Saturday, April 28, 2012

HOSPITALI YA SELIANI YATOA MSAADA WA MADAWA



Na ASHURA MOHAMED-ARUSHA

HOSPITALI ya Seliani iliyopo mkoani hapa imetoa msaada wa madawa kwa wagonjwa zaidi ya 50 wenye magonjwa sugu katika kanisa la KKKT usharika wa Ilboru.

Akikabidhi misaada hiyo kwa wagonjwa hao mhudumu wa Hocpiece/Home based care kutoka hospitali hiyo Bw. Emanueli Abrahamu alisema kuwa jamii inatakiwa kujitokeza na kuwatia moyo wasiojiweza ili wasijione wametengwa .

Aidha alisema kuwa watanzania wanatakiwa kuacha kuwanyanyapaa wagonjwa kwa kuwanyima haki zao za msingi  na badala yake wawapatie misaada na kuwatia moyo ili wazidi kuishi kwa matumaini

Vile vile aliwaasa wagonjwa kuacha kujinyanyapaa kwani unyanyapaa huondoa utu wa mtu ambapo unyanyapaa mojawapo ni pamoja na kuacha masharti ya utumiaji wa madawa na kutokuhudhuria sehemu zinazotolewa misaada .
Nae bw Elphas Thomas ambaye ni mwinjilisti wa kanisa hilo alisema kuwa wagonjwa ambao wamepatiwa misaada huo wa madawa ya kupunguza makali  ni wale    wenye magonjwa kama vile kansa,ukimwi na TB.

Aidha alieleza kuwa misaada mingine iliyotolewa  kwa wagonjwa hao ni pamoja na nguo,vyakula,na matunda ambapo pia huduma hiyo inategemea kuwahudumia wagonjwa zaidi ya elfu tatu na mia sita ambao wapo majumbani.

Hata hivyo wagonjwa hao waliopatiwa misaada hiyo waliishukuru taasisi ya selian kwa kuwapatia msaada huo nna kusema kuwa watakuwa wajumbe wa kuwashauri kwenda kupima afya zao ili kupunguza maambukizi ya magonjwa hayo sugu.

No comments: