Wednesday, May 30, 2012

TANZANIA YAUNGANA NA NCHI NYINGINEZO DUNIANI KUADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA WALINDA AMANI WA UMOJA WA MATAIFA

Mgeni rasmi Naibu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Mahadhi Juma Maalim na Naibu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) hapa nchini Bibi. Hopolang Phororo na UwaGeneral Officer Commanding (GOC) Meja Jenerali Hassan Vuai Chema akitoa heshima zake.  wakishiriki kuimba wimbo wa taifa katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya walinda amani  Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa inayoadhimishwa kila Mwaka tarehe 29 Mei. Picha zote na MO BLOG
Mgeni rasmi Naibu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Mahadhi Juma Maalim  akiweka shada la maua katika mnara wa kumbukumbu ya mashujaa.
Naibu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) hapa nchini Bibi. Hopolang Phororo akiweka Shada la Maua kama ishara ya kuwakumbuka walinda Amani wa Afrika.
 General Officer Commanding (GOC) Meja Jenerali Hassan Vuai Chema akiweka shada la maua.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Azania wakitoa burudani za nyimbo za kuhamasisha Amani na Upendo.

Naibu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) hapa nchini Bibi. Hopolang Phororo akizungumza machache wakati wa maadhimisho hayo ambapo pia alisoma ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-Moon kuwa leo tunatoa heshima kwa Walinda Amani zaidi ya 2900 ambao wamepoteza maisha wakiwa kazini katika miaka iliyopita na kuahidi kuendeleza kazi yo kurejesha Amani katika nchi  zenye vita.
Amesema katika siku hii ya Umoja wa Mataifa ya Walinda Amani tuitumie kukumbuka jinsi watu walivyojitolea maisha yao, na tuahidi kuimarisha ushirikiano wa kidunia ambao unawafanya hawa wavaa kofia za Bluu waonekane kama alama ya Amani duniani kote.
Baadhi ya Mabalozi, Maafisa wa Ubalozi, Wakuu wa vitengo mbalimbali vya Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Wanadiplomasia, Maafisa wa Serikali na Maafisa kutoka jeshi la ulinzi la Wanachi wa Tanzania (JWTZ).
Baadhi ya Mabalozi, Maafisa wa Ubalozi, Wakuu wa vitengo mbalimbali vya Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Wanadiplomasia, Maafisa wa Serikali na Maafisa kutoka jeshi la ulinzi la Wanachi wa Tanzania (JWTZ).
Mgeni rasmi Naibu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Mahadhi Juma Maalim akitoa hotuba wakati wa maadhimisho ya Siku ya Walinda Amani Duniani 2012 ambapo amesema Kauli mbiu ya Mwaka huu imelenga kuunganisha majeshi yote ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa katika kuhakikisha bara la Afrika linakuwa na Amani na Utulivu.
Kauli mbiu ya Mwaka huu ni "PEACE KEEPING AS GLOBAL PARTNERSHIP".
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Mahadhi J. Maalim akiagana na baadhi ya Maafisa wa Vikosi vya kulinda Amani wa Umoja wa Mataifa.
Naibu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) hapa nchini Bibi. Hopolang Phororo akisalimiana na baadhi ya Maafisa wa Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa

No comments: