ABIRIA na dereva wa gari aina ya Toyota 
Hiace yenye namba za usajili T224 ADZ inayofanya safari zake kati ya 
mjini Morogoro na Bigwa,  leo mchana wamenusurika kuungua kwa moto baada
 ya gari hilo kushika moto eneo la  mlima wa Kwa Mnyonge jirani na 
kiwanda cha mifuko ya nailoni cha Ladwa. 
Moto huo ulizimwa na Wasamaria Wema kufuatia tukio hilo ambapo dereva aliwahi kuzivua nguo zake zilizokuwa zimeanza kushika moto ulioanzia kwenye injini. Dereva huyo hakupata madhara yoyote.
Moto huo ulizimwa na Wasamaria Wema kufuatia tukio hilo ambapo dereva aliwahi kuzivua nguo zake zilizokuwa zimeanza kushika moto ulioanzia kwenye injini. Dereva huyo hakupata madhara yoyote.
 
No comments:
Post a Comment