P.T
Wakizungumza na mwandioshi wa habari
hizi leo eneo la tukio wananachi wa eneo hilo walisema kuwa bwawa hilo
limeendelea kupoteza maisha ya wananchi wa eneo hilo na kuwa kila mwaka
lazima kutokee tukio la mtu kufa maji.
Hivyo walisema kuwa kutokana na bwawa hilo kutokuwa na msaada mkubwa kwao kutokana na maji yanayopatikana hapo kuwa machafu yasio na yasiyotumika kwa matumizi ya kunywa wala kupikia chakula wanaomba uongozi wa Manispaa ya Iringa kuangalia uwezekano wa kufukia bwawa hilo ama kuliwekea uzio kwa usalama wao .
Akizungumza kwa niaba ya wananchi wenzake waliofika kushuhudia tukio hilo Yona kalinga alisema kuwa bwawa hilo kwa sasa linatumika zaidi na wakandarasi wanaojenga barabara mbali mbali ikiwemo ya Iringa- Dodoma kwa kuchota maji ya kumwagilia barabara wanazojenga .
" Tunashindwa kujua kwa nini Manispaa ya Iringa inashindwa kufukia bwawa hili ama kuweka uzio kuzunguka bwawa ili kuepusha madhara zaidi kwa watoto na wananchi wanaozunguka bwawa hilo"
Mjumbe wa serikali ya mtaa wa Kihesa Kilolo Mary kabogo alisema kuwa tukio la mtoto huyo kufa maji lilitokea juzi ambapo mtoto huyo alitoweka nyumbani katika mazingira ya kutatanisha mara baada ya kushiriki chakula cha jioni .
Alisema kuwa mtoto huyo ambae alikuwa akiishi na bibi yake baada ya kutoweka uongozi wa serikali ya mtaa na wananchi walifanya jitihada za kumtafuta katika maeneo mbali mbali na kukiri kuwa tukio la pili kwa watu kufa maji katika eneo hilo.
Hata hivyo alisema uongozi wa serikali ya mtaa huo unaungana na mawazo ya wananchi kutaka eneo hilo kuwekewa uzio uli kuepusha ajali zaidi ya maji kwa watoto na watu wazima.
Kuhusu mtoto huyo inasadikika alikufa maji baada ya kufika eneo hilo kwa lengo la kuogelea katika bwawa hilo.
Kabogo alisema kupitia miradi ya TASAF wanampango wa kupendekeza eneo hilo kuwekwa uzio kama njia ya kuwaepushia ajali zaidi na kuwa tayari suala la kupendekeza eneo hilo kuwekewa uzio lipo katika mipango ya mtaa huo.Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo .

No comments:
Post a Comment