Rais Barack Obama amesema kwamba watu wa jinsia moja wawe na haki ya kuoana.
Bwana Obama amesema daima amekuwa  mgumu kukubali kwamba wanaume na wanawake wenye uhusiano wa mapenzi ya  jinsia moja nchini Marekani watendewe haki na jamii kwa kutambua  uhusiano huo, lakini amekuwa akipitia kile anachokiita mabadiliko ya kimtazamo kuhusu suala la ndoa za jinsia moja.
Kwa kauli hii Obama anakuwa rais wa kwanza wa  Marekani kuunga mkono ndoa za jinsia moja, suala ambalo limeleta  mgawanyiko miongoni mwa raia wa Marekani. Kumekuwa na maoni tofauti  miongoni mwa Wamarekani kuhusu kuunga mkono ndoa za aina hii.
Rais Obama anasema amejadili suala hilo na  familia, marafiki na majirani kwa muda mrefu na kutilia maanani  wafanyakazi wenzake na askari ambao wamejikita katika uhusiano wa  mapenzi ya jinsia moja.
Hatimaye amekuja na hitimisho kwamba ndoa zilizozoeleka hazikidhi matarajio ya wote.
Mpinzani wake katika uchaguzi wa rais wa mwaka  huu, Mitt Romney, wa chama cha Republican amesema bado anabakia kupinga  ndoa za watu wa jinsia moja.
Amesema wakati akiunga mkono ndoa ambazo  hazijatambuliwa kisheria, kwa maoni yake, suala la ndoa za kawaida ni  jambo lingine tofauti na hizo ndoa za jinsia moja.
Kauli ya Bwana Obama, imekuja siku moja baada ya  jimbo la North Carolina kupitisha mabadiliko ya katiba ya jimbo hilo,  yanayofafanua kuwa ndoa ni muungano tu kati ya mwanaume na mwanamke.

No comments:
Post a Comment