UNIVERSITY OF DAR
ES SALAAM
Academic Staff
Assembly
TAARIFA KWA UMMA
Hii ni kuitaarifu jumuiya ya Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam na umma kwa ujumla kuwa, katika kusheherekea uhuru wa Tanzania
Bara, Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDASA) kwa
ushirikiano na IPP Media wameandaa Kongamano la Uhuru litakalofanyika siku ya
Jumapili tarehe 9 Desemba 2012 katika Ukumbi wa Nkrumah kuanzia saa 8 alasiri
hadi saa 12 jioni. Mada kuu ya Kongamano ni, “Uhuru wetu na Mustakabali wa Taifa kwa Miaka 50 Ijayo”.
Kongamano hilo litajikita katika vipengele vifuatavyo:-
a) Amani na Utulivu wa Taifa letu kwa
Miaka 50 Ijayo;
b) Elimu na Maendeleo ya Taifa kwa
Miaka 50 Ijayo;
c) Rasilimali zetu kwa Maendeleo ya
Kiuchumi ya Taifa.
Kongamano hilo litarushwa moja kwa moja na
ITV, Radio One na Capital Radio ili wananchi wote waweze kufuatilia kongamano
hilo muhimu. Watakaongoza mjadala ni Prof. Gaudence Mpangala, Dkt Martha Qorro,
Dkt Haji Semboja, Dkt. Kitila Mkumbo, Bw. Maggid Mjengwa na Mhandisi Joshwa
Raya. Watakuwepo pia wazungumzaji waalikwa kama vile: Mzee Joseph Butiku, Dkt
Aldin Mutembei, Mh. January Makamba (Mb), Julius Mtatiro, Usu Mallya na Esther
Wassira.
Kongamano linategemewa kufungwa na Mh. Bernard
Membe (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Wote mnakaribishwa..Limetolewa na Uongozi wa UDASA
No comments:
Post a Comment