Taarifa za hivi punde kutoka Bungeni Mjini Dodoma,zinaeleza kuwa Kusudio la Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini,Mh. Zitto Kabwe la kutaka kupiga kura za kuanzishwa kwa mjadala wa kutokuwa na imani na Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda,limepigwa chini na Spika wa Bunge,Mh. Anne Makinda.
Akisoma kanuni za Bunge,Mh. Spika alisema kwa mujibu wa kanuni za Bunge na Katiba ya Nchi,kusudio la kutaka kumuondoa Madarakani Waziri Mkuu kwa kupiga kura ya kutokuwa na Imani nae ambayo ni taarifa ya maandishi inapaswa kuwasilishwa kwake siku 14 kabla ya siku husika.
Hivyo kwakuwa ofisi yake haijapata taarifa ya maandishi ju ya zoezi hilo,basi zoezi hilo moja kwa moja litakuwa ni batili, na kwasababu kikao hicho cha Bunge kinatarajiwa kufungwa siku ya jumatatu,basi hakutakuwa na uwezekano wa zoezi hilo kukamilika.
Awali Mbunge wa Jimbo la Bumbuli,Mh. January Makamab aliomba muongozo wa Spika kuhusu jambo hilo ndipo Spika,Mh. Anne Makinda akasimama na kutoa ufafanuzi huo
No comments:
Post a Comment