Thursday, November 29, 2012

KIFO CHA AJALI CHA SHARO MILIONEA KIWAEPUKE WASANII WENGINE



Sharo Milionea enzi  za uhai  wake
Baadhi ya watu wakiliangalia gari aina ya Toyota Harrier lenye namba za usajili T 478 BVR alilokuwa akiendesha msanii wa filamu na muziki Hussein Ramadhani Mkieti ‘Sharo Millionea’ kutoka jijini Dar es salaam kuelekea Kijijini kwao Lusanga Wilaya ya Muheza  mkoa wa Tanga. Sharo Millionea alikufa papo hapo na mwili wake kuhifadhiwa Hospitali ya Teule Muheza Tanga.

Gari aina ya Toyota Harrier lenye namba za usajili T 478 BVR alilokuwa akiendesha msanii wa filamu na muziki Hussein Ramadhani Mkieti ‘Sharo Millionea’ kutoka jijini Dar es salaam kuelekea Kijijini kwao Lusanga Wilaya ya Muheza  mkoa wa Tanga. Sharo Millionea alikufa papo hapo na mwili wake kuhifadhiwa Hospitali ya Teule Muheza Tanga.
Wakati  bado  watanzania  wakiwa katika majonzi  na maombolezo ya  kifo cha msanii maarufu nchini Hussein Ramadhan  a.k.a Sharo Milionea ,wadau wa mtandao  huu  wa www.fourwaysbukobablogspot.com  wametoa tahadhari kwa wasanii  maarufu hapa nchini na pamoja na watu maarufu  kuacha kutafuta  kifo kama kilichomkuta  Sharo Milionea.
Wadau  hao  wamesema  kuwa  kifo cha Msanii  huyo ni sawa na kifo cha kukitafuta  mwenyewe  kutokana na kushindwa  kutafuta  dereva  wa  kumwendesha na badala yake  kuifanya kazi hiyo ya udereva  huku akitambua  kuwa hana ujuzi  wa  kutosha wa kuifanya kazi  hiyo.
Kwani  wamedai  kuwa mbali ya kuwa bado hakuna anaeelezea  chanzo cha  kifo cha Msanii  Sharo Milionea  ila uchunguzi  wa awali  unaonyesha  taili moja  wapo la gari yake  lilipasuka na kupelekea gari hilo  kuhama njia na kupinduka mazingira ambayo yanaonyesha  wazi  kuwa Sharo alikuwa katika mwendo mkali na hakuweza  kulimudu gari lake.
Hata  hivyo inasadikika kuwa katika fani  hiyo ya udereva Msanii  huyo kama ameingia  siku  za hivi karibuni baada ya  kuibuka na umaarufu na kuamua kununua usafiri  wake wa  kutembelea.
Hivyo  wamedai  kuwa  iwapo angekuwa na dereva wa  kumwendesha basi yawezekana ajali isingemkuta ama hata kama ingemkuta basi yawezekana uhai  wake  leo usingepotea.
Uchunguzi  uliofanywa na mtandao  huu  umebaini  kuwa  wasanii  wengi   maarufu hapa nchini  hawajapitia kozi za udereva na pindi  wanapopata  fedha  wanakimbilia  kununua
Wapo  wasanii  wengi ambao siku  za hivi karibuni  wamepata kununua magari yao na  hivyo bila  kuchukua tahadhali kwa  kutafuta madereva upo uwezekano wa ajali kama  hizi  kuendelea  kutokea .
Hivyo  kuna haja ya  askari  wa usalama barabarani  kunusuru maisha ya  wasanii  wetu na  watu maarufu hapa nchini ambao  wanaendesha magari yao  kuwabana ili kuonyesha leseni zao na vyeti vya vyuo ambao wamesomea udereva.

No comments: