliza  mwenyekiti wa kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe. John Cheyo  (katikati) wakati alipofanya ziara ya kikazi Bungeni Dodoma. Kushoto ni  Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Zainabu Vulu. Balozi Sefua  alifanya ziara ya kikazi Bungeni kwa lengo la kujitambulisha  
 
 Katibu Mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue (Kulia) akimsikiliza makamu  mwenyekiti wa kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma  (POAC) Mhe. Deo  Filikunjombe wakati alipofanya ziara ya kikazi Bungeni Dodoma. Katikati   ni Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Zitto Kabwe. Balozi Sefua alifanya  ziara ya kikazi  Bungeni kwa lengo la kujitambulisha 
   . Katibu Mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue (Kulia) akizungumza na  mwenyekiti wa kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) Mhe. Agustino  Mrema wakati alipofanya ziara ya kikazi Bungeni Dodoma. Kushoto  ni  Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Idd Azzan. Balozi Sefua alifanya  ziara ya kikazi Bungeni kwa lengo la kujitambulisha 
  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akisaini kitabu cha wageni  katika ofisi ya  katibu wa Bunge Bungeni Dodoma. Balozi Sefua alifanya ziara ya kikazi  Bungeni kwa lengo la kujitambulisha kwa viongozi mbalimbali wa Bunge.
    Katibu wa Bunge  Dkt. Thomas Kashililah akiwa katika mazungumzo na  katibu Mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue, wakati Balozi Sefue  alipofanya ziara ya kikazi Bungeni Dodoma. Kushoto ni Msaidizi wa Katibu  wa Bunge Nd. Emmanuel Mpanda, pamoja na Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge  Ndg. John Joel.
  Katibu wa Bunge  Dkt. Thomas Kashililah akimkabidhi Katibu Mkuu  Kiongozi Balozi Ombeni Sefue vitabu vya orodha ya Wabunge pamoja na  kanuni za kudumu za Bunge wakati alipofanya ziara ya kikazi Bungeni  Dodoma.


 
 
No comments:
Post a Comment