Wednesday, April 11, 2012
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa  Injinia Stella Manyanya akizungumza na viongozi wa kata ya Katandala (Hawako  Pichani) katika Ofisi za Kata hiyo katika Manispaa ya Sumbawanga jana kwenye  kikao cha Kamati ya kuhamasisha na kuchangisha fedha kwa ajili ya kumalizia  ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Shule ya Kilimani Azimio ili kuwezesha  wanafunzi waliofaulu na kukosa vyumba vya madarasa waweze kwenda Shule kabla ya  mwezi huu wa Aprili kuisha. (Picha na Hamza Temba-Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)- rukwareview.blogspot. com  
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia  Stella Manyanya akizungumza na waandishi wa habari Peti Siyame (Dailynews/  Habari Leo, kushoto)  na Mussa Mwangoka  (Mwananchi, kulia) jana  walipotaka  kujua juu ya kampeni iliyoanzishwa na Serikali ya Mkoa wa huo katika kuhamasisha  wananchi kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule za Sekondari  katika Manispaa ya Sumbawanga ili kuhakikisha wanafunzi waliofaulu wanakwenda  shule kabla ya mwezi huu kuisha. Katikati ni Mkurugenzi wa Manispaa ya  Sumbawanga Ndugu William Shimwela. Tangu kampeni hiyo ianzishwe ni wiki moja  sasa na tayari wananchi wengi wamehamasika kuchangia. (Picha na Hamza Temba-Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)  
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa  Injinia Stella Manyanya akizungumza na wakazi wa Kata ya Majengo katika Manispaa  ya Sumbawanga huku akiwasisitiza juu ya usafi wa mazingira katika mtaa wao  pamoja na kuwaagiza kuchangia katika sekta ya elimu kwa ajili ya ujenzi wa Shule  za Kata kama ilivyo sera kuu ya Serikali katika Shule hizo kuwa ni shule za  jamii hivyo wanapaswa kuchangia na Serikali kuwaongezea nguvu. (Picha na Hamza Temba-Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)- rukwareview.blogspot. com.



No comments:
Post a Comment