LEO Jumanne, Macho na Masikio ya wengi yakiwa yameelekeza kwenye uwanja wa Nou Camp kushuhudia mpambano wa Marudiano za Raundi ya Mtoano ya UCL, UEFA CHAMPIONS LEAGUE Barcelona wameweza kurudisha goli zote mbili ambazo zimefungwa na Lionel Messi, Akifunga goli la kwanza dakika ya 5 na goli la pili kulifunga dakika ya 39.
Ac Milan wamecheza kipindi chote cha kwanza kwa kulinda lakini mpaka Barcelona wanarudisha magoli yote hayo walikuwa wanapita kwenye ngome yao kama kawaida. Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinaisha Barcelona walikuwa wanaongoza kwa bao 2-0 na Agg ikiwa ni 2-2.
Nani kama Lionel Messi, akitupia goli la pili na kufanya 2-0 na Agg ikiwa 2-2
Kipindi cha pili Barcelona waliweza kuongeza bao jingine kupitia kwa David Villa katika dakika ya 57 baada ya mchezaji wa Ac Milan kuukosa mpira huo na hatimaye David Villa kuupata na kutupia nyavuni. Dakika za lala salama Ac Milan wakafanya makosa yale yale wakachapwa goli la 4 bila kutegemea na kushtukiziwa haraka haraka na hatimaye mchezaji wa Barca Jordi Alba kutokomeza bao katika dakika ya 90 na kufanya 4-0 na Agg Ikiwa 4-2.Mashabiki wa Barca wakiwa wametupia meseji zao kiaina kushinikiza kichapo kwa Ac Milan
Lionel Messi akipongezwa.
David Villa akifunga bao la kirahisi baada ya mchezaji wa Ac Milan kuukosa mpira huo na hatimaye kumfika miguuni David Villa na kuipachikia bao la tatu Barcelona.
David Villa akishangilia baada ya kutupia gili la 3
Wachezaji wa Milan wakiwa wamemweka mtu kati... Messi....
Tito Vilanova wa Barcelona akiwa anajionea timu yake ikichinja mtu
Ronnie Wood (of Rolling Stones fame)naye alikuwepo kwenye mtanange huo uliokuwa na mashabiki wengi hapo Nou Camp
David Villa akishangilia baada ya kufunga goli la 3 usiku huu
VIKOSI:
Barcelona: Valdes, Dani Alves, Pique, Mascherano, Jordi Alba, Xavi, Busquets, Iniesta, Pedro, Messi, Villa.
Subs: Pinto, Fabregas, Puyol, Sanchez, Adriano, Song, Tello.
Goals: Messi 5, 40, Villa 55, Jordi Alba 90.
AC Milan: Abbiati, Abate, Mexes, Zapata, Constant, Montolivo, Ambrosini, Flamini, Niang, Boateng, El Shaarawy.
Subs: Amelia, De Sciglio, Muntari, Robinho, Nocerino, Bojan, Bonera.
Ref: Viktor Kassai (Hungary)
Subs: Pinto, Fabregas, Puyol, Sanchez, Adriano, Song, Tello.
Goals: Messi 5, 40, Villa 55, Jordi Alba 90.
AC Milan: Abbiati, Abate, Mexes, Zapata, Constant, Montolivo, Ambrosini, Flamini, Niang, Boateng, El Shaarawy.
Subs: Amelia, De Sciglio, Muntari, Robinho, Nocerino, Bojan, Bonera.
Ref: Viktor Kassai (Hungary)
No comments:
Post a Comment