Friday, March 22, 2013

KAMATI ZA BUNGE ZAENDELEA NA KAZI DAR ES SALAAM

IMG_0718
Msaidizi wa CAG Ndg. Fransis Mwakapalila wa tatu kutoka kushoto akisoma ripoti za ukaguzi zilizofanywa na Ofisi ya CAG mbele ya kamati ya LAAC wakati wa vikao vya kamati leo Dar es salaam, Kamati ya Bunge ya LAAC ilikutana na wataam kutoka Ofisi mbalimbali na CAG kuangalia baadhi ya utekelezaji wa majukumu yake

IMG_0723
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Abdalah Kigoda akifafanua jambo mbele ya wajumbe wa kamati ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara katika kikao kilichofanyika Ofisi ya Bunge leo. Kamati hiyo ilikutana na watendaji wa wizara hiyo kwa lengo la kupata taarifa ya utekelezaji wa majukumu yake. Katikati ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Mahamoud Hassan Mgimwa (Mb) na aliyekushoto ni Ndg. Michael Kadebe, katibu wa Kamati hiyo.  IMG_0738
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Mussa Hassan Zungu na baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo akiwa katika picha ya pamoja na Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Tanzania mara baada ya kukutana nao leo. kamati hiyo ilikutana na wabunge hao kupata taarifa kutoka Bunge la Afrika Mashariki.

No comments: