Wanawake watatu wakazi wa Kijiji cha Kashishi, Kata ya Nzanzui Tarafa
ya Kinang'weli, Wilayani Itilima Mkoani Simiyu watalazimika kukihama Kijiji
chao baada ya wananchi wenzao kijijini hapo kuwatuhumu kwa Imani za
Kishirikina.
Akizungumza na Blog hii, Katibu Tarafa wa Kinang'weli, Sheila Kikula,
amesema wananchi hao hivi sasa wapo chini ya uangalizi wa Polisi na bado
maamuzi hajafikiwa rasmi kuwa ni wapi wahamie na Polisi wamewapeleka kuchukua
vyombo vyao.
Taarifa zilizotolewa zinasema kuwa chanzo cha akina mama hao
kushambuliwa kwa mijel;edi na wananchi kasha kuwatishia kuwapotezea uhai ni
kuugua kwa kijana mmoja kijijini hapo aliyedai kulogwa na akina mama hao.
Mara baada ya taarifa hizo kusambaa siku ya Juma pili ndipo wakavamiwa
na kushambuliwa lakini kijana huyo alipelekwa Hospityali ambako amelazwa hadi
hivi sasa akisumbuliwa na ugonjwa wa Malaria.
Kikula amesema akina mama aho ambao ni vikongwe wameshambuliwa vibaya
kwa fimbo na wananchi wenzao jambo ambalo limepelekea kuvimba mwili na kuwa na
majeraha ya hapa na pale.
Aidha Katibu Tarafa huyo amesema wananchi hawana budi kuacha vitendo
vya kikatili na kujichulia sheria Mkononi dhidi ya watuhumiwa wowote bali watoe
taarifa Polisi na kushughulikiwa kisheria.
Pia ametoa wito kwa Viongozi wa Dini mbalimbali nchini kufika eneo hilo
na kutoa huduma za kiroho kwani Wimbi la imani hizo za kishirikina ambalo
kiserikali haliaminiki ni kukosekana kwa huduma za kiroho miongoni mwa Jamii.
“Ipo haja kwa viongozi wa dini na madhehebu kufika hapa na kuanzisha
makanisa na Misikiti ili watu wawe na hofu ya Mungu na kuacha imani ambazo
hazimpendezi Mungu”, alisema Kikula.
Na Father
Kidevu Blog, Itilima-Simiyu
No comments:
Post a Comment