Saturday, April 21, 2012

UVUMI WA TETESI KATIKA MITANDAO YA KIJAMII USIKU WA KUAMKIA LEO

UNAWEZA KUWA WA KWELI AU HAPANA

Mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe 
 Kutokana na uvumi ulioenea usiku wa kuamkia leo huko Dodoma kufuatia shutuma za wabunge dhidi ya mawaziri kadhaa wa Wizara wanaotuhumiwa kutowajibika vya kutosha na kutuhumiwa kwa wizi katika wizara wanazoziongoza, usiku wa mkuamkila leo Katibu wa wabunge wa CCM bungeni mama Jenista Muhagama amewaambia waandishi wa habari kwamba ni kweli walikuwa na kikao na wamechukua maamuzi magumu, lakini yeye siyo msemaji wa suala hilo hivyo huenda taarifa zaidi zitatolewa ufafanuzi wakati wowote kuhusu suala hilo,  msemaji  wa wabunge wa CCM Bungeni ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

Wabunge wa CCM walichachamaa sana katika suala hili na wamelivalia njuga  vyakutosha wakipaza sauti kwamba lazima mawaziri hao wawajibike, tutawaletea taarifa zaidi kadiri tutakavyozipata. 

No comments: