Tuesday, August 13, 2013

CHEZEA MZUNGU WEWE !!!!!!!!!!Waliomwagiwa tindikali kupandikizwa ngozi tena

acid d5ef7


Wasichana wawili ambao ni raia wa Uingereza waliokuwa walimu wa kujitolea mjini Zanzibar, Kate Gee (18) na Kristie Trup (18), ambao walimwagiwa Tindikali, sasa wanatakiwa kupandikizwa ngozi nyingine. (HM)

 
Akizungumza Daktari Mohammed Jawad, ambaye anawaangalia kwa ukaribu zaidi wagonjwa hao, alisema kwamba Katie ambaye aliathirika zaidi anahitaji kupandikizwa ngozi nyingine.
 
Alisema kutokana na majeraha ambayo aliyapata mwalimu huyo aliharibika ngozi yake hivyo anahitajika kupandikizwa ngozi nyingine ili arudi katika hali yake ya kawaida.
 
"Vipimo vilionyesha kwamba mgonjwa huyo alipata majeraha makubwa hivyo anahitajika kupandikizwa ngozi nyingine," alisema.
 
Kwa sasa walimu hao wanapata huduma ya matibabu katika Hospitali ya Chelsea and Westminster iliyopo London walikopelekwa wakitokea Tanzania wiki iliyopita.
 
Familia ya wagonjwa hao imeonekana kuwa karibu zaidi na mabinti hao baada ya kuwapeleka moja kwa moja hospitalini hapo kwa matibabu zaidi.
 
Msemaji wa hospitali hiyo alisema kwamba wagonjwa hao wanaendelea na matibabu vizuri na hali zao siyo mbaya sana kama ilivyokuwa awali.
 
"Wagonjwa wanaendelea vizuri na matibabu na kila siku familia zao zinakuja hapa kuwaona na kuwafariji, kwa kweli hali zao ni nzuri," alisema msemaji huyo wa hospitali hiyo.
 
Siyo mara ya kwanza
Mtandao mmoja wa kijamii unaofahamika kwa jina la www.ziro99.blogspot.com umeandika taarifa kwamba walimu waliomwagiwa tindikali mjini Zanzibar walishawahi kumwagiwa tena.
 
Habari za kuaminika zilizopatikana kupitia mtandao huu zilifichua kwamba mmoja wa walimu hao alishawahi kushambuliwa wakati akiwa kisiwani humo wiki mbili zilizopita.
 
Kwa mujibu wa mmoja wa marafiki zao, akizungumza kupitia katika mtandao huu Oli Cohen, mwenye miaka 21, alisema: "Katie alishambuliwa wiki mbili zilizopita na mwanamke mmoja wa Kiislamu baada ya kuimba wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani."
 
"Alishtushwa mno na tukio hilo, lakini hakupatwa na hofu kiasi cha kufikiria kurejea nyumbani. Akaendelea kuishi hapo kumalizia safari yake na kazi yake ya kujitolea." Chanzo: mwananchi

No comments: