Saturday, May 19, 2012

JE UNAWEZA AMIN HILI


WAHADZABE WATAKA NYAMA YA NYANI NA NGIRI ILI KUTEKELEZA ZOEZI LA SENSA MWAKA HUU



NA MWANDISHI WETU

JAMII ya Wahadzabe nchini wameitaka serikali kuhakikisha kuwa ina wapatia nyama ya nyani na ngiri Agosti 24 na 25 mwaka huu, kwa ajili ya kujikusanya ili wapate kutekeleza mpango wa sensa itakayofanyika Agosti 26 kinyume cha hapo itakuwa ni vigumu kwao kuhesabiwa.

Kiongozi wa jamii hiyo, Athuman Gwamanda, alisema kupatiwa nyama hiyo kutawafanya siku hiyo kutulia katika maeneo maalum na kurahisisha viongozi wanaosimamia zoezi hilo la kuhesabu watu kuwapata kirahisi na kuwahesabu.

Alisema iwapo serikali haitawapatia mahitaji hayo itambuwe kuwa hawatakuwa tayari kuhesabiwa siku hiyo kwani wataendelea na shughuli zao za ukusanyaji wa matunda kama kawaida hivyo kufanya zoezi hilo la kuhesabiwa kuwa gumu.

Gwamanda alitanabaisha kuwa nyama ya nyani kwa siku hiyo itakuwa na umuhimu kwani imekuwa ikitumika kuwapatia supu akina mama ambao wamejifungua watoto ambapo nyama ya ngiri ni maalum kwa matambiko ambayo yanafanyika kila siku katika jamii hiyo.

Alitaja nyama nyingine kama nyumbu punda kuwa ni kwa ajili matumizi ya chakula cha kawaida.

Aidha, alisema jamii hiyo minatambuwa umuhimu wa sensa lakini hata hivyo, kwa upande mwingine wanaona kama haiwasidii kwani huduma nyingi za kimaendeleo huwa hazi wakii kirahisi kwa mfano wao hawahitaji hospitali shule wala barabara.

Jamii hiyo ambayo inakisiwa kufikia idadi ya watu wasiopungua 1700 imekuwa ikiishi katika mapori ya vijiji vya Yaeda Chini Mkoani Manyara ambapo wamekuwa wakiishi katika vikundi vidogo vidogo katika maeneo ya mkoa huo.

No comments: