Mwili wa Marehemu Kanumba!!!!
Hapapitiki kuingia Nyumbani kwa Marehemu Kanumba,njia imezibwa magari hayaingii ni kwa miguu tu na Trafiki yupo kazini.
Hali Nyumbani kwa Kanumba.
' Lulu'
' Lulu'
Inatia huzuni kweli pole dada.
Dada huyu wakati anaingia kapiga mayowe hadi huruma,Kaingia na night dress.
TBC ikiwa na maojiano na wanafamilia ya Kanumba
Tasnia ya filamu nchini Tanzania inaomboleza kifo cha msanii maarufu wa filamu nchini hapa Steven Kanumba ambaye amefariki usiku wa kuamkia Jumamosi nyumbani kwake Sinza Vatican jijini Dar es Salaam. Taarifa zinasema marehemu alisukumwa na kuanguka na kugonga kichwa chini upande wa Nyuma na kusababisha kifo chake.
Polisi mkoani Dar es Salaam imethibitisha kuwa inamshikilia kwa mahojiano msanii huyo wa kike kutokana na kuhusika na kifo cha Kanumba, ambaye alijizolea umaarufu mkubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati na hadi Afrika Magharibi baada ya kuwashirikisha katika filamu zake baadhi ya wasanii Maarufu wa Kinigeria akiwemo Mercy Johnson na Noah Ramsey.
Marehemu ambaye alizaliwa mwaka 1984, alianza kujipatia umaarufu mwanzoni mwa mwaka 2000 wakati huo akiigiza katika Michezo ya luninga kupitia kundi la maigizo la Kaole Sanaa.
Aliendelea na kuigiza filamu nyingi ambazo zilimpatia umaarufu mkubwa kiasi cha kusafiri mara kadhaa nchi za nje, ambako alitambulika kama mmoja wa wasanii wenye vipaji vikubwa ambaye aliitangaza fani ya filamu nchini Tanzania maarufu kama Bongo Movies.
Tangu kuanza kutangazwa kwa taarifa za kifo chake mapema alfajiri, mamia kwa maelfu ya watu wamekuwa wakimiminika kwa wingi nyumbani kwa marehemu, huku vyombo vingi vya habari vikizipa kipaumbele mara kwa mara taarifa za kifo cha msanii huyo.
MAMA YAKE KANUMBA ALIVYOPOKEA TAARIFA ZA MSIBA WA MWANAE HUKO BUKOBA
Mama Mzazi wa Steven Kanumba anayeitwa Flora Mtegoa.
WAKATI Taifa la Tanzania likiwa katika majonzi mara baada ya kupoteza moja kati ya vijana wake walio peperusha vyema ndani na nje ya mipaka pendera yake kupitia tasnia ya Filamu STEVEN KANUMBA, yafuatayo ni mahojiano kati ya mdau wa blog ya G. Sengo mkoani Kagera mwandishi wa habari anayeitwa Nicolaus Ngaiza, aliyoyafanya na Mama Kanumba (Flora Mtegoa).
Katika mahojiano yaliyofanyika leo majira ya saa nane mchana katika uwanja wa ndege Bukoba katika harakati za safari kuelekea jijini Dar es salaam ILIKUWA HIVI:-
Nicolaus Ngaiza:- Mama unamwelezeaje Steven Kanumba katika kipindi cha uhai wake?
MAMA:- Kanumba mtoto wangu mtiifu, rafiki yangu, mpendwa wangu, mtotowangu wa karibu na jana niliongea naye kwenye simu na alfajiri naambiwa kafa.
Nicolaus Ngaiza:- Pengine alizaliwa sehemu gani mwaka gani?
MAMA:- Kanumba alizaliwa tarehe 8/1/1984 mkoani Shinyanga, katika hospitali ya Government Shy.
Nicolaus Ngaiza:- Baba yake yuko hai?
MAMA:- Baba yake yuko hai yuko Shinyanga anaitwa Charles Kanumba
Nicolaus Ngaiza:- Katika kipindi hiki kigumu unawambiaje watu wa Bukoba?
MAMA:- Naomba waniombee kwani hali yangu siyo nzuri kwani niko katika kipindi hiki kigumu.
Nicolaus Ngaiza:- Labda mama kijijini kwenu ni wapi?
MAMA:- Mimi natoka Wilayani Muleba, kata ya Izigo, kijiji cha Itojo.
Nicolaus Ngaiza:- Steven Kanumba sisi tunamjua kwa jina hilo jeh! hakuwa na jina la kinyumbani?
MAMA:- Hakuwa na jina lolote la kinyumbani zaidi ya hilo Kanumba la Kisukuma yeye ni msukuma.
Nicolaus Ngaiza:- Tungependa kujuwa neno la mwisho mlio weza kuzungumza pamoja.
MAMA:- Aliniambia mama natuma nauli uje tuagane naondoka naenda Marekani, akiwa mwenye furaha, tunataniana...
Nicolaus Ngaiza:- Labda aliwahi kukwambia ndoto zake katika maisha kwamba analenga kufanya nini?
MAMA:- Yeye ndoto zake ni kuendeleza sanaa yake na ninashukuru alikuwa amefika mbali kisanaa.
Nicolaus Ngaiza:- Labda kifamilia alikuwa ameoa au alikuwa na mtoto?
MAMA:- Hajawahi kuoa na hakuwa na mtoto...

Mpaka mama mzazi wa kanumba anaondoka tuliweza kupata maneno hayo tu toka kwa mama huyo ila tuliendelea kuongea na mama yake mdogo anayeishi maeneo ya bukoba mjini yeye amesema kuwa mpaka sasa ajielewi ila anasubili wakifika dar es salaam ndo atajua nini niaendelea
Je taratibu za mazishi ziko je?Kwa kuwa wazazi wa Kanumba wapo hai siwezi sema mwanetu atazikwa wapi ila nahisi ni mwazna au huko huko Dar
CHANZO: MJENGWA BLOG
Mwakilishi wetu kutoka Bukoba aliyesafili mpaka Dar es salaam ataendelea kutujuza zaidi juu ya msiba huo tukae pamojaaaaaaaaaaaaaaaaaa..................
No comments:
Post a Comment