Tuesday, November 27, 2012

MSANII/MUIGIZAJI/MCHEKESHAJI SHARO MILIONEA HAYUPO NASI.




Msanii/Muigizaji/Mchekeshaji Hussein Ramadhani Mtioeti (27) maarufu SHARO MILIONEA amefariki dunia katika ajali ya gari jijini Tanga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Prudence Masawe, amethibitisha kutokea kwa ajali na kusema kuwa marehemu amefikwa na umauti baada ya gari lake aina ya Toyota Haria lenye namba za usajili T478DVR kuacha njia na kupinduka.
Hili ni pigo jingine kwa Tasnia ya Filamu nchini Tanzania, hasa ukizingatia kuwa juma lililopita alifariki msanii Mlopelo na wakati Sharo Milionea anafariki tayari tasnia hiyo ya bongo Move ipo katika Msiba mwingine mzito wa Mcheza Filamu John Steven anaetarajiwa kuzikwa kesho.
Kamanda Massawe amesema kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa mbili usiku wa Novemba 26, 2012 katika kijiji cha Maguzoni Soga Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga.
Akisimulia zaidi RPC Massawe anasema kuwa marehemu alikuwa akiendesha gari hilo na alikuwa peke yake bila abiria mwingine na ajali kumfika akiwa katika kijiji hicho kilichopo kati ya segera na Muheza.



“Marehemu ndie alikuwa akiendesha gari lile, na lililopopinduika yeye alirushwa nje lkupitia kiooo cha mbele na umauti kumfika hapo hapo” alisema Kamanda Massawe.
Aidha Kamanda Massawe amesema msanii huyo alikuwa akitokea jijini Dar es Salaam na alikuwa akienda nyumbani kwao Muheza.
Inakumbukwa kuwa Msanii huyo aliyejizolea umaarufu mkubwa kwa staili yake ya utembeaji na uongeaji alipata al;inusurika katika ajali nyinge mapema mwaka huu baada ya basi alilokuwa akisafiria la Taqwa kutoka nchi jirani ya Burundi kupata ajali Mikese mjini Morogoro Januari 5 mwaka huu akirejea Dar es Salaam


FOURWAYSBUKOBA Blog inatoa salamu za Pole kwa Familia, wasanii wa Filamu, Vichekesho na muziki nchini kwa Msiba huo mzito hasa ukizingatia kuwa bado wapo katika Msiba wa Mcheza filamu John Stephen anaetarai kuzikwa kesho Makaburi ya Kinondoni.
KAZI YA MUNGU HAINA MAKOSA

No comments: