Ndugu zangu,
Njia yetu kwenye safari ya kwenda Brazil jana usiku imewekewa mlima na jamaa zetu wa Morocco. Niliuangalia mchezo mzima. Nilisikitika sana, kuwa, tulikuwa na bahati mbaya sana ya mchezaji wetu kupigwa red card kwenye kipindi cha kwanza na jamaa zetu wa Morocco kwenda mapumziko na goli moja mfukoni.
Niliiona hali ya kuchanganyikiwa kwenye benchi letu la ufundi. Na kosa kubwa lilikuwa kumtoa Ulimwengu. Ujumbe ulitumwa uwanjani kuwa sasa tunajihami zaidi. Ni kosa. Kulichangia kushindwa kwetu, maana, Morocco kwa jana hawakutisha kabisa. Tulitakiwa kujiamini na kuthubutu kuwashambulia badala ya kufikiri kujihami zaidi. Naam, jana tumeshindwa.
Tafsiri yake?
Kandanda ina miujiza yake na imetokea zaidi ya mara elfu moja. Na inavyoonekana kwenye karatasi
Watanzania tunaweza pia kuupanda mlima waliotuwekea WaMorocco tukisaidiwa na miujiza ya kandanda.
Mechi yetu na Ivory Coast sasa ndio itakayokuwa ’ Mama na Bibi’ wa mechi zote Taifa Stars kuwahi kucheza. Ni LAZIMA tuwafunge WaIvory Coast hapa nyumbani. Hata kwa goli moja tu.
Ina maana gani?
Ivory Coast wanaweza kupoteza mechi na sisi, na hata na Morocco. Watagota na pointi 10. Wakati huo huo, mbali ya kuwafunga Ivory Coast, sisi tunaweza kuwafunga pia Gambia hapa nyumbani na kumaliza na pointi 13. Lakini , sare na Gambia itatuweka pabaya kwa vile Ivory Coast wana idadi kubwa ya magoli ya kufunga kuliko sisi. Maana, wote tutamaliza na pointi kumi na Ivory Coast watasonga mbele kwa advantage ya magoli. Hivyo, tunalazimika kushinda mechi mbili zijazo na kubeba pointi zote sita. Inawezekana.
Faida nyinginezo mbele yetu?
Tukishinda mechi mbili zijazo na hata Ivory Coast wakishinda mechi yao na Morocco na kuibuka wa kwanza kwenye kundi, basi, nasi, tuna nafasi ya kwenye karatasi ya kuwemo kwenye ’ Best Loosers’ na hivyo kuendelea kuwemo kwenye mchakato wa safari ya kwenda Rio De Janeiro, Brazil.
Na hilo likishindikana, basi, kwa kushinda mechi mbili zijazo ni lazima tutapanda ngazi nyingi kwenye viwango vya FIFA. Nao ni ushindi pia.
Kila la Heri Taifa Stars Yetu!
Maggid,
Iringa.
0754 678 252

No comments:
Post a Comment