Mechi muhimu:
Manchester City v Queens Park Rangers
Sunderland v Manchester United
Kwa mara ya 6 katika historia ya Ligi Kuu England, Bingwa atapatikana Siku ya Mwisho lakini haijawahi kutokea Bingwa akapatikana kwa Tofauti ya Magoli.
Mbali ya hilo, hii ni mara ya kwanza kwa Timu pinzani za Mji mmoja kuwa ndizo zinazogombea Ubingwa.
Manchester City wao wanatafuta Ubingwa wao wa kwanza baada ya Miaka 44 wakati Manchester United wanataka kutetea Taji lao na kufikisha Ubigwa wa 13 tangu Ligi Kuu kuanzishwa na wa 20 kwa jumla.
Man United na Man City zote zina Pointi 86 lakini City wanaongoza wakiwa na ubora wa tofauti ya magoli manane.
Kwenye Mechi za Jumapili, ili kutwaa Ubingwa Man City wanahitaji kulingana au kupata matokeo bora kupita Man United labda itokee Man United wawashindilie Sunderland mibao kama mvua.
Lakini ikiwa Man City atatoka sare au kufungwa na QPR na Man United kuifunga Sundeland, Man United watatwaa Ubingwa.
.
KUFUZU KUCHEZA ULAYA
Mechi muhimu:
Everton v Newcastle
Tottenham v Fulham
West Brom v Arsenal
Arsenal, Tottenham Hotspur na Newcastle United wao watakamata nafasi za 3, 4 na 5 lakini yupi atakuwa wapi ndiyo Kitendawili.
Timu itakayomaliza nafasi ya 3 moja kwa moja itaingia hatua ya Makundi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao.
Timu itakayoshika nafasi ya 4 kawaida huanza Mechi za Mchujo za UEFA CHAMPIONZ LIGI lakini safari hii kuna utata kwani ikiwa Chelsea, ambaye yuko kwenye Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI kucheza na Bayern Munich hapo Mei 19, atashinda Ubingwa wa Ulaya wao ndio watacheza hatua ya Makundi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI na Timu itakayokamata nafasi ya 4 itacheza UEFA EUROPA LIGI.
Lakini, ikiwa Chelsea watafungwa na Bayern, basi ile Timu itakayokamata nafasi ya 4 itacheza Mechi za Mchujo za UEFA CHAMPIONZ LIGI na ile Timu ya nafasi ya 5 na Chelsea, ambao wao watamaliza Ligi wakiwa nafasi ya 6 na pia ndio Mabinngwa wa FA Cup, watacheza EUROPA LIGI.
Katika kutwaa nafasi ya 3, Arsenal wapo kwenye usukani wakiwa na Pointi 67, Spurs wa 4 na wana Pointi 66 na wa tano ni Newcastle wenye Pointi 65.
Arsenal wanahitaji ushindi tu kuchukua nafasi ya 3.
.
KUSHUKA DARAJA
Mechi muhimu:
Manchester City v Queens Park Rangers
Stoke City v Bolton Wanderers
Tayari Blackburn Rovers na Wolves zimeshuka Daraja na bado ipo Timu moja kuungana nao.
Queens Park Rangers wanapigania maisha yao kutoshushwa Daraja wakitinga Etihad kucheza na Man City ambao wanataka ushindi watwae Ubingwa.
Wengine wanaopigana kujinusuru ni Bolton Wanderers ingawa pia, kimahesabu, Aston Villa bado wapo hatarini.
Mahesabu ya hawa ni haya:
Bolton lazima waifunge Stoke ugenini au wanaporomoka.
Bolton wakishinda na QPR kufungwa na Man City, Bolton watapona.
Ikiwa QPR watapata sare na Man City, basi Bolton watalazimika kuifunga Stoke kwa tofauti ya bao 9 ili wao wanusurike.
ANASENAJE SIR ALEX FERGUSON?
Wakati Bosi wa Manchester United Sir Alex Ferguson akisali kuomba Manchester City wateleze wakicheza na QPR Jumapili na wao kuifunga Sunderland ili watwae Ubingwa, Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema wao wanataka ushindi wakicheza ugenini na West Bromwich Albion ili wajihakikishie kuchukua nafasi ya 3 na hivyo kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao.
Jumapili Mei 13 ndiyo Siku ya mwisho ya Msimu wa Ligi Kuu England na Timu zote 20 zitakuwa Uwanjani kwa wakati mmoja.
Akiongelea Mechi za Jumapili, Sir Alex Ferguson amesema: ‘Tunachoweza kufanya ni kushinda Mechi yetu na kuomba upuuzi utokee kwenye Mechi ya City’
Pia aliitaka QPR iige kilichofanywa na Aberdeen Mwaka 1983 wakati yeye ni Meneja wao walipoifunga Timu kigogo Real Madrid kwenye Fainali ya Kombe la Washindi Barani Ulaya.
Alisema: ‘Mika 29 iliyopita niliichukua Aberdeen na tuliwafunga Real Madrid kwenye Fainali ya Ulaya tukiwa na Wachezaji wadogo wa nyumbani tu!’
Aliongeza: ‘Hii ni changamoto kwa QPR-kufanya walichofanya Aberdeen! City ni wagumu lakini siku zote binadamu ni binadamu na huwezi jua nini kitatokea!’
Nae Arsene Wenger, ambae Timu yake Arsenal inataka ushindi tu ili kutwaa nafasi ya 3, ametamka: ‘Tukishinda Mechi na WBA basi nafasi ya 3 ni yetu na hatujali matokeo mengine!’
Meneja wa klabu ya Manchester city Roberto Mancini anasema ana imani na wachezaji wake kutimiza jukumu lao na kuvishwa kilemba cha Mabingwa wa msimu huu.
Roberto Mancini amesema: Nawaamini kwa asili mia 100. Wanafahamu vyema kua ushindi wa Ligi na kuin'goa United kutoka kilele cha soka ilichoshikilia kwa mda mrefu ni jukumu lao.
Aliongezea kusema kua' wamejitahidi na kupambana kila wanapoingia uwanjani katika Ligi ambayo ni mojapo ya Ligi kali duniani.
Mancini amemalizia kwa kusema ninavyohisi ni kwamba mwishoni ni mshindi ni yule anayestahili ushindi''
Klabu ya City iliongoza ligi kwa pointi 8 na kujikuta nyuma ya mahasimu wao Manchester united kwa pointi 8 baada ya kufungwa kwenye uwanja wa Arsenal tareh 8 mwezi Aprili.
Manchester City inapambana na QPR kwenye uwanja wa Etihad huku United ikielekea uwanja wa Brittania kuchuana na Sunderland.
Mancini anasema kua "nadhani kwa wakati huu ilikua bora kwentu kupoteza mechi dhidi ya Arsenal, kwa sababu hilo lilitupunguzia shinikizo''
Daima tumeamini, na kuendelea kucheza soka safi licha ya kua na matatizo kipindi cha mwezi mmoja tu.
Adel Tarabti
Ferguson na Meneja wa QPR Mark Hughes wamezielezea mbinu za Mancini kama za kuzuia, ambapo Ferguson anadai kuwa walipocheza dhidi ya City ilitumia wacheza kiungo watano.
MAREFA MECHI ZA JUMAPILI HII:
Chelsea v Blackburn Rovers
-Lee Mason [Saa 11 Jioni]
Everton v Newcastle United
-Andre Marriner [Saa 11 Jioni]
Manchester City v Queens Park Rangers
-Mike Dean [Saa 11 Jioni]
Norwich City v Aston Villa
-Martin Atkinson [Saa 11 Jioni]
Stoke City v Bolton Wanderers
-Chris Foy [Saa 11 Jioni]
Sunderland v Manchester United
-Howard Webb [Saa 11 Jioni]
Swansea City v Liverpool
-Mike Halsey [Saa 11 Jioni]
Tottenham Hotspur v Fulham
-Phil Dowd [Saa 11 Jioni]
West Bromwich Albion v Arsenal
-Mike Jones [Saa 11 Jioni]
Wigan Athletic v Wolverhampton Wanderers
-M Oliver [Saa 11 Jioni]
MSIMAMO WA SASA ULIVYO KABLA YA LEO.
[Kila Timu imecheza Mechi 37, kwenye Mabano Tofauti ya Magoli]
1 Man City Pointi 86 [63]
2 Man United 86 [55]
3 Arsenal 67 [24]
4 Tottenham 66 [23]
-------------------------------------
5 Newcastle 65 [7]
6 Chelsea 61 [21]
7 Everton 53 [8]
8 Liverpool 52 [8]
9 Fulham 52 [-1]
10 WBA 47 [-6]
11 Sunderland 45 [0]
12 Swansea 44 [-8]
13 Norwich 44 [-16]
14 Stoke 44 [-17]
15 Wigan 40 [-21]
16 Aston Villa 38 [-14]
17 QPR 37 [-22]
--------------------------------------
18 Bolton 35 [-31]
19 Blackburn 31 [-29] =IMESHUSHWA DARAJA
20 Wolves 25=IMESHUSHWA DARAJA
No comments:
Post a Comment