HAKUNA MCHUNGAJI WA KUJIITA MTUME: MCHUNGAJI SALOME MULAMBA
NA MWANDISHI WETU
MCHUNGAJI wa Kanisa la ‘Gospel Ministry Church’ (GMC), Salome Mulamba Ulimwengu amesema hakuna Mchungaji mwenye uhakika wa kujiita Mtume bali mwenye uwezo wakujua hayo ni mungu pekee.
Kauli hiyo ilitolewa na Mchungaji huyo wakati alipokuwa akizungumza jana, na Fullshangweblog.com kuhusu tabia iliyozuka kwa baadhi ya watu kujipa vyeo hivyo vya utume ambapo ni kinyume na vitabu vya dini hiyo.
Mchungaji Salome alitanabaisha kuwa hata vitabu vya dini hiyo vinasema hakuna mtu mwenye uwezo wa kujiita mtume kwani kwa kujifananisha hivyo ni makosa yanayofanywa na baadhi ya watu ambao roho zao zimetawaliwa na taama za kidunia.
Alisema utume wa kweli hudhihirika kwa mhusika kutokana na matendo yake yatokanayo na roho mtakatifu inapomwiingia kikamilifu huku akiachana na mabo yote machafu ya duniani.
Mchungaji huyo alisema watu wanaojipa cheo hicho wamekuwa wakificha kitu huku wakijua fika kuwa lengo lao ni kutaka kujipatia mali na utajili ambao hauendani na utukufu wanaojitangazia mbele ya waumini.
Aidha, Mchungaji huyo alitoa wito kwa kuiomba jamii kujisogeza karibu na nyumba za ibada ikiwa ni moja ya njia kuu zitakazoidia katika kuepukana na mporomoko wa maadiri ambao unaonekana kushika kasi katika kila kona.
No comments:
Post a Comment