Wednesday, December 12, 2012

CAPITAL ONE CUP: BRADFORD CITY 1 vs ARSENAL 1,(PENATI 3-2) QUARTER - FINAL. ARSENAL YATUPWA NJE NA TIMU YA DARAJA LA PILI!!, BRADFORD YAINGIA FAINALI KWA HISTORIA KUBWA!! MZEE WENGER HOI!!

Kikosi cha Wenger ambacho kina ukame wa miaka saba ya kukosa taji lolote waliokuwa wamepangwa na timu hiyo ya daraja la pili katika michuano hiyo huku wao wakipewa nafasi kubwa ya kutinga hatua ya nusu fainali. Leo usiku kikosi hicho alichopanga mzee Wenger kimeshindwa kusonga hatua ya nusu fainali baada ya kufungwa na Bradford City kwa mikwaju ya penati.Kocha wa Arsenal Arsene Wenger akikatiza kuelekea sehemu ya Arsenal uwanjani hapo Bradford
Goli la Bradford limefungwa na Garry Thompson dakika ya 19 kipindi cha kwanza baada ya kupata mpira uliokoswa koswa katikati na wa frii kiki na hatimaye kuifungia timu yake goli.
Kipindi cha pili kilipoanza bado Bradford walikuwa awajakata tamaa na kushiba goli hilo moja, wakazidi kuendeleza mashambulizi na kukosa kosa magoli  kwenye goli la Arsenal.Wachezaji wa Bradford City wakipongezana baada ya kufunga goli dakika ya 19.

Nathan Doyle (kushoto) akimjambua mchezaji wa Arsenal Santi Cazorla
Pia kipindi  cha pili Arsena wamepata nafasi za kufunga wakakosa, Gervinho amepata nafasi nyingi za kufunga ingawa ameshindwa kuonesha cheche zake kuzifumania nyavu za Bradford
Dakika ya ya 88 Cazorla anapiga cross na mchezaji Thomas Vermaelen anatupia kwa kichwa na kufanya 1-1 zinaongezwa dakika 4 za nyongeza.
Mpira unaisha dakika 90 na wanaongezewa tena muda wa dakika 30. Mashambulizi ya Arsenal kwa Bradford City yanaongezeka kwa kuwa Bradford wamerudi nyuma kulinda.
Dakika 15 za kipindi cha kwanza katika dakika 30 zinakatika bila kufumgana na wanaendelea kumalizia dakika 15, Cazorla anajaribu kutupia lakini mpira unagonga mwamba, na mashuti mengine yanakuwa hayana macho yanatoka nje.mzee wenger alionekana kama anamashaka ya kushinda leo 

Muda unaisha wa dakika 30 inaongezwa dakika 1 nayo inaisha, mikwaju inafata..
Bradford wanaanza kupiga penati ...1,2,x,4,x  = 3
Arsenal wanafatia kupiga penati .... .x,2,3,4,= 2
wenye akili zao wakishangilia.....

VIKOSI
Bradford: Duke, Darby, Meredith, McHugh, McArdle, Thompson (Jones 72), Atkinson (Turgott 92), Jones, Doyle, Hanson, Wells (Connell 74)
Subs not used: McLaughlin, Good, Ravenhill, Hines
Goal: Thompson 16
Booked: Wells, Doyle
Arsenal: Szczesny, Sagna, Mertesacker, Vermaelen, Gibbs, Wilshere, Ramsey (Rosicky 69), Cazorla, Coquelin (Chamakh 60), Podolski (Oxlade-Chamberlain 69), Gervinho
Subs not used: Mannone, Squillaci, Jenkinson, Arteta
Goal: Vermaelen 88
Booked: Gervinho, Vermaelen
Referee: Mike Dean
Attendance: 23,971

No comments: