Shirikisho la Filamu TanzaniaTAFF limeandaa Semina ya siku mbili kwa ajili ya kutayarisha mpango Mkakati wa miaka mitano ijayo. Semina hiyo itafanyika katika ukumbi wa Ofisi za TCRA Jengo la Mawasiliano Towers ubungo kuanzia saa 3 asubuhi tarehe 30 – 31, Julai 2012.
Semina hiyo inafuatia baada ya kufanyika ya awamu ya kwanza ambayo ilifanyika 28 – 20 Mei 2012 katika Ukumbi wa Hotel ya White Mark iliyopo eneo la Ubungo Plazza Mjini Dar es Salaam.
Aidha Wajumbe wataohudhuria semina hiyo wanatoka taasisi za Benki za N.M.B, CRDB , Backelys Bank, Bank of India, TRA , TCRA, TBS, NSSF , Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Bodi ya Filamu Tanzania, BASATA, COSOTA, ITV Equity Bank, European Union, Foundation for Civil Society, Ubalozi wa Sweden, Uholanzi, US – AID, Global Publishers, UNESCO, UNICEF, TGNP, T.I.B Mpigile Company , Wizara ya Viwanda Biashara, Tigo, Vodacom, TBL, ADB, TWAWEZA, Ubalozi wa Canada, Ubalozi wa Ufaransa , Ubalozi wa Denmark ,Wasanii kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Morogoro, Mwanza,Pwani na Dodoma..
Malengo ya Semina hiyo ni kujadili na kuweka utekelezaji wa vipaumbele muhimu vya utekelezaji wa majukumu ya Shirikisho la Filamu.
No comments:
Post a Comment