Sunday, April 22, 2012

REAL YAISHUGHULIKIA BARCA, NI KAMA TAYARI MABINGWA

Barcelona Vs Real Madrid 1-2 21/4/2012 [HD] (All Goals) 


 
REAL Madrid wapo karibu mno na ubingwa wa Ligi Kuu ya Hispania, La Liga wakihitaji kushinda mechi moja tu zaidi ili kujihakikishia taji hilo.
Hiyo inafuatia ushindi wa mabao 2-1 leo kwenye Uwanja wa Camo Nou katika mchezo wa marudiano wa La Liga.
Zikiwa zimebaki mechi nne ligi hiyo kuisha, Real sasa wanaizidi pointi saba Barca.
Vijana wa Jose Mourinho walipania haswa leo na hawakuwa wenye kutaka mzaha hata kidogo, kwani iliwachukua dakika 17 tu kupata bao la kwanza, mfungaji S. Khedira.
Barca walirudi kwenye vyumba vya kupumzikia mbele ya maelfu ya mashabiki wao wakiwa vichwa chini kutokana na kuwa nyuma kwa bao hilo.
Kipindi cha pili Barca walilazimika kusubiri hadi dakika ya 70, kupata bao la kusawazisha, mfungaji Sanchez.
Wakati wengi wakiamini historia ya Barca kutoka nyuma mbele ya Real na kushinda itaendelea, mwanasoka bora wa zamani wa dunia, Mreno Cristiano Ronaldo alibatilisha imani hiyo.
Dakika tatu tu tangu Sanchez aifungie Barca, Ronaldo aliifungia Real bao la ushindi kufuatia kazi nzuri ya Ozil.

 

 

No comments: