Tuesday, June 19, 2012

Mnyika Akitoka Nje Ya Bunge


Mbunge wa jimbo la Ubungo John Mnyika akitoka nje ya viwanja vya Bunge la Tanzania jana mjini Dodoma baada ya kukataa kufuta kauli ya kumdhalilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa dhaifu. Mbunge huyo alitoa kauli hiyo wakati akichangia Bajeti ya serikali ya mwaka 2012/13 katika mkutano unaoendelea.Picha na Tiganya Vincent- MAELEZO- Dodoma



Mbunge wa Jimbo la Ubungo John Mnyika akiteta na Mbunge wa jimbo la Wawi Hamad Rashid Mohamed (kushoto) na Mbunge wa Bariadi Mashariki John Cheyo mara baada ya kuondolewa Bungeni jana mjini Dodoma baada ya kukataa kufuta kauli ya kumdhalilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa dhaifu. Mbunge huyo alitoa kauli hiyo wakati akichangia Bajeti ya serikali ya mwaka 2012/13 katika mkutano unaoendelea.





Mbunge wa jimbo la Ubungo John Mnyika akitoka katika ukumbi wa Bunge la Tanzania jana mjini Dodoma baada ya kukataa kufuta kauli ya kumdhalilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa dhaifu. Mbunge huyo alitoa kauli hiyo wakati akichangia Bajeti ya serikali ya mwaka 2012/13 katika mkutano
unaoendelea. 

MSIMAMO WA MBUNGE WA UBUNGO JOHN MNYIKA KUHUSU KAULI ALIYO ITOA BUNGENI

   John Mnyika akisindikizwa na askari wa bunge. picha kwahisani ya issamichuzi.blogspot.com
Huu ndio msimamo wa mbunge wa ubungo jonh mnyika baada ya kutolewa leo bungeni

Msimamo wangu wa sasa juu ya Kauli yangu bungeni!

Nitatoa tamko la kina baadae kuhusu kilichotokea lakini kwa ufupi ubovu wa bajeti hii ni matokeo ya udhaifu wa Rais Kikwete, yeye ndiye aliyesaini Mpango wa Taifa wa miaka mitano kama Kiongozi Mkuu wa Nchi tena kwa wino mwekundu kama Amiri Jeshi Mkuu. Na yeye ndiye Mwenyekiti wa baraza la mawaziri, bajeti hii iliyoacha kuzingatia mpango wa Taifa imepita kwenye baraza alilloliongoza, pia kushindwa kutekelezwa kwa bajeti iliyopita ni matokeo pia ya udhaifu wa taasisi ya Urais.

Pia kwa mujibu wa Katiba Rais ndiye ambaye anapeleka bajeti bungeni, Waziri mwenye dhamana anapeleka tu kwa niaba. Rais amepewa mamlaka makubwa juu ya bajeti ibara ya 99 imeweka mipaka kuhusu mambo ambayo bunge lina mamlaka nayo huku ibara ya 90 inasema bunge likikataa bajeti rais ana mamlaka ya kuvunja bunge. Hivyo Rais Kikwete anapaswa kuagiza Waziri wa Fedha bajeti iondolewe irudi kwenye baraza la mawaziri ikafanyiwe marekebisho!

No comments: