Na: Mwandishi wetu.
KATIBU
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Abdulrahaman Kinana, amewataka
mawaziri wa Serikali ya awamu ya nne kufanya kazi kwa kasi ili
kutekeleza ilani
ya uchaguzi kwani wakishindwa kufanya hivyo watawajibishwa na
chama.Alisema chama hakitawavumilia mawaziri ambao hawatekelezi majukumu
yao na
kukifanya chama hicho kichukiwe na wananchi.
Alisema
kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) mawaziri watakuwa wakitoa
taarifa za utendaji kazi na kwamba wajumbe wa Nec watawabana kwa maswali
ili
kupata ufafanuzi wa kina katika masuala mbalimbali ya wizara zao.Alisema
kila waziri, mbunge na Diwani anayetokana na chama hicho atakuwa
akipimwa utendaji wake katika kuwahudumia wananchi wa eneo lake na taifa
kwa
ujumla.
Kinana alisema hakuna kiongozi yeyote wa Serikali aliyejuu ya chama hicho
bali chama kipo juu yao na ni wajibu wao kuwa watiifu kwa chama na wananchi
wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yao.
“Naomba ieleweke kwamba CCM imejipanga katika kuwaunganisha na kuwahudumia
Watanzania, hivi sasa tunaanza utaratibu mpya ambapo mawaziri watakuwa wakitoa
maelezo.
Alisema kama kuna kiongozi ambaye ataona kuwa kasi yetu ni kubwa ni bora
akaachia ngazi.
Akizungumzia makundi ndani ya chama hicho , Kinana alisema kuwa tangu ulipomalizika uchaguzi wa ndani kuna baadhi ya viongozi walioshindwa wamekuwa wabinafsi kwa kutochaguliwa katika nafasi za uongozi hali inayowafanya kujiona bora kuliko wengine.

Alisema kutokana na hali hiyo kuna baadhi ya makada wa CCM wamekuwa wabinafsi
huku wakiibuka na sababu mbalimbali ikiwamo rushwa.
“Watu wamekuwa wabinafsi kwa kukosa nafasi za kuchaguliwa ndani ya chama.
Kama hakupita anaibuka na sababu lukuki na hata kudai aliyechaguliwa hafai bali
yeye ndiye anayefaa,” alisema.
Kinana akizungumzia utendaji kazi wa mawaziri alisema kuanzia kikao kijacho
cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, watakuwa wakitoa taarifa hizo ambapo
wajumbe wa NEC watawabana kwa maswali na kuhitaji ufafanuzi wa kina katika
masuala mbalimbali ya wizara zao.
Alisema kila Waziri, Mbunge na Diwani anayetokana na chama hicho atakuwa akipimwa utendaji wake katika kuwahudumia wananchi wa eneo lake na Taifa kwa ujumla.
Alisema kila Waziri, Mbunge na Diwani anayetokana na chama hicho atakuwa akipimwa utendaji wake katika kuwahudumia wananchi wa eneo lake na Taifa kwa ujumla.
Alisema hakuna kiongozi yoyote wa Serikali aliyekuwa juu ya chama bali chama
kipo juu yao na wajibu wao kuwa watiifu kwa chama na wananchi wakati wote wa
utekelezaji wa majukumu yao.
“Ninapenda ifahamike sasa CCM, imejipanga katika kuwaunganisha na kuwahudumia
Watanzania, hivi sasa tunaanza utaratibu mpya ambapo Mawaziri watakuwa wakitoa
taarifa zao katika vikao vya NEC na kuhojiwa maswali na wajumbe.
“Kila Waziri atahojiwa utendaji wa shughuli za Serikali katika Wizara yake na utekelezaji wa ilani na ikiwa kuna atakayeonekana kuwa hafai hatua zitachukuliwa stahiki zitachukuliwa.
“Kila Waziri atahojiwa utendaji wa shughuli za Serikali katika Wizara yake na utekelezaji wa ilani na ikiwa kuna atakayeonekana kuwa hafai hatua zitachukuliwa stahiki zitachukuliwa.
No comments:
Post a Comment