
Na Tiganya Vincent- MAELEZO- Dar es salaam
Katibu  Mkuu wa Wizara ya Fedha Ramadhan Khijja amesema kuwa Serikali  itaendelea kukiwezesha Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) ili kiendelea  kuzalisha wataalam mbalimbali watakaochangia kuleta maendeleo nchini.
Khijja  ametoa kauli hiyo jana jijini Dar es salaam mara baada ya kuzindua  maadhimisho ya miaka 40 tangu Chuo hicho kilipoanzishwa mwaka 1972 kwa  lengo la kuzalisha watalaam wa kada mbalimbali.
Alisema  kuwa Chuo hicho kimeendelea kuwa muhimu katika kuwaendeleza vijana na  hata watumishi waliopo kazini na hivyo kuboresha kada mbalimbali ikiwemo  elimu juu ya masuala ya bima na fedha.
Hivyo  ametoa wito kwa wazazi kuendelea kuwapeleka watoto wao katika Chuo  hicho kwa ajili ya kupata utalaam ambazo utawasaidia wao binafsi na  Taifa kwa ujumla.
Khijja alisema katika ya sasa ni vema wazazi wakawapatia watoto wao elimu kwani ndio itakayowakomboa.
No comments:
Post a Comment